Wewe ulikuwepo Kariakoo wakati wa kizaazaa!?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Wengine tulifuatilia hapa JF, wengine kwenye TV, wengine kwenye Redio, lakini labda wewe ulikuwepo Kariakoo ukiona matukio yote "Laivu" hebu tumwagie jinsi watu walivyokuwa wana kihoro, wezi walifanya nini, maeneo ya Kariakoo Sokoni palikuwaje, vipi wanazi wa Simba walisimama kuhami jengo lao au na wao walitimua mbio kama farasi asiye na muongozaji?

Wanajeshi walipofika Kariakoo watu waliwashangilia au waliwazomea, wananchi wa kawaida ambao walikuwa hawana upande kwenye ile kasheshe walikuwa wana maoni gani!? ulitumia mchina wako kupiga picha au mabomu yalikutoa machozi hadi njia ukawa huioni?

Wewe ulikuwepo Kariakoo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom