Wewe ni mtu muhimu sana kwangu ndio maana nimetenga muda wangu kuongea na wewe

AMEN

Member
Feb 25, 2014
10
20
Ewe mwanadamu uliyepata nafasi ya kusoma huu ujumbe.Jua ya kwamba mimi nakutakia mema.Hunijui sikujui ila nacho jua ya kwamba wote tuna Baba mmoja Adam na Mama Mmoja Hawa.Tunaishi kwenye Dunia hii Tukiwa na Lengo la kuishi MAISHA MAZURI NA BORA kwenye ulimwengu huu wa sasa na Maisha bora zaidi kwenye ulimwengu ule ujao. Upendo nilionao kwako ewe Mwanadamu ndio ulio nisukuma kuwasiliana nawe.

Hii dunia ya sasa Watu wanao ishi ndani yake wanasumbuliwa sana tatizo la kusikia Mawazo ya ovyo yanayo onekana kama mazuri lakini kumbe ndani yana haribu tabia nzuri ya Mtu.Jambo hili limepelekea kuwepo kwa watoto ,vijana,wa baba, Wa mama wenye tabia za ajabu.Mawazo haya yasiyo faa yana ingizwa kwa nguvu kwenye akili za Watu kwa njia ya matumizi mabaya yasiyo zingatia maadili ya mitandao ya kijamii, nyimbo mbaya,miziki mibaya ,movie mbaya picha mbaya, Matangazo mabaya.Na ndoto mbaya hasa wakati wa usiku.
Hivyo basi mtu asipo tenga muda wa kutosha wa kusafisha akili yake inapelekea yeye KUPUNGUKIWA UWEZO WA KUCHUKUA MAAMUZI MAZURI.

Mtu anapo pungukiwa uwezo huu muhimu wa KUCHUKUA MAAMUZI MAZURI .Yeye mwenyewe anakuwa hajui anaona maamuzi anayo chukua ni sahihi na ni maamuzi yake . Kumbe siyo .Hayo maamuzi kapandikiziwa bila yeye kujua.

Yeye anaona kawaida tu kumbe akili yake imesha wekewa vitu vigeni au magugu bila Yeye kujua.Hii inapelekea mtu kuishi maisha ambayo sio yake au maisha fake .Anaishi maisha ya yule aliye mpandikizia vitu vigeni ndani ya akili yake .

Hivyo inampasa mtu kutenga muda wa kutosha wa kusafisha akili yake ili asije kujikuta kapandikiziwa Mawazo yasiyo faa bila kujua.

ENYI WANADAMU MNAO SOMA MAKALA HII MJITAHIDI KUEPUKA MAMBO YOYOTE YALE YANAYO SABABISHA KUPANDIKIZIWA MAWAZO YASIYO FAA( UN WANTED MIND) KWENYE AKILI ZENU.

Safisha akili yako kwa kutenga muda wa kujionya pamoja na kusoma au kusikiliza KITABU CHENYE MANENO YA KWELI,MASAFI NA MUHIMU NA YENYE NGUVU YA KUBADILISHA MAISHA YAKO soma na tafakari kwa bidii ,soma au sikiliza sauti ya kitabu hiki usiku na mchana .

Soma kwa bidii kubwa na kwa mpangilio maalumu kwa kufanya hivyo itapelekea wewe kuwa na uwezo wa kuona Mawazo yasiyo faa (Un wanted Mind) yanayo onekana kama mazuri kwa nje Kumbe ndani ni machukizo makuu ya uharibifu na kisha kuyaepuka haraka sana kabla hayaja tekelezwa.

Pia Tenga muda wa kutosha wa kuwasiliana na yule aliye kuleta huku Duniani.Tenga muda wa kutulia na kukagua na kuepuka mambo yote yanayo pelekea uvamiwe na Mawazo mabaya kisha yaepuke hayo.

Asante na nakutakia siku njema.
 
Back
Top Bottom