Wewe Na Simu Yako

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
211
Inashangaza sana jinsi tekinologia za kisasa zinavyozidi kushika kasi na kuendelea kwa mwendo wa kasi sana ,inaonekana tu kama miaka michache iliyopita mtu alipotakiwa kuchangua Huduma za Simu za mkono basi alilazimika kwenda MOBITEL kilazima au TTCL kwa simu za mezani , kwa kupindi cha sasa hivi hakuna wasi wasi tena wa mambo hayo kuna kampuni nyingi za simu za mikono ambazo hutoa huduma nyingi , nafuu na kwa umakini zaidi ya enzi hizo .

Pia kuna simu za aina nyingi madukani kwa sasa zenye vitu kama kamera , muziki na kadhalika wenye simu hizo wanataka wawe na uwezo wa kutumia vitu hivyo ndani ya simu zao na watoa huduma hizi wanatakiwa kuhakikisha kampuni zao zinatoa huduma hizi kwa wateja wao .

Kutokana na hali ya uchumi ya watanzania wengi , mtu hapendi gharama kubwa sana katika kuendesha simu yake , kutokana na majukumu mengine ya kimaisha , wengine hawaajui jinsi ya kuchagua mitandao inayoendeana na mambo yao wanayotaka wao .

Hapa chini kuna mawazo mbadala jinsi unavyoweza kufanya ili uweze kutumia simu yako na mtoa huduma yako ya simu kwa umakini zaidi na iliyo na gharama nafuu .

- Mfano ungetaka kampuni inayotua huduma hiyo ya mawasiliano kwa gharama ndogo kutokana na uwezo wako si ndio ? unatakiwa ujiuliza maswali kadhaa kabda hujarukia , mfano wanatoa huduma yoyote maalumu kwa ajili ya familia mfano familia yenu ya watu 10 je kampuni husika inaweza kuwasaidia kupunguza gharama au wana parkage yoyote maalumu kwa ajili ya familia ?

- Tunaona watu wanavyokuwa na namba zaidi ya 2 za simu , wengine wanasimu mbili wengine huweka na kuchomoa katika simu hiyo , sio wote wanapenda hivi , ni kutokana na mitandao yenyewe haina uhakika sana , unatoka hapa kwenda kibaha hapo unakuta zantel haifanyi kazi unalazimika kubadili line , wengine ni kutokana na gharama za baadhi ya mitandao wengi sasa wanatumia Tigo kwa sababu ya longa longa 2 .


- Je wanatoa huduma za bure za mawasiliano kwa namba maalumu katika mtandao huo huo ? mfano mimi natumia tigo naweza kuchangua namba maalumu ambayo naweza kupiga bure baadhi ya simu au wakati wowote ?

- Kuna wakati wanatoa dakika bure za maongezi kila mwezi au kila unaponunua au kuongeza salio katika simu yako ? kama zantel wanatoa dakika za bure binafsi sijawahi kutumia ila huwa naona matangazo yao katika mitaa

- Wanatoa SMS za bure kila unapoongeza salio Fulani katika simu yako ? kwa hakika nimeona hii katika Vodacom na siku hizi wameanzisha kadi mpya maalumu kwa sms pekee au kama sio bure je wanatoa huduma ya sms ambayo wewe unauwezo wa kuitumia ?

- Pamoja na kuongea siku hizi katika simu nyingi unaweza kucheza games , kudownload miziki na milio au hata kutazama video je hapa kampuni husika inatoa bonus gani kwa wateja wao ambao wanataka kucheza games , kudownload miziki na milio ya simu je ni nafuu ?

- Angalia katika majukwaa ya mtandao usikie wenzako wanasema nini kuhusu mitandao ya simu na watoa huduma , ili nawe uweze kuchangua unataka nini kutokana na uwezo wako na huo ndio utakuwa mwanzo mzuri wa kuweza kupata huduma nzuri za simu kutokana na uwezo wako .
Ninavyosema uangalie katika majukwaa wenzako wanasema nini namaanisha katika hii mitandao kuna matatizo ambayo yapo na hawa hawahangaiki kuyashugulikia . mfano kutokana na Longa longa 2 ya tigo , kuna baadhi ya saa ukimpigia mtu wa tigo simu yake inakuwa busy kwa hata dakika 10 hata kama haongei.
-
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom