Wewe ni mpenzi wa Movies? (Session 05). Tupia jicho hapa..

SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
8,413
23,712
Niaje, wakuu? Kama kawaida tunakutana katika mfululizo wetu wa tano sasa wa kugusiana filamu kuhamasishana kuzitazama na kuzielewa.

Bila maneno mingi, na tuanze. Karibu.

IDENTITY ya 2003.

InShot_20200614_225758162.jpg

Kuna watu wanaamini hamna kitu kinachotokea duniani kwa bahati mbaya. Kila kitu kimepangwa na kipo kwa ajili ya lengo fulani mahususi. Kuanzia huyo uliyenaye kwenye mahusiano mpaka wale unaokutana nao barabarani. Kazini ulipo mpaka mahali unapokaa.

Je, wewe unaamini vivyo?

Basi ipo hivi, wakati kesi moja matata ya mauaji inayomkabili bwana mmoja kwa jina Malcom ikiwa inaskizwa, inabainika kulikuwa na tatizo katika uendeshaji wa kesi hiyo kwani kuna baadhi ya nyaraka ambazo zilikuwa zikionyesha kuwa mtuhumiwa huyo ana matatizo ya akili hazikuwamo ama tuseme zilifichwa kwa makusudi (kama ambavyo mwanasheria wa mtuhumiwa alivyokuwa akiamini).

Hivyo kutokana na ushahidi huo kuonekana kwa kukawia, kesi ikabidi isogezwe mbele kidogo kwa ajili ya uskilizaji mpya kwa kuzingatia nyaraka hizo.

Wakati hayo yakiendelea, watu kumi wasiojuana wanakutana kwenye moja ya ‘Motel’ kwa kujihifadhi kutokana na hali mbaya ya hewa – kulikuwa na mvua inayoambatana na upepo mkali sana! Miongoni mwa watu hao alikuwapo dereva aliyekuwa anamwendesha mwigizaji maarufu wa vipindi vya televisheni, wazazi waliokuwa wameambatana na mtoto wao wa kiume, polisi anayemsafirisha mtuhumiwa hatari wa kesi za mauaji, msichana mmoja malaya na ‘couple’ changa iliyoingia kwenye ndoa hivi karibuni.

Kutokana na barabara kufurika maji, hamna njia inayoingia wala kutoka, watu hawa wanalazimika kutumia usiku wao hapa, lakini si punde makazi haya yanageuka kuwa tafarani kubwa baada ya mauaji ya ajabu kuanza kujiri huku muuaji asijulikane ni nani! Mtu mmoja baada ya mwingine anauawa na kando yake inakutwa ufunguo uliotiwa namba zenye kufuatana.

Wakiwa wanahaha kujua ni nini kinachoendelea hapa, wakabaini kuwa moteli hiyo ilikuwa imejengwa karibu na makaburi ya wahindi wekundu (Red Indians), hivyo wakaanza kudhani pengine kuna nguvu za kishirikina zinafanya kazi kwenye mauaji hayo.

Kule kwenye kesi ya mauaji ya bwana Malcom, shauri likasikizwa upya, na kutokana na nyaraka zilizoonyeshwa na pia ushahidi wa daktari wa akili, mtuhumiwa bwana Malcolm anabainika kuwa na matatizo fulani ya ubongo yanayopelekea kuwa na uwezo wa kujinyumbulisha kwenye nafsi kumi na moja za binadamu tofauti!

Nyaraka ambayo iliwasilishwa ilikuwa na diary yake ambayo ndaniye kulikuwa na mawazo tofauti tofauti yaliyoandikwa miandiko tofauti kabisa kana kwamba ni watu tofauti walioandika. Hapo mwanasheria wa Malcom anatoa hoja kuwa mauaji yaliyofanyika, bwana Malcom hayajui wala kuyatambua kwa lolote lile.

Yani kwa ufupi ni kwamba, japo mwili ni wa Malcom ndio ambao umebainika kushiriki kwenye mauaji kadha wa kadha lakini ulikuwa katika nafsi ya tofauti, kila nafsi ina matendo yake … matendo ambayo hakuna nafsi nyingine inayoyajua ama kuyaelewa!

Sasa tukirudi kule moteli, bado mauaji yanaendelea … na kama kawaida kwenye kila mojawapo inabainika funguo yenye namba. Na kama haitoshi, siri za kila mmoja aliyepo hapo zinaanza kuwa bayana. Siri za ndani. Siri ambazo zinaanza kutuaminisha kuwa watu hawa hawakuwapo hapa kwa bahati mbaya bali kwa sababu.

Je, ni siri gani hizo? Na ile kesi inayoendelea mahakamani kumhusu bwana Malcom na nafsi zake kumi na moja ina mahusiano gani na mauaji haya? … Je, anayeua wenziwe ni nani na kwanini kwenye kila mauaji anaacha funguo yenye namba?

Na nafsi kumi na moja za bwana Malcom ni zipi haswa?

Tuliza kichwa, enjoy kazi hii!

CLOSE ya 2019.

InShot_20200614_225736627.jpg

Bila shaka ushawahi tazama movie maarufu ya ‘The Bodyguard from Beijing’ ya bwana Jet Li. Mbali na hiyo kuna hizi hapa zenye mahadhi kama hayo, My Beloved Bodyguard (2016), Iron Protector (2016) na The Hitman’s Bodyguard (2017) kwa uchache tu kwani filamu hizi zipo nyingi sana.

Lakini utofauti wake ni hii ni kwamba, humu ndani Bodyguard ni mwanamke … mwanamke wa shoka haswa, lakini si kama wale wa kina SALT na UNDERWORLD. Huyu unaona kabisa ubinadamu wake zaidi kuliko u-superhuman, na hiko ndo kinafanya filamu hii kuwa tamu.

Let’s get down to the point!

Mwanamke aitwaye Sam Carlson ana rekodi nzuri ya kuwa mlinzi wa karibu ambapo karibuni tu alionyesha umahiri wake kwenye zoezi la kuwaokoa waandishi wa habari wawili ndani ya nchi ya Sudani kusini pale walipovamiwa na genge hatari la wazawa.

Kutokana na hayo, mwanamke huyu anaukwaa kazi mpya ya kumlinda binti aitwaye Zoe ambaye si muda mrefu baba yake, bilionea Eric, alikufa kutokana na matatizo ya moyo akamwachia mwanae hisa zake zote za kampuni, kitu ambacho kilimkwaza sana mama yake wa kambo, kwa jina Rima, ambaye alitaraji angelipatiwa yeye ukizingatia ni familia yake ndiyo ilivumbua kampuni hiyo iliyokuwa inaendeshwa na bwana Eric.

Rima ndo’ CEO wa kampuni lakini alitaka zaidi na zaidi, na hata ndo yeye aliyemwajiri Sam kumlinda Zoe baada ya kuona bodyguard mwanaume ataleta matata kama aliyepita kwa kumshuku kuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti Zoe.

Basi kazi inakuja pale ambapo Rima anamshawishi Zoe kwenda nchini Morocco kutazama nyumba yao ingali wakiwa wanas’kilizia dili fulani la madini la pesa ndefu. Wakiwa huko, mbali na nchi yao mama, ndipo mashambulizi yaso na idadi yanaanza kumuandama Zoe huku Sam akiwa na mtihani mkubwa wa kuonyesha umahiri wake kazini. Ubaya zaidi ni kwamba hata polisi wa nchi hiyo ngeni nao wapo upande wa wauaji kiasi kwamba kunakuwa hakuna pa kukimbilia wala wa kumuamini!

Katika sekeseke hilo, Zoe anajikuta akimuua mmoja wa polisi na habari zinasambaa kwenye vyombo vya habari na kuanza kuathiri kampuni yao kiasi kwamba kampuni shindani inayoitwa Sikong inafanikiwa kuteka lile dili la madini, lakini vilevile sura za wahusika zikatapakazwa kwenye vyombo hivyo vya habari wakinadiwa kama watu wanaosakwa kwa uhalifu!

Sasa kazi inakuwa kubwa kwa mlinzi Sam. Anadhamiria kumsafirisha Zoe ndani ya nchi hii ambayo imegekuwa kuwa sifongo watorokee Spain, lakini wataanzia wapi ukizingatia hata ‘passport’ hawana achilia mbali sura zao zinatambulika wakitafutwa na maadui na wanausalama kwa pamoja?

Na je, mtu anayehusika na haya mashambulizi ni nani haswa? Rima, mama wa kambo wa Zoe? Kama ndio, ni mali tu ndo zamtoa roho ama kuna kingine? … kama si yeye, ni nani haswa yupo nyuma ya yote haya? … utastaajabu.

THE SIEGE OF JADOTVILLE ya 2016.

InShot_20200614_225747211.jpg

Achilia mbali 13 HOURS: Secret soldiers of Benghazi, DUNKIRK na 7 DAYS IN ENTEBBE ambazo ni misheni za kweli za kijeshi zilizowahi kutokea, kuna hii pia ambayo imesahaulika na utamu wake. Filamu ambayo sio tu inakuburudisha bali inakufundisha pia sehemu fulani ya historia ambayo inapuuzwa ama kusahaulika.

Ipo hivi … katika miaka hiyo ya 1960’s, kunatokea mauaji ya waziri mkuu wa Congo, bwana Patrice Lumumba. Kifo hicho kinapelekea mlipuko wa vita ya wenyewe kwa wenyewe kiasi cha kutishia amani ndani ya Congo haswa mashaka yakiwa katika jimbo tajiri wa madini, Katanga, ambapo huko kuna vikundi vya kijeshi vinayopigania makampuni ya uchimbaji wa madini wakishukiwa huenda wakatumia mwanya huo kama njia ya kuanzisha harakati za kuitwaa Congo.

Nyumba ya vikundi hivyo kuna mikono ya wafaransa na wabelgiji lakini pia wakiungwa mkono na baadhi ya waafrika wa Katanga. Waziri mtawala wa jimbo la Katanga, bwana Moise Tshombe anahaha. Kutokana na zogo hili, kiongozi wa Umoja wa mataifa (UN), anaona kuna uwezekano mgogoro huu ukapeleka kutokea kwa vita ya tatu ya dunia hivyo anaamua kuchukua hatua kukabili tatizo kama maji hayajafika shingoni.

Anatuma kikosi kidogo cha kutunza amani cha wanajeshi wa Ireland ambao wanaenda kuweka kambi katika kitongoji cha Jadotville (kwa sasa kinaitwa Likasi) ndani ya Katanga. Wakati huohuo, afisa wa UN, Dr. Conor, anaanzisha misheni ya kivita ‘Operation Morthor’ dhidi ya vikundi vya kifaransa na kibelgiji pasipo kushirikisha kikosi hichi cha wa Ireland.

Matokeo yake wanakufa wana-Katanga thelathini, na kupelekea kuzuka kwa vita baina ya vikosi vya wana-Katanga wakiwa wanaongozwa na wafaransa na wabelgiji ambao wanaanzia mashambulizi katika kitongoji cha Jadotville!

Kwa idadi wanakikundi hao walikuwa kama alfu tatu hivi, huku wanajeshi wa-Ireland wakiwa mia moja hamsini tu! Sasa je, wanajeshi hawa watatoboa dhidi ya wenyeji walioungana na mataifa yanayoinyemelea Congo na rasilimali zake? … kazi ilikuwa pevu.

Ni jasho na damu.

LOCKOUT ya 2012.

InShot_20200614_225710628.jpg

Teknolojia hubadilika kila uchwao. Karibia kila sekta inaguswa na mabadiliko haya aidha kwa haraka ama taratibu. Lakini jambo moja la kujiuliza ni je kila kinacholetwa na teknolojia hiyo, kitakuwa na mema kwetu?
Filamu hii inajulikana pia kwa jina la MS One: Maximum Security, mahadhi yake ni miaka ya mbele huko ambako teknolojia inakuwa imepevuka kuliko sasa kiasi kwamba dunia imekuwa na namna ya kujiweka salama dhidi ya wahalifu hatari zaidi kwa kuwafungia jela iliyopo angani, ambapo huko wafungwa huwekwa katika hali fulani ya pumbazo wakitumikia miaka yao yote ya adhabu mpaka kikomo chake.

Basi bwana mmoja, kwa jina Snow, ambaye ni agent wa zamani wa CIA, anajikuta matatani na serikali yake akituhumiwa kumuua agent wa CIA anayeitwa Frank ndani ya chumba fulani katika moja ya hoteli ingali kiuhalisia hakufanya hivyo. Anahojiwa kwa nguvu akilazimishwa kukiri kosa ambalo hajalifanya na haijalishi namna gani anajitetea, haaminiki. Chief wa CIA anaamini bwana huyo ndo muhusika.

Ingali hayo yakiwa yanaendelea, binti wa Rais wa Marekani, Emilie, msichana mwenye kujawa na udadisi mkubwa, anatembelea gereza la MS One ambalo lipo angani akiwa amedhamiria kwenda kufanya tafiti yake huko kuwa mahadhi hayo ambayo wafungwa wanatunziwa huwasababishia kupata matatizo ya akili.

Huenda binti huyu alisahau kuwa hili eneo linahifadhi wahalifu hatari zaidi ama alikuwa anajiamini na ulinzi wake maana haya maamuzi kwa mtu mwingine sidhani kama angelifanya, wazungu husema curiosity killed the cat, na waswahili husema mwanakulitafuta …..

Basi binti huyu akiwa katika shughuli zake huko, akajikuta matatani baada ya silaha alokuwa nayo mlinzi wake kutua mikononi mwa mhalifu ambaye anatumia nafasi hiyo kuwaweka chini ya ulinzi na kuwafungulia wahalifu wenzake huru huku binti wa Rais akiwa mashakani.

Sasa kutokana na hili jambo, chief wa CIA anachekecha kichwa na kuona ni bwana Snow tu ndiye ana uwezo wa kumkomboa binti huyo. Anamshirikisha lakini Snow anakataa. Ili kumshawishi, anamuahidi bwana Snow kuwa endapo akifanya hivyo, basi atakuwa huru dhidi ya kesi nzito inayomkabili.

Kwasababu ya kutaka uhuru wake, Snow anaingia kazini.

Vipi, atatoboa dhidi ya kundi la wahalifu hao hatari? Je, ni nani alimuua Frank, agent wa CIA mpaka bwana Snow kuingizwa matatani? … na ni nini Emilia anatakitaka haswa kwenye gereza la MS One? Atafanikiwa?

BONUS MOVIE:

INFAMOUS ya 2020.

InShot_20200614_225818637.jpg

Achilia mbali uraibu (addiction) wa vitu mbalimbali kama vile sigara, pombe na madawa, siku hizi kuna uraibu mpya na hatari – uraibu wa mitandao ya kijamii (social networks addiction). Kuna watu ni kheri walale njaa lakini sio wakose bundle wakashindwa kuperuzi instagram, whatsapp, Youtube ama Facebook!

Sasa ni kheri hao, kuna ambao wanaenda mbali zaidi ya hapo wakihakikisha wanakuwa maarufu kwenye mitandao hiyo kwa namna yoyote ile, hata kwa kukaa uchi na kujirekodi video za utupu cha umuhimu ‘followers’ na ‘comments’. Mengine baadae!

Basi ipo hivi, msichana anayeitwa Arielle, waitress wa mgahawa ndani ya mji mdogo wa Florida, ana ndoto ya kuwa maarufu haswa pasipo kujali hana ‘connection’ wala chochote kile. Akiwa katika hamu hiyo, bahati mbaya ama nzuri, anakutana na kijana aliyetoka jela si muda, kwa jina Dean, ambaye anaungana naye na kutengeneza team ya kusaka umaarufu kwa njia yoyote ile.

Walipochekecha mawazo wakaona njia nyepesi na ya haraka ya kufikia wanapopataka ni mitandao ya kijamii, huko wawe wanapost vitu vya hatari na vitata kwani ndivyo ambavyo hukamata ‘attention’ ya watu zaidi.

Sasa vitu hivyo ni ipi? Picha za uchi ama? Hapana, wao wakaona waende mbali zaidi kwa kufanya uhalifu wakiwa wanaurekodi kisha wanautuma mubashara kwenye mitandao. Kweli wazo likafanya kazi. Upesi Arielle akaanza kupata wafuasi kedekede mitandaoni, likes na comments! Roho yake ikasuuzika.

Lakini kama ilivyo kwa kula nyama za binadamu, Arielle akawa anataka zaidi na zaidi. Kila tone la umaarufu aliloupata halikukidhi kabisa kiu chake. Tamaa hiyo ikapelekea aanze kufanya matendo makubwa na hatari zaidi, kukimbizana na polisi, kufanya ujambazi na hata kuua kabisa! … kila alipokuwa anayafanya hayo akazidi kujizolea umaarufu na wafuasi, wengine wakija kustaajabu, wengine wakifurahia na wengine wakishangazwa na uchizi huu.

Njaa yake hii ya kutaka zaidi, inamtisha mpaka mpenzi wake, bwana Dean, ambaye anastaajabu ni nini mwisho wa yote haya.

Je, ni nini gharama ya umaarufu huu?

Kwa leo tuishie hapa... ukihitaji hizi movies zote na ziada nimekusogezea kwa urahisi kabisa, zama hapa kwa telegram:

Movies Na Stories

Na kule pande za youtube, nimewawekea kazi hii hapa... wewe tu ushindwe..

Niaje, wakuu? Kama kawaida tunakutana katika mfululizo wetu wa tano sasa wa kugusiana filamu kuhamasishana kuzitazama na kuzielewa.

Bila maneno mingi, na tuanze. Karibu.

IDENTITY ya 2003.

View attachment 1478803

View attachment 1478804
Bila shaka ushawahi tazama movie maarufu ya ‘The Bodyguard from Beijing’ ya bwana Jet Li. Mbali na hiyo kuna hizi hapa zenye mahadhi kama hayo, My Beloved Bodyguard (2016), Iron Protector (2016) na The Hitman’s Bodyguard (2017) kwa uchache tu kwani filamu hizi zipo nyingi sana.

Lakini utofauti wake ni hii ni kwamba, humu ndani Bodyguard ni mwanamke … mwanamke wa shoka haswa, lakini si kama wale wa kina SALT na UNDERWORLD. Huyu unaona kabisa ubinadamu wake zaidi kuliko u-superhuman, na hiko ndo kinafanya filamu hii kuwa tamu.

Let’s get down to the point!

Mwanamke aitwaye Sam Carlson ana rekodi nzuri ya kuwa mlinzi wa karibu ambapo karibuni tu alionyesha umahiri wake kwenye zoezi la kuwaokoa waandishi wa habari wawili ndani ya nchi ya Sudani kusini pale walipovamiwa na genge hatari la wazawa.

Kutokana na hayo, mwanamke huyu anaukwaa kazi mpya ya kumlinda binti aitwaye Zoe ambaye si muda mrefu baba yake, bilionea Eric, alikufa kutokana na matatizo ya moyo akamwachia mwanae hisa zake zote za kampuni, kitu ambacho kilimkwaza sana mama yake wa kambo, kwa jina Rima, ambaye alitaraji angelipatiwa yeye ukizingatia ni familia yake ndiyo ilivumbua kampuni hiyo iliyokuwa inaendeshwa na bwana Eric.

Rima ndo’ CEO wa kampuni lakini alitaka zaidi na zaidi, na hata ndo yeye aliyemwajiri Sam kumlinda Zoe baada ya kuona bodyguard mwanaume ataleta matata kama aliyepita kwa kumshuku kuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti Zoe.

Basi kazi inakuja pale ambapo Rima anamshawishi Zoe kwenda nchini Morocco kutazama nyumba yao ingali wakiwa wanas’kilizia dili fulani la madini la pesa ndefu. Wakiwa huko, mbali na nchi yao mama, ndipo mashambulizi yaso na idadi yanaanza kumuandama Zoe huku Sam akiwa na mtihani mkubwa wa kuonyesha umahiri wake kazini. Ubaya zaidi ni kwamba hata polisi wa nchi hiyo ngeni nao wapo upande wa wauaji kiasi kwamba kunakuwa hakuna pa kukimbilia wala wa kumuamini!

Katika sekeseke hilo, Zoe anajikuta akimuua mmoja wa polisi na habari zinasambaa kwenye vyombo vya habari na kuanza kuathiri kampuni yao kiasi kwamba kampuni shindani inayoitwa Sikong inafanikiwa kuteka lile dili la madini, lakini vilevile sura za wahusika zikatapakazwa kwenye vyombo hivyo vya habari wakinadiwa kama watu wanaosakwa kwa uhalifu!

Sasa kazi inakuwa kubwa kwa mlinzi Sam. Anadhamiria kumsafirisha Zoe ndani ya nchi hii ambayo imegekuwa kuwa sifongo watorokee Spain, lakini wataanzia wapi ukizingatia hata ‘passport’ hawana achilia mbali sura zao zinatambulika wakitafutwa na maadui na wanausalama kwa pamoja?

Na je, mtu anayehusika na haya mashambulizi ni nani haswa? Rima, mama wa kambo wa Zoe? Kama ndio, ni mali tu ndo zamtoa roho ama kuna kingine? … kama si yeye, ni nani haswa yupo nyuma ya yote haya? … utastaajabu.

THE SIEGE OF JADOTVILLE ya 2016.

View attachment 1478805

Achilia mbali 13 HOURS: Secret soldiers of Benghazi, DUNKIRK na 7 DAYS IN ENTEBBE ambazo ni misheni za kweli za kijeshi zilizowahi kutokea, kuna hii pia ambayo imesahaulika na utamu wake. Filamu ambayo sio tu inakuburudisha bali inakufundisha pia sehemu fulani ya historia ambayo inapuuzwa ama kusahaulika.

Ipo hivi … katika miaka hiyo ya 1960’s, kunatokea mauaji ya waziri mkuu wa Congo, bwana Patrice Lumumba. Kifo hicho kinapelekea mlipuko wa vita ya wenyewe kwa wenyewe kiasi cha kutishia amani ndani ya Congo haswa mashaka yakiwa katika jimbo tajiri wa madini, Katanga, ambapo huko kuna vikundi vya kijeshi vinayopigania makampuni ya uchimbaji wa madini wakishukiwa huenda wakatumia mwanya huo kama njia ya kuanzisha harakati za kuitwaa Congo.

Nyumba ya vikundi hivyo kuna mikono ya wafaransa na wabelgiji lakini pia wakiungwa mkono na baadhi ya waafrika wa Katanga. Waziri mtawala wa jimbo la Katanga, bwana Moise Tshombe anahaha. Kutokana na zogo hili, kiongozi wa Umoja wa mataifa (UN), anaona kuna uwezekano mgogoro huu ukapeleka kutokea kwa vita ya tatu ya dunia hivyo anaamua kuchukua hatua kukabili tatizo kama maji hayajafika shingoni.

Anatuma kikosi kidogo cha kutunza amani cha wanajeshi wa Ireland ambao wanaenda kuweka kambi katika kitongoji cha Jadotville (kwa sasa kinaitwa Likasi) ndani ya Katanga. Wakati huohuo, afisa wa UN, Dr. Conor, anaanzisha misheni ya kivita ‘Operation Morthor’ dhidi ya vikundi vya kifaransa na kibelgiji pasipo kushirikisha kikosi hichi cha wa Ireland.

Matokeo yake wanakufa wana-Katanga thelathini, na kupelekea kuzuka kwa vita baina ya vikosi vya wana-Katanga wakiwa wanaongozwa na wafaransa na wabelgiji ambao wanaanzia mashambulizi katika kitongoji cha Jadotville!

Kwa idadi wanakikundi hao walikuwa kama alfu tatu hivi, huku wanajeshi wa-Ireland wakiwa mia moja hamsini tu! Sasa je, wanajeshi hawa watatoboa dhidi ya wenyeji walioungana na mataifa yanayoinyemelea Congo na rasilimali zake? … kazi ilikuwa pevu.

Ni jasho na damu.

LOCKOUT ya 2012.

View attachment 1478806

Teknolojia hubadilika kila uchwao. Karibia kila sekta inaguswa na mabadiliko haya aidha kwa haraka ama taratibu. Lakini jambo moja la kujiuliza ni je kila kinacholetwa na teknolojia hiyo, kitakuwa na mema kwetu?
Filamu hii inajulikana pia kwa jina la MS One: Maximum Security, mahadhi yake ni miaka ya mbele huko ambako teknolojia inakuwa imepevuka kuliko sasa kiasi kwamba dunia imekuwa na namna ya kujiweka salama dhidi ya wahalifu hatari zaidi kwa kuwafungia jela iliyopo angani, ambapo huko wafungwa huwekwa katika hali fulani ya pumbazo wakitumikia miaka yao yote ya adhabu mpaka kikomo chake.

Basi bwana mmoja, kwa jina Snow, ambaye ni agent wa zamani wa CIA, anajikuta matatani na serikali yake akituhumiwa kumuua agent wa CIA anayeitwa Frank ndani ya chumba fulani katika moja ya hoteli ingali kiuhalisia hakufanya hivyo. Anahojiwa kwa nguvu akilazimishwa kukiri kosa ambalo hajalifanya na haijalishi namna gani anajitetea, haaminiki. Chief wa CIA anaamini bwana huyo ndo muhusika.

Ingali hayo yakiwa yanaendelea, binti wa Rais wa Marekani, Emilie, msichana mwenye kujawa na udadisi mkubwa, anatembelea gereza la MS One ambalo lipo angani akiwa amedhamiria kwenda kufanya tafiti yake huko kuwa mahadhi hayo ambayo wafungwa wanatunziwa huwasababishia kupata matatizo ya akili.

Huenda binti huyu alisahau kuwa hili eneo linahifadhi wahalifu hatari zaidi ama alikuwa anajiamini na ulinzi wake maana haya maamuzi kwa mtu mwingine sidhani kama angelifanya, wazungu husema curiosity killed the cat, na waswahili husema mwanakulitafuta …..

Basi binti huyu akiwa katika shughuli zake huko, akajikuta matatani baada ya silaha alokuwa nayo mlinzi wake kutua mikononi mwa mhalifu ambaye anatumia nafasi hiyo kuwaweka chini ya ulinzi na kuwafungulia wahalifu wenzake huru huku binti wa Rais akiwa mashakani.

Sasa kutokana na hili jambo, chief wa CIA anachekecha kichwa na kuona ni bwana Snow tu ndiye ana uwezo wa kumkomboa binti huyo. Anamshirikisha lakini Snow anakataa. Ili kumshawishi, anamuahidi bwana Snow kuwa endapo akifanya hivyo, basi atakuwa huru dhidi ya kesi nzito inayomkabili.

Kwasababu ya kutaka uhuru wake, Snow anaingia kazini.

Vipi, atatoboa dhidi ya kundi la wahalifu hao hatari? Je, ni nani alimuua Frank, agent wa CIA mpaka bwana Snow kuingizwa matatani? … na ni nini Emilia anatakitaka haswa kwenye gereza la MS One? Atafanikiwa?

BONUS MOVIE:

INFAMOUS ya 2020.

View attachment 1478809

Achilia mbali uraibu (addiction) wa vitu mbalimbali kama vile sigara, pombe na madawa, siku hizi kuna uraibu mpya na hatari – uraibu wa mitandao ya kijamii (social networks addiction). Kuna watu ni kheri walale njaa lakini sio wakose bundle wakashindwa kuperuzi instagram, whatsapp, Youtube ama Facebook!

Sasa ni kheri hao, kuna ambao wanaenda mbali zaidi ya hapo wakihakikisha wanakuwa maarufu kwenye mitandao hiyo kwa namna yoyote ile, hata kwa kukaa uchi na kujirekodi video za utupu cha umuhimu ‘followers’ na ‘comments’. Mengine baadae!

Basi ipo hivi, msichana anayeitwa Arielle, waitress wa mgahawa ndani ya mji mdogo wa Florida, ana ndoto ya kuwa maarufu haswa pasipo kujali hana ‘connection’ wala chochote kile. Akiwa katika hamu hiyo, bahati mbaya ama nzuri, anakutana na kijana aliyetoka jela si muda, kwa jina Dean, ambaye anaungana naye na kutengeneza team ya kusaka umaarufu kwa njia yoyote ile.

Walipochekecha mawazo wakaona njia nyepesi na ya haraka ya kufikia wanapopataka ni mitandao ya kijamii, huko wawe wanapost vitu vya hatari na vitata kwani ndivyo ambavyo hukamata ‘attention’ ya watu zaidi.

Sasa vitu hivyo ni ipi? Picha za uchi ama? Hapana, wao wakaona waende mbali zaidi kwa kufanya uhalifu wakiwa wanaurekodi kisha wanautuma mubashara kwenye mitandao. Kweli wazo likafanya kazi. Upesi Arielle akaanza kupata wafuasi kedekede mitandaoni, likes na comments! Roho yake ikasuuzika.

Lakini kama ilivyo kwa kula nyama za binadamu, Arielle akawa anataka zaidi na zaidi. Kila tone la umaarufu aliloupata halikukidhi kabisa kiu chake. Tamaa hiyo ikapelekea aanze kufanya matendo makubwa na hatari zaidi, kukimbizana na polisi, kufanya ujambazi na hata kuua kabisa! … kila alipokuwa anayafanya hayo akazidi kujizolea umaarufu na wafuasi, wengine wakija kustaajabu, wengine wakifurahia na wengine wakishangazwa na uchizi huu.

Njaa yake hii ya kutaka zaidi, inamtisha mpaka mpenzi wake, bwana Dean, ambaye anastaajabu ni nini mwisho wa yote haya.

Je, ni nini gharama ya umaarufu huu?

Kwa leo tuishie hapa... ukihitaji hizi movies zote na ziada nimekusogezea kwa urahisi kabisa, zama hapa kwa telegram:

Movies Na Stories

Na kule pande za youtube, nimewawekea kazi hii hapa... wewe tu ushindwe..

Naona Leo umekuja kitofauti kidogo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom