Werena na kombani wanasubiri nini kujihudhuru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Werena na kombani wanasubiri nini kujihudhuru?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mallaba, Jan 3, 2011.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  CHAMA Cha Wananchi (CUF), kimemshauri Rais Jakaya Kikwete, kuwafukuza Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema kutokana na kuwachanganya Watanzania kuhusu suala la Katiba.
  Mbali na ushauri huo chama hicho pia kimeeleza kuwa kauli za watendaji hao wa serikali zimesababisha hata kauli ya Rais aliyoitoa Desemba 31 mwaka huu, kuhusu suala hilo ionekane ina utata na hivyo kuitaka Ikulu kuondoa utata huo kwa kuifafanua zaidi.

  Hayo yalielezwa jana na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
  Mapema mwezi ulipo, wakati mjadala wa Katiba ukiwa umepamba moto, Kombani ambaye ndiye waziri mwenye dhamana akitoa maoni yake juu ya suala la katiba mpya alisema haoni umuhimu wa suala hilo sasa na kufafanua kwamba serikali haina bajeti yake.

  "Katiba mpya kwa sasa haiwezekani kabisa kwani sio muhimu na kuwa serikali haina bajeti ya kushughulikia katiba mpya," alisema Kombani. Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema, alisema "Kuandika Katiba mpya hapana, lakini kufanya marekebisho kwa kuondoa au kuongeza mambo fulani kwenye katiba, ruksa.”

  Jaji Werema alisema hayo Desemba 27 mwaka jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa hafla ya kumwapisha Jaji Mkuu Mpya, Jaji Mohamed Othman Chande.

  "Suala la kubadilisha ibara zinazoonekana kutokidhi haja na kuingiza mambo mapya kwenye katiba, linakubalika na kwamba hayo yamekuwa yakifanyika," alisisitiza Jaji Werema na kutolea mfano mabadiliko ya katiba yaliyoruhusu kuingizwa kwa haki za binadamu.

  Werema alisema “Lakini si kila mtu analolisema lifuatwe. Tukisema kila mtu anachokisema tukifuate haitakuwa sawa. Kwa mfano mimi kule kwetu wafugaji nao watataka mambo ya ng’ombe wao yaingizwe kwenye katiba, na Wahaya pia wanaweza kusema tuingize kwenye katiba ndizi zao, hii si sawa;” alisisitiza Jaji Werema.
  Jana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mtatiro kutokana na watendaji hao kupingana kwa kauli, CUF inamtaka Rais Kikwete kuwapumzisha Kombani na Werema walioonekana kuropoka mambo ya kuwakatisha tamaa Watanzania kuhusu suala hilo.

  "Kama Rais Kikwete atakuwa makini, anapaswa sasa kuwapumzisha Kombani na Werema ili wasiendelee kutia doa jeusi serikali yake ambayo tayari imejaa kila aina ya matatizo," alisema Mtatiro.


  [​IMG]
  "Kombani alisema katiba mpya kwa sasa haiwezekani na siyo muhimu, lakini pia serikali haina bajeti ya kushughulikia suala hilo, Jaji Werema alisisitiza kwa nguvu zote kwamba katiba mpya haiwezekani na akasema kitakachofanyika ni kuiwekea viraka katiba hii, iliyotoboka na Rais sasa anasema ataanzisha mchakato wa kuitazama upya katiba ya nchi kwa lengo la kuihuisha. Huku ni kutuchanganya," alisema Mtatiro.

  Aliendelea "CUF tunasema wanatuchanganya kwa kuwa kwa kauli hizo za Kombani na Werema, kauli ya Rais pia sasa ina utata kwani naye hakutaka kueleza anasimamia lipi kati ya kuiwekea viraka katiba iliyopo au kuandika katiba mpya." Aliendelea "Katika mambo hayo ya katiba, watu wake wakubwa na wataalamu ni hao, sasa inapotokea wanatofautiana kimsimamo hadharani halafu rais naye anakuja na msimamo wake, ni tatizo kubwa linalohitaji ufumbuzi wa kina," alisema Mtatiro.

  Mtatiro alibainisha kuwa CUF itapingana na juhudi zozote za serikali kuunda Kamati ya Marekebisho ya Katiba itakayoenda kufanya kazi ya kutia viraka katika katiba iliyopo, kwani lengo la Watanzania si marekebisho ya katiba bali kuandikwa katiba mpya.

  "Kama kauli ya rais Kikwete inaamanisha kutaka iundwe katiba mpya, CUF inamuunga mkono, lakini kama anataka kuifanyie marekebisho katiba iliyopo, hatutashirikiana naye," alisema.


  [​IMG] Julius Mtatiro, Kama Rais Kikwete atakuwa makini, anapaswa sasa kuwapumzisha Kombani na Werema ili wasiendelee kutia doa jeusi Seriakli yake

  Akinukuu hotuba ya Rais Kikwete, inayosema “jambo la nne ambalo tulilo kubaliana kufanya ni kuanzisha machakato wa kuitazama upya katiba ya nchi yetu kwani lengo la kuihuisha ili hatimaye tuwe na katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne,” Mtatiro alisema, rais hakueleza bayana nini anachotaka kifanyike.
  Wakati Jitihada za kumpata waziri Kombani kuzungumzia msimamo huo wa CUF zikigonga mwamba jana, Jaji Werema aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa "Sijiuzulu ng'o." kwa kauli hizo.

  Alisema ''Wanaotaka nijiuzulu ni wale wasiofikiria, kwani kila mtu ana nafasi yake ya kuongea kuhusu katiba. Mimi nimetoa mawazo yangu na wengine wakitaka watoe ya kwao," alisema Werema. Aliendelea, ''Kunitaka nijiuzulu ni fikra za kichanga sana na potofu. Mtu mwenye upeo mpana hawezi kusema Mwanasheria Mkuu ajiuzulu kwa hili,"alisema.
   
 2. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Watu hawa wawili; celina komabani Na fredrick Werema wamelita doa jeusi baraza jipya la mwaziri maana hadi sasa ndio mawaziri pekee walioonyesha kupotoka na kukurupuka kutoa matamshi yanayowachefua wananchi. Mwaziri wengi wengineo nawapa a big up so far so good. ni kufutwa kazi au la ni jukumu la JK kumua. BUT it is a blemish. kwa Werema namwambia kazi za umma sio zizi la ngombe kule ukuryani, heshimu watu utaheshimika, tumeshaona wanasheria wakuu wengi nchi hii, please put your mind into gear before you utter anything, watanzania walimchagua JK na sio Werema
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  nico mgaya 2011-01-03 11:22
  werema na kombani ni aina ya wale watu wanaodhani wanauwezo wa kujua fikra za wakubwa wao na kuziongea ili kuwaridhisha na matokeo yake ni kwamba watu wa aina hii huwa hawafikirii kabisa ni watumwa wa mawazo. be yourself please! kuna kila sababu ya kutowashirikish a kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya.
   
 4. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu JK ni msanii na Ikulu TUKUFU amegeuza jumba la sanaa.
  Alicho kisema Kombani na Werema ndicho kilichokuwa/kilichoko akilini mwa JK.
  Kumbuka ilani ya uchaguzi ya CCM haijaongelea katiba mpya hata kidogo na kwenye kampeni hawakuweza kusema hata kwa kukosea.
  Kumbuka Mwanasheria mkuu anateuliwa na rais na Kombani pia
  Kumbuka Rais kaunga mkono ongezeko la bei ya umeme na kusema hana maelezo mazuri zaidi ya yale yaliyotolewa na EWURA, na hii ni ishara kwamba kila kinachofanyika na idara za serikali JK anakifahamu.
  Ni dhahiri alichosema Kombani na Werema JK alivifahamu kabla ya wahusika hawajasema hadharani.
  JK kafanya USANII kuwakana watu wake hawa wawili (Werema na Kombani ) kuwa anaanzisha mchakato wa KATIBA mpya, hili ni changa la macho

  Serikali ya JK imejaa Mafisadi, wasanii na washikaji wake na ni ya kishkaji hivyo hakuna jipya.
  JK, Kombani na Werema wote ni wamoja.
   
 5. d

  dotto JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Werema na Combania wamesema kile ambacho Kikwete analenga kufanya. Kwani Kikwete yeye amesema au katoa vision yoyote juu ya katiba. Ila kitendo chake cha kuleta tume yaonyesha kuwa katika viatu vya werema na combania.
   
 6. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Mabele nimekukubali, Huyu JK alijua kila kitu na hilo silikatai. Lakini ingawa hawakuwa nalo hili kwenye Ilani yao ya CCM jamaa amebidi asome nyakati na kuona kuwa hapa piga ua lazima KATIBA iwepo, basi akaona bora awakane jamaa zake.
   
 7. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kwa hiyo una maanisha kuwa JK ataweka Viraka kama Werena alivyosema?
   
 8. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Haina haja ya kuwashupalia hawa viumbe wajiuzuru wakati bado hatujajua kama kweli tutapata katiba mpya.
  Tukumbuke mwaka 2005 tuliambiwa kutakuwa na maisha bora kwa kila mtanzania na mpaka sasa maisha ndio yanazidi kuw magumu huku watu wakiwa wamekwishasahau ahadi wlizopewakabla,inawezekana kabisa Kombani na mwenzake wanasema kweli,tatizo lililopo sasa ni kuwa hatuna uhakika wa nani mkweli kati yao na rais.
  Je mnakumbuka ahadi za JK 2005?
  Alitimiza ngapi na ngapi hakutimiza?Ahadi ya Kadhi ilitimia?
  Mwaka 2010 katoa ahadi ngapi?
  Kama aliwahi kusema serikali haina pesa za kuwalipa walimu mishahara kama walivyoomba,hizo za kuandaa maoni na katiba yenyewe zitatoka wapi?
  Mimi bado naamini kabisa kuwa inawezekana watendaji wa rais wanajua kinachoendelea na ndio maana wakatoka na kauli kama zile,tusubiri tuone nani ni mkweli katika hili.
   
 9. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  ahadi za bajaji kwa wazaai wote, Viwanja vya ndege kila mji, kuifanya kigoma kuwa DUBAI, na mengine mengi zaidi
   
 10. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  hakuna mawaziri wa kuwapa big up pale...wote ni hovyo. hebu onajinsi ngeleja anavyoropoka halaf we unasema eti unawapa heko. wizara nzima labda ukimmtoa magufuli na mwakyembe is a crap...
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  MTEGO WA NOTI, Sikukatalii kuwa wizara zote ni usanii mtupu, lakini pia lazima tukumbuke kuwa ingawa ni usanii tupu basi kuana walau uhafadhali wa wengine, kuliko hawa wanajitoa mbele ya jamii na kupinga kitu wasichokuwa nacho hata uhakika, je huwa wanatoa hizo mamalaka toka wapi? Hawa si ndio wanaomwakilisha RAISI JK? Iwezje wajiongelee yao wenyewe? Na shawishika kusema kuwa hata lazima kuwa na mchezo mchafu unaofanyika.. subiri tuone
   
 12. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  JK ni msanii na ataendelea kuwa msanii, anajua sana anachokifanya na alichokisema. Selina na Werema pia wanajua kinachoendelea. Ni dhahiri usanii ndio utakaofuata hapa, kama kuna juhudi zozote zilizoanzishwa kudai katiba mpya zisirudishwe nyuma sababu eti JK kasema anaunda tume, kwanza hata hakusema tume ni ya muda gani na itaongozwa na nani, atatuzuga hadi miaka yake minne ipite kisha anaamka mwaka wa 5 kiusanii na kujifanya kuiweka rasmi kwenye ilani ya CCM anamuachia anaefuata jumba bovu limuangukie.
   
 13. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hili swala hawezi kulikwepa hata siku moja, ama zake ama zetu
   
Loading...