Wew soma tu hii makala: Si lazima kuchangia hoja!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wew soma tu hii makala: Si lazima kuchangia hoja!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mizambwa, Feb 8, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Hata wagonjwa wakifa!  Mwandishi: Charles Misango
  NAANDIKA makala hii nikiwa sijali kwa lolote na chochote kitakachonipata kutoka kwa yeyote.

  Kama wao wasivyojali, nami sasa sijali tena kuwalea watu wasiojali wengine. Wasijali watu wanyonge, masikini na wasiokuwa na uwezo wa kunufaika na uchumi wa nchi.

  Sijali tena kuwaambia hata wakichukia na kunichukia! Siwezi kuwajali hata kama wangekuwa rafiki ama ndugu yangu. Undugu na urafiki unaoua watu nani anaujali? Na niujali kwa manufaa gani?

  Wiki jana saa tano na dakika arobaini, nilipita kando ya lango la Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure, nikielekea hoteli niliyofikia. Kando ya lango hilo nilikuta kundi la wananchi walioonekana kuwa katika mjadala mzito.

  Sikujali kusikiliza kinachoendelea, hasa baada ya kuona wawili kati ya walio katika kundi hilo ni kina mama waliovalia vilemba vya Chama Cha Mapinduzi.

  Hata hivyo, nililazimika kusimama baada ya kusikia sauti kali ya kilio, kilichoandamana na maneno ya; ‘wauaji wakubwa'! Nilijizuia kutojali kwa muda ili nijue kulikoni.

  Nilichokipata ni simulizi ya kusikitisha. Niliambiwa kuwa nusu saa iliyoppita alifikishwa mama mmoja mjamzito ambaye hali yake ilikuwa mbaya na alihitaji huduma ya haraka kunusuru maisha yake na ya kiumbe chake.

  Naambiwa kuwa kwa zaidi ya nusu saa hakupewa msaada wowote na wahudumu waliokuwapo, kila mmoja alikuwa akipita lwake bila kujali kilio cha kuomba msaada kilichotolewa na mama huyo. Hakuna aliyejali uhai wake na kilio hicho kilipokewa kama wimbo wa pambio kanisani.

  Watu hao wananiambia kuwa baada ya jitihada za kuwaomba madaktari waliokuwapo kushindikana, mume na ndugu wa mama huyo mjamzito wakaamua kumchukua na kumpeleka sehemu nyingine ambako waliamini wangepata msaada. Hawakufika hata hatua kumi, mama huyo akaaga dunia na kiumbe chake!

  Ni katika dakika hiyo ya kifo cha mama huyo na mtoto wake, kilometa chache tu kutoka ilipo hospitali hiyo, Rais Jakaya Kikwete, anasikika akitamba kuwa CCM ndicho chama pekee kinachopendwa na Watanzania na kwamba kimejipanga kushinda nafasi zote za uongozi zilizonyakuliwa na wapinzani (CHADEMA?) katika jiji hilo ili kuwaletea wananchi maisha bora!

  Anatamka kwa tabasamu pana kama ilivyo kawaida yake, maneno yanayopokewa kwa shangwe, vigeregere na nderemo kubwa toka kwa mamia ya wafuasi wa chama hicho waliosafirishwa bure kutoka kila kona ya mkoa kuja ‘kujaza' Uwanja wa CCM Kirumba zilikofanyika sherehe za miaka 35 ya chama hicho.

  Kundi hilo linaelekea Uwanja wa CCM Kirumba kwa nyimbo na shangwe, ambako huko Kikwete na chama chake wameandaa mlo mzito kwa watu wote.

  Wote hawa, hakuna anayejali wala kuguswa na vifo vya watu wasio na hatia kama kile cha mama mjamzito na mtoto wake kutokana na mgomo mzito na mkubwa wa wataalamu na wahudumu wetu wa afya.

  Wana CCM hawa hawajali kabisa na tukio la mgomo unaoendelea kutikisa nchi kiasi cha kusababisha vifo vya watu maskini na wanyonge kila siku. Wanajali ngoma, muziki wa TOT, huku viongozi wake katika namna ya kushangaza wakiwaza ushindi wa mwaka 2015.

  Wengine wamesambaa mikoani wakiongoza matembezi ya CCM na kutoa hotuba za majigambo na madaha ya kuwa serikali inawajali wanyonge. Wengine wanatumia magari ya serikali katika shughuli za chama bila aibu wala woga. Wote na magwanda yao ya kijani, wanahubiri propaganda na kuacha kuhangaika na maisha ya watu.

  Hakuna anayejali hata kidogo! Wanazungumza na kutamba kuwa CCM inapendwa na watu! Mtu gani akipende chama kisichojali wanyonge? Chama kisichoumia kwa kupoteza uhai wa watu kwa kuendekeza sherehe zinazotumia mamilioni ya fedha kwa kula na kunywa huku watu wanakufa!

  CCM wanataka nani awajali kama yenyewe haiwajali wengine? Mamilioni kiasi ya fedha yaliteketea nchi nzima kwa madai ya kusherehekea miaka 35 ya uhai wake.

  Kingekuwa chama cha watu makini wanaojali watu, kingechukua uamuzi mgumu wa kufuta sherehe hizo na kuelekeza fedha zilizotumika kutimiza matakwa ya madaktari hata kwa yale masharti machache kati ya mengi waliyotoa.

  Nakuapia, kama CCM wangefanya hivyo, wangeonekana kuwa chama makini, kinachojali na kupigania haki za watu. Kingefuta sherehe hizi, kingekuwa kimefanya kampeni kubwa ambayo haijapata kuwapo.

  Lakini wapi! Waahirishe sherehe kisa kuna mgonjwa hana huduma? Aliyekwambia wanajali hayo mambo ni nani?

  Kiburi cha hawa hakiji hivi hivi tu. Kina msingi wake na wanauamini sana. Wanapewa jeuri na sisi Watanzania wenyewe ambao hatujali kabisa mambo ya msingi.

  Waliowapa kichwa serikali ya CCM ni sisi Watanzania wenyewe kwa tabia yetu ya kutojali mambo ya msingi. Hakuna anayesumbuka kujua hadi leo mgomo wa madaktari umesababisha vifo vya watu wangapi! Tunaishia kulalamika na kulaani tu. Hatujali; kila mtu na lwake.

  Ingekuwa nchi ya watu wanaojali, leo hii CCM isingekenua meno na kutamba kwa hotuba zisizo na mashiko mbele ya watu wanaokufa bila msaada.

  CCM kwa kujua kuwa Watanzania wengi hawajali, inafanya lolote na chochote na kusema kila aina ya neno bila woga! Chama hicho kinajua kuwa hata akitokea mtu anayetaka kuonesha dalili za kujali kama wengine sisi, atashukiwa kwa kasi kama kifaranga cha kuku kwa kila aina ya vitisho.

  Kibaya sana, hata sisi ambao tunaumizwa na watu hawa wasiojali, tunarukiana kwa mbwembwe, kebehi na jeuri ya maneno, kwa kuitwa kila aina ya majina machafu, na wengine kufunguliwa mashitaka eti ya kuhatarisha amani ya nchi.

  Ngoja niulize, kuna amani katika nchi hii? Amani gani ya watu wanaokufa kwa sababu mwenye madaraka na uwezo hajali? Kuna amani gani kwa watu waliokata tamaa ya maisha na wanaishi bila matumaini? Kuna amani gani kwa watu wanaoongozwa na viongozi wanaoendesha nchi kama wanafanya mchezo wa komedi? Sijali zaidi sasa, nawaomba Watanzania tukatae kuwajali watu wasiotujali!

  NI MAKALA KATIKA GAZETI LA TANZANIA DAIMA:
   
 2. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  na sichangiiiiii ka mleta mada ulivotusihi,

  nimeshaisoma.
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  mizambwa

  inaumia sana
   
 4. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Hii ndio serikali legelege isiyowajali wananchi wake, bali inawatoa kafara ili ishinde chaguzi.


  Mizambwa
  inaniuma sana!!!
   
 5. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Well constructed, well written and well presented.
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Dah huo ndio ukweli na ukweli ambao viongozi hawataki kuusikia wala kuusoma
  Wao wako kwenye kilele cha furaha ila walio wengi wako kwenye shida na vilio
   
 7. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Ukitaka unaweza kusema ''serikali nzuri ni namna ya viongozi bora (waliopewa madaraka na mamlaka) wanavyoihudumia jamii yao ili mambo yasogezwe mbele kimaendeleo''. Serikali ikiwa na aidha viongozi wabovu au legevu jamii haiwezi kuhudumiwa inavyopaswa.
   
 8. double R

  double R JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 1,356
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Hizi roho za watu zilizopotea ni laana kwao, zitawalilia. Inawezekan isiwe leo, ila ipo siku (iliyo karibu) watepokea stahili yao. Naomba macho yangu yashuhudie hilo.
   
 9. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  tuna bora viongozi na siyo viongozi bora
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Ukishakuwa na kiongozi ambaye uwezo wake unafanana na hawa jamaa hapa, ujue tumeliwa............anaweza akafanya makeke washkaji zake wakatuletea jeans na tshirts.....

  [​IMG]
   
 11. MANI

  MANI Platinum Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Mkuu upo sahihi kabisa ni matumaini yangu 2015 tutachagua viongozi bora na sio bora viongozi !
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Sasa kwanini walikuwa wanaimba mapambio ya kanisani badala ya kutoa huduma? aise hii nchi nafikri wakrito wamefikia pabaya kwenye ubaguzi; juzi mwalimu mkuu anawafukuza wanafunzi huku akisema yesu ameshinda; kitu gani kinaendelea kwenye mioyo ya wakristo??

   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  科羅拉多大峡谷·懸空玻璃橋--可承受72架波音飛機的重量,可抵御80公里外發生的8级地震,站在1200米高的懸空玻璃上俯瞰大峽谷和科羅拉多河,你的心臟能否被hold住?
  科羅拉多大峡谷·懸空玻璃橋--可承受72架波音飛機的重量,可抵御80公里外發生的8级地震,站在1200米高的懸空玻璃上俯瞰大峽谷和科羅拉多河,你的心臟能否被hold住?
   
 14. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu kwani Sekou Toure ni hospitali ya kanisa gani hadi wawe wanaimba mapambio?
  Hapakuwa na gloves wala catheter, wala delivery pack hapo unasemaji? Ambulance haikuwa na mafuta ya kuweza kumleleka Bugando.

   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwandishi wa Makala hii nampa pole sana kwa sababu moja.

  Kwanza kabla hujasoma hiyo sababu, hebu soma sahihi yangu hapa chini na ndiyo urudi kusoma sababu.

  Sababu yenyewe ni kuwa "CCM ndiyo kwanza wanakusanya hela kwa ajili ya sherehe za MUUNGANO."

  Hahahahaaa, I love this Party. I love this Country.
   
 16. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mwandishi wa makala alinyimwa lile pilau nini.....lol
   
 17. k

  katesh Senior Member

  #17
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwandishi ni wale wale tu!
   
Loading...