Wewe unaamini bila ya CCM kuwepo hakuna Tanzania?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,260
33,857
Kutokana na mambo mbali mbali yanayotokea kwenye siasa za nchi yetu nimeona niulize hili swali.

Wewe kama Mtanzania mwenye akili timamu unaamini kuwa bila ya Chama Cha Mapinduzi kuwa madarakani nchi ya Tanzania haitakuwa salama. Kwa nini unaamini hivyo?
 
Itakuwa salama endapo hawa MaCCM yakikubali kushindwa maana wao ndio watakuwa chanzo cha machafuko endapo wasipokubali kushindwa
 
Itakuwa salama endapo hawa MaCCM yakikubali kushindwa maana wao ndio watakuwa chanzo cha machafuko endapo wasipokubali kushindwa
Hawajawahi kuwaza iko siku watashindwa, na hata wakishindwa hawataamini kama wameshindwa!
 
Kutokana na mambo mbali mbali yanayotokea kwenye siasa za nchi yetu nimeona niulize hili swali.

Wewe kama Mtanzania mwenye akili timamu unaamini kuwa bila ya Chama Cha Mapinduzi kuwa madarakani nchi ya Tanzania haitakuwa salama. Kwa nini unaamini hivyo?

FB_IMG_1509843520041.jpg
 
Kwanza kabisa umeshafika Libya,Congo ya Kabila,Uganda,Rwanda,Burundi,Central africa,umeshiba pilauukoloni mambo leo haujawahi waacha watu salama
 
Kutokana na mambo mbali mbali yanayotokea kwenye siasa za nchi yetu nimeona niulize hili swali.

Wewe kama Mtanzania mwenye akili timamu unaamini kuwa bila ya Chama Cha Mapinduzi kuwa madarakani nchi ya Tanzania haitakuwa salama. Kwa nini unaamini hivyo?
Hii nchi ni kubwa kuliko CCM.CCM itapita ila Tanzania itabaki
 
Bila CCM Tanzania itasonga,tena yaweza kuwa maradufu ya sasa.

Tena itasitawi vyema,kwani ile laana ya unafiki wa kijamaa itakuwa imekwisha.

Kwani hao wana CCM ni akina nani,kama siyo wajomba zetu,baba na mama zetu tuliochangia nao damu ila tukatofautiana nao tofauti za kiitikadi tu!

Serikali itakuwepo,Tanzania pia itakuwepo kesho au kesho kutwa haijalishi kashinda CHADEMA au hao CCM.

Swali pekee la kujiuliza ni:Je CCM wameshajiandaa na wataridhika kuishi kama Chama bila ya Dola?
 
Kama hakipo basi nitaanzisha chama changu na naamini nilivyo nitapata wanachama wengi nchini kupita hata waliopo CCM. Na chama changu kitaongoza nchi hii vizuri kuliko

Eeeeh nitakuita nawe upate cheo chako... au bado hutaki chama..eeeh
Nitaanza kuvuta vichwa vya JF hata wale walio kimya miaka hii kwa kutambua nondo zao enzi hizo yaani miaka hiyo iliyopita..

Kwa nguvu ya pamoja nikiwa mwenyekiti ni kishindo cha historia.. tutamzidi Magu kwa sababu miaka usogea mapya utokea kwa kwenda na wakati na kusoma mengi.. na mengine atakuwa ameyaweka sawa pia..

Eeeeeeeh
Nimeandika halafu nimechekelea..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom