Wewe endelea kuwa na fikra hizi maana utaendelea kubaki nyuma kila siku

Lazaro Samwel

Member
Apr 27, 2019
33
26
Author- Coach Lazaro Samwel

Kuna watu mpaka sasahivi hawajui umuhimu wa facebook,instagram,whatsapp n.k kwasababu bado wanajua hii mitandao ya kijamii ni upotezaji wa muda.

Kuna mtu anajua mitandao ya kijamii ni kwaajili ya kuonesha maisha yake tuu na kufuatilia maisha ya watu wengine basi.

Nakumbuka kuna bwana mmoja nilipokuwa Live instagram nikifundisha mwanafunzi wangu namna ya kufanya matangazo ya kulipia fb akasema unapenda Facebook kweli.

Unajua sababu ya kuuliza ilikuwa ni nini? Alidhani facebook ni mtandao wa kurefresh tuu basi na hauna manufaa mengine.

Haya ndo makosa makubwa ambayo yanafanya wafanyabiashara wengi kuzidi kubaki nyuma katika biashara zao kwasababu bado wanatumia njia za kizamani kutafuta wateja au kufanya mauzo ambayo sio ya kuridhisha kabisa.

Wafanyabiashara wengi bado wanaona mitandao ya kijamii
kama sehemu ya kupoteza muda,makosa makubwa sana kama na wewe ni miongoni mwao.

Nikuulize tuu.

Kwani unakosa nini kama mfanyabiashara endapo hautatumia mitandao ya kijamii kama ofisi nyingine ya biashara yako?

Ngoja nikupe baadhi ya majibu ya swali hili na mengine utajiongeza mwenyewe.

1. Unajiweka katika nafasi ya kuzidi kumpa nguvu mshindani wako kukuondoa sokoni kwasababu kwa sasa asilimia kubwa ya watu kabla ya kununua bidhaa yoyote mara nyingi hutumia mitandao ya kijamii kama sehemu ya kufanya uchunguzi wa bei na sehemu ambayo wanaweza pata bidhaa nzuri.

Inamaana kama
haupo na mshindani wako akawepo kwenye mitandao ya kijamii kwa kifupi tayari umeshakosa mteja.

2. Kama hautumii mitandao ya kijamii na unakuta wateja wa biashara yako wanapatikana kwenye mitandao ina maana itakuwa ni ngumu sana kujenga brand yako katika soko ambalo upo.

Kwa sasa connection baina ya biashara na wateja unaweza kujengwa kwa content ambazo mtu unatengeneza kwenye mitandao yako ya kijamii kwaajili yako.

3.Itakuchukua muda sana kuwataarifu wateja wako juu ya bidhaa au huduma mpya ambayo inawezekana umeileta kwenye biashara yako.

Mitandao ya kijamii imekuwa ni sehemu muhimu sana katika karne hii kupasha habari watu haswa wateja kwa uharaka juu ya jambo lolote jipya katika biashara zetu hivyo kama hautumii mitandao ya kijamii ni lazima pia ukubali kupata changamoto ya watu kuwa na mwitikio wa haraka kwa huduma au bidhaa yako mpya au ofa ambayo unayo.

4. Lazima mauzo yako yatakuwa sio ya kuridhisha haswa kama upo kwenye B2C maana mbinu za kizamani nyingi katika biashara zimekuwa hazina nguvu kwa wakati huu wa kidigitali.

Watu wengi kwa sasa wana smartphone na wengi ni kama wamekuwa addicted na matumizi ya simu na hata ukiangalia wengi kwa sasa wanatumia mitandao ya kijamii kununua vitu ambavyo wanahitaji, sio nguo,simu,viatu wengi wanaplace order online na kutumiwa au wengine kwa kuona biashara ya mtu online anaweza kwenda ofisi na akanunua alichokiona kwenye mitandao.

Hapa pia lazima nikuongezee kitu ambacho ni muhimu sana katika kufanya mauzo.

Kwenye mitandao ya kijamii kama facebook,instagram n.k wana huduma ya kulipia matangazo yako kufikia watu wengi ambao wanahitaji huduma yako wengi tunapenda kuita Sponsoring Ads

Hauwezi kusema kwakupost tuu kwenye mitandao ya kijamii basi unaweza kupata wateja,kufanya matangazo ya kulipia kuna kupa nafasi kubwa sana ya kufikia watu wengi na kupata wateja wengi ambao watanunua bidhaa au huduma yako.

Kwanini sasa uache kutumia huduma hii?

Unafanya tangazo la $5 lakini unaweza ingiza hata 150,000/= kwenye tangazo lako, ni nani ambaye kwa kusubiri tuu anaweza fanya mauzo ya faida kubwa namna hii? Wapo wachache sana.

Tunapoelekea biashara nyingi ambazo bado wamiliki wameng’ang’ania mifumo ya zamani watapata tabu sana kwenye swala la kuuza kwasababu dunia inabadilika kwa kasi sana na mitandao ya kijamii inakuwa na nguvu kubwa sana.

Kuna mambo mengi sana ambayo mfanyabiashara anaweza nufaika na mitandao ya kijamii.

Lakini hivi ni vichache vya kujifunza kuweza kukushtua kidogo kuangalia umuhimu wa mitandao ya kijamii kwako wewe mfanyabiashara.

Lazaro Samwel
Author-10 Books | Sales And Marketing Expert | Professional Copywriter
#akiliyaushindi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom