Wewe ni mshindi siku zote. Usiruhusu changamoto unazopitia zikubadilishe mtazamo

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
"Kwenye safari ya maisha kuna mambo magumu yanaweza kukufanya uhisi kuchoka na usitamani tena kuendelelea na safari ya kuyaelekea mafanikio uliyoyatazamia, na hii yote inasababishwa na ugumu fulani unaoweza kukutana nao kwenye eneo ulilopo."

"Sikia ndugu yangu watu wengi sana wanapokutana na changamoto za kimaisha wamekuwa ni watu wa kuchoka na kujiona hawawezi tena kuyafikia mafanikio yao, nawe pia yawezekana ni miongoni mwao."

"Napenda nikusihi na kukuhamasisha ya kuwa USICHOKE katika hali uliyopo maana kama ukiruhusu kuchoshwa na hayo magumu unayokutana nayo fahamu hivi ya kuwa hautaweza kuyafanyia kazi kwa ufanisi yale mambo yatakayochangia wewe kupata mafanikio."

"Kwani kuna mazingira Mwenyezi MUNGU atakuaminisha ya kuwa anaweza kukuvusha ila kwa sababu ya kuchoka kwako hautaweza kuyachuchumilia yaliyo mbele yako kwa wakati ujao maana tayari moyoni mwako utakuwa ushakata tamaa yaani hiko hivi kuchoka ni ishara ya kukata tamaa."

"Ni kweli umefungua biashara ila haupati faida nakusihi usichoke endelea kutafuta mbinu bora za kuikuza biashara yako huku ukimwomba Mwenyezi MUNGU, na pia ni kweli unasoma sana ila matokeo yako darasani ayaridhishi hii hali isikufanye uchoke kwani tambua bado unaweza kufanikiwa kwa sababu Mwenyezi MUNGU yupo nawe."

"Na tena yawezekana una mipango mizuri ya kimaisha ila changamoto ipo ni wapi upate pesa na hali hii imekutia uchovu na kukufanya uchoke sikia nakusihi usichoke bado una nafasi ya kubadili hali yako ukafikia mafanikio yako, Katika yote fahamu hivi ukiruhusu kuchoka na ukakata tamaa hautaweza kuziona fursa za kimaendeleo na pia hautaweza kumwomba Mwenyezi MUNGU kwa ufanisi na kwa ujasiri katika imani isiyo na shaka wala wasiwasi."

"Ndugu yangu ni kipi hakijakaa sawa kinakufanya uchoke ndani mwako na umeruhusu nafsi yako kuinama, pole, usichoke tambua ya kuwa wewe ni wa thamani mbele za Mwenyezi MUNGU, katika hali zote unazopitia yeye yupo nawe, yaani atakutia nguvu na utasimama tena katika upya wa maisha yenye furaha na amani huku ukimtukuza yeye katika Kristo Yesu."

"Fahamu hivi ndugu yangu unayehisi kuchoka ya kuwa Mwenyezi MUNGU anakuwazia mema siku zote na mawazo yake kwako ni ya AMANI (Yeremia 29:11) na ni ya kukupa tumaini siku zako za mwisho, tambua hivi wewe ni mshindi siku zote na wala usiruhusu changamoto unazopitia zikubadilishe mtazamo na ukaanza kujiona hauwezi kufanya makubwa."

MUNGU ANAKUPENDA, USICHOKE UNAWEZA KUFANIKIWA

FB_IMG_1633041599595.jpg
 
Back
Top Bottom