Brownj
Senior Member
- May 8, 2017
- 139
- 80
Tunaishi na watu tunaamini katika watu, kila mtu amefika alipo kwasababu ya uwepo wa watu wengine. Humu kwenye jukwaa naamini kuna watu wengi sana wenye fikra, mawazo, upeo, elimu, busara, ujuzi na mafanikio tofauti tofauti hivyo tuungane pamoja kama ndugu kushirikiana na kushauriana kwani mmenijenga sana hasa nyakati za changamoto mbalimbali.
Ngoja nieleze kwa ufupi unaoeleweka maana siwezi kusema yote kwa kuandika hapa nitatumia wiki nyingi sana. Nimekusanya pesa kiasi cha mil1 naombeni ushauri nifanyie nini ili izalishe nifanye biashara gani ndugu zangu au kama kuna mtu ataona inafaa kushirikiana katika wazo analoliamini ni productive basi ni jema pia tukafanya wote ubia japo sina elimu sana juu ya biashara ila napenda sana.
Elimu yangu ni kidato cha sita nimesoma kwa msaada wa walimu wenyewe na baadhi ya marafiki kwani wazazi wangu hawajiwezi kabisa nilishaanza kusoma chuo lakini sikuweza kuendelea mara baada ya semester ya pili kuanza kwa sababu za kiuchumi nawashukuru baadhi ya ma lectures na utawala kwa ujumla walinisapot sana ikafika hatua baada ya kuona loan board bado hawaingizi pesa basi nikapostpone masomo nikaingia mtaani kusaka pesa.
Sasa naogopa kurudi tena chuo maana baada ya hii pesa kuisha nitarudia taitzo lilelile Lakini pia nitumie nafasi hii kuomba kama kuna mdhamini anaweza kunidhamini nipo tayari kwani napenda sana kusoma tena sana lakini umaskini imekua kikwazo sana kwangu. Nimesoma PCB advance lengo langu la kuwa daktari bado lipo moyoni naamini nikitengeneza pesa kupitia biashara au nikipata mdhamini nitarudi chuo tu.
Nipo Dar Mbezi karibuni wakuu kwa maswali maoni na ushauri