S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Wewe neno uchochezi mbona umekuwa maarufu sana siku hizi? Kwani zamani ulijificha wapi? Lakini nasikia zamani saaana ulikuwa Maarufu sana katika Mataifa mbalimbali, na kwa sasa upo Mataifa mengi hasa Afrika. Ivi huwa unasifa gani ili Mimi, Ndugu zangu na wengine TULIJUE kwa undani zaidi na zaidi. Nasikia watu wakikuhoji tu, unakuwa mkali sana , ebu niambie leo sifa zako ili nami nizifahamu nisije nikakuhoji ukanizuru.
Kuna wengine waliniambia kwamba wewe hupenda watu ambao hawahoji maswala yako bali wale wanaopenda kukusifia sifia. Wewe neno Mchochezi unapenda nini hasa?. Wengine wameniambia kuwa ni kukaa kimya tu kwani eti huwa unajisikia salama salmini kabisa.
Nasikia wewe neno Uchochezi ulishawahi kudhuru, kufunga na hata kuuwa Watu maarufu na wasio maarufu katika Mataifa mbalimbali; na uliuwa na kufunga Wanafalsafa, Wapigania Haki za Binadamu, Wana-Mapinduzi na Viongozi katika nchi mbalimbali.
Kwa mfano, eti wewe neno Uchochezi ulifanya yafuatayo????
1. Ulimuuwa Mwanafalsafa wa Kigiriki Socrates kwa sababu alikuhoji na kuanza kuwaelimisha watu bila ithini yako uchokozi.?
2. Ulimuuwa mpigania haki za binadamu na aliyekuwa anapinga ubaguzi wa rangi Marekani Martin Luther Jr.King.?
3. Ulimuuwa Che-Guavara Mwana-Mapinduzi wa kweli Duniani na ambaye amebaki kuwa alama ya ukombozi Duniani kote.?
4. Wakati wa Ukoloni, ulimtia hatiani Mwalimu Nyerere kwa sababu alikuwa anakupinga kwa hoja.?
5. Ulimuuwa Mwana na Mzalendo wa Afrika na Mzawa wa Congo Patrice Lumumba (aliyekuwa Waziri Mkuu wa Congo).?
6. Ulimfunga Nelson Mandela miaka 27 kwa sababu ya kupinga Ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini.?
7. Ulimuuwa Thomas Sankara, Che Guavara wa Afrika kwa sababu ya kupinga maovu ya Watawala si kwake tu, bali Duniani kote.?
8. Nasikia Wapigania Uhuru wengi wewe neno Uchochezi uliwafunga?. Na wale waliokusifia uliwakumbatia na kuwakarimu kabisa. Kuna wengine walikupinga sana kama wakina Mkwawa, Mirambo na wengine, lakini mwisho wa siku uliwashinda. Bila shaka wewe neno Uchochezi utakuwa na nguvu nyingi sana.
9. Nasikia wewe neno Uchochezi mara nyingi chochote atakachoongea yule ambaye anataka kuingia madarakani hata kwa njia halali za Kidemokrasia huwa humpendi kumsikia kabisa. Nasikia, Uganda kuna watu kila siku unawaweka ndani, nasiki hata nchini kwetu upo kila sehemu nasikia unataka watu wanyamaze na ikibidi wakusifie, ivi wewe neno Uchochezi unapenda nini hasa?.
10. Nasikia una mkono mrefu sana wewe neno mchochezi, na hakuna atakayeweza kukukimbia.?
11. Inasadikika kuwa wadadisi wa mambo husemi hata Yesu Kristu aliyokuwa anayahubiri neno la Mungu yale maneno yalikuchukiza mno mpaka ukachukua hatua hiyo uliyoichukua.?
12. Yule Prof.maarufu sana aliyewahi kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Walter Rodney miaka ya 1970s nasikia alikuja hapa kwa sababu hapa alikuwa anapendwa lakini alikotoka ulimchukia sana wewe neno Uchochezi. Mwisho wake kwa sababu una mkono mrefu kilichotokea Wana Historia wanajua.
13. Hata Marais Maarufu inasadikika hukupenda ukweli wao, kwa mfano Abrahamu Lincoln, Rais wa zamani wa Marekani mlitofautiana kidogo lakini sijui kilitokea nini.?
14. Nasikia unaogopeka sana wewe neno Uchochezi, lakini kuna watu baadhi wako tayari kufa kwa sababu ya kukupinga wewe na wanaacha kusema ukweli.?
15. Wengi inasadikika kuwa uliwachukia na kuwafunga pamoja na kuwazuru.?
Nasikia unaogopa sana UMOJA yaani watu wanaokupinga na wameungana.
1. Afrika ya Kusini waliungana kukukabiri wakakushinda.?
2. Mwalimu Nyerere naye alipata kukudhibiti sana kwa sababu ya Umoja wa Watanzania.?
Watu waliogawanyika, wanaopenda kukusifia nasikia unawapenda sana. Lakini mwisho wa siku, ukiwamaliza wale wanaokupinga, hata wanaokusifu leo hawako salama kabisa.
Kuna mtu mmoja alikusifu sana huko Ujerumani wakati wa Utawala wa Hitler, lakini mwisho wa siku alijikuta peke yake na ukokosa wa kumshughulikia mwisho wa siku ukamshughulikia yeye mwenyewe na alijuta kwelikweli.
Sasa wewe neno UCHOCHEZI jina lingine unaitwaje sasa?
1. Dikteta?
2. Mkoloni?
3. Mpenda Maendeleo?
4. Mpenda Sifa tu?
5. Mungu Mtu?
6. Mzalendo?
Ngoja Niishie hapa nisije nikakuuzi maana huna dogo wala kubwa.!!!
13/January/2017