Werema, Muhongo: Tunasubiri neno la Rais tuachie ngazi

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,366
2,000

Frederick Werema

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, wamesema baada ya hukumu ya Bunge sasa wanasubiri neno la Rais.

Viongozi hao waliyasema hayo jana, ikiwa ni siku chache tangu Bunge kupendekeza mamlaka za uteuzi ziwavue madaraka.

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyowasilishwa bungeni na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilionyesha viongozi hao walifanya makosa kadhaa na kusababisha uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Viongozi wengine ambao mamlaka zao za uteuzi zilitakiwa kuwavua nyadhifa zao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye aliingiziwa Sh bilioni 1.6, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, Sh bilioni 1.6 na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja Sh milioni 40.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Profesa Muhongo alisema: "Sina maoni, sasa wewe unataka kujua nini… kwani wewe umeonaje na ni lazima nikujibu au unataka nikujibu porojo… sasa nakujibu kwamba kaulize Bunge kuhusu hilo suala la Escrow na kama una maswali kuhusu mambo ya umeme nenda Tanesco watakujibu."

Jaji Werema: Siwezi kubishana na Bunge

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, alisema hana kauli wala maoni yoyote na hawezi kubishana na Bunge.

"Siwezi kubishana na Bunge kwa sababu wenye mamlaka wamepewa kazi kuchukua hatua, acha wafanye kazi, au unataka nisemeje tena?" alihoji Jaji Werema.

Hatima ya Askofu Kilaini, Nzigilwa

Kanisa Katoliki nchini limesema haliwezi kuwaadhibu maaskofu wake waliotajwa kuingiziwa fedha zilizotokana na kashfa hiyo kwa sababu wanawajibika kwa kiongozi wa kanisa hilo duniani, Papa Francis.

Maaskofu wa kanisa hilo waliotajwa kwenye kashfa hiyo ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini aliyedaiwa kupewa Sh milioni 80.5 na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa, Sh milioni 40.4.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, alisema hadi sasa hawajataarifiwa kama kuna kosa limefanyika, hivyo hawawezi kukutana.

"Kama kungekuwa na kosa angetaarifiwa rais wa baraza… kwakuwa hakuna kosa hakuna dharura yoyote ya kusema tukutane.

"Kama kanisa hatuna sababu ya kusema tuhamaki tuwaadhibu kwa sababu askofu yuko chini ya baba mtakatifu," alisema Askofu Niwemugizi.

Hata hivyo, alisema kama vyombo vya dola vikifanya uchunguzi na kubaini kuna makosa ya kinidhamu au kijinai, hapo ndipo wanaweza kuchukua hatua.

"'Unless' uchunguzi ukifanywa wakasema kuna makosa ya kijinai na kinidhamu taratibu nyingine zinaweza zikachukuliwa.

"Jambo hili linazungumzwa kisiasa zaidi na ukweli haukusemwa bungeni… hizi ni mbio za urais, sasa wanataka kuwaingiza na wengine ambao hawahusiki," alisema.

Kuhusu Benki ya Biashara ya Mkombozi ambayo ilihusika kupitisha fedha hizo, Askofu Niwemugizi alisema ilifuata taratibu zinazotakiwa ndiyo maana walienda Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kujiridhisha.

"Benki inafanya biashara, na mteja anapoleta fedha wanafuata taratibu zinazotakiwa, benki nyingine ziliona wivu kwa kukosa hizo fedha na ndio wanaochochea," alisema.

CAG mpya kuipitia Ripoti ya IPTL

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Juma Asaad, amesema kazi yake ya kwanza ni kuipitia tena ripoti ya ofisi yake juu ya Akaunti ya Tegeta Escrow iliyojadiliwa bungeni hivi karibuni.

Profesa Asaad aliyasema hayo baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

"Nikianza kazi nitaipitia ripoti ya IPTL ambayo ilizua mjadala mkubwa katika Bunge hivi karibuni kwa sababu sijui kilichoandikwa, lakini nikiisoma na kutumia uzoefu wangu nitaweza kujua kinachoendelea," alisema Asaad.

Alisema pia atafanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuhakikisha anatenda haki kwa kila atakayehusishwa na ripoti ili Serikali iweze kuchukua uamuzi.

"Siwezi kumuonea mtu, bali nitafanya kazi kwa uadilifu ili kuhakikisha kuwa natenda haki kwa kila mmoja, kwa sababu nina uzoefu wa mambo hayo, hivyo basi nitahakikisha haki inatendeka.

"Hii ni dhamana kubwa kwangu niliyopewa na rais, siwezi kumwangusha, hivyo basi nitahakikisha natimiza majukumu yangu kwa mujibu wa sheria ili ripoti zote ziwe na kiwango," alisema.

Christopher Ole Sendeka

Siku chache baada ya Bunge kupitisha maazimio nane kuhusu kashfa ya Escrow, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM), ameibuka na kusema baadhi ya wabunge walipokea rushwa ili kupoza mjadala bungeni.

Alisema rushwa ilivyokuwa inagawiwa kama njugu mjini Dodoma ilisababisha baadhi ya wabunge kutetea hoja za kuwalinda watuhumiwa jambo ambalo halikuwa sawa.

Akizungumza na MTANZANIA jana kwa njia ya simu, Sendeka ambaye anafahamika kwa misimamo yake, alisema baadhi ya wabunge ambao waliipinga ripoti ya CAG na ile ya PAC hawakuwa na nia njema.

Baadhi ya wabunge waliokuwa vinara wa kutetea watuhumiwa na kupinga ripoti hiyo ni pamoja na Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi, Asumpta Mshama (Nkenge), Livingstone Lusinde (Mtera) na Richard Ndassa (Sumve) wote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia.

Ole Sendeka alisema pamoja na kwamba hana ushahidi wa kimahakama, lakini kulikuwa na dalili za wazi za kuwapo vitendo vya rushwa kutolewa kwa baadhi ya wabunge.

"Siwezi kuwa na ushahidi wa kimahakama, lakini kulikuwa na dalili za wazi za rushwa kutolewa nje nje bila aibu na ndiyo maana ulishuhudia namna wengi walivyokuwa hawataki kuona ukweli ukisemwa na wakati mwingine kuwatetea mafisadi huku wakiwatupia kashfa wengine," alisema Sendeka.

Alisema ni jambo lililo dhahiri kwamba kulikuwa na rushwa kutokana na baadhi ya wabunge kubadili misimamo yao ya awali.

"Hata wale ambao kawaida yao walikuwa na misimamo katika mambo ya msingi na taifa kwa ujumla, walibadilika ghafla jambo lililotushangaza na hilo lilituaminisha kwamba kulikuwa na rushwa ilitolewa kwa sababu haiwezekani mtu kutetea vitu ambavyo viko wazi," alisema.

Chanzo: Mtanzania
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Tunamshauri Rais asisikilize majungu. Hawa wachapa kazi hawafai kuachishwa kazi hata chembe.

Rais baki nao hawa umalize nao awamu yako, hayo majungu ya akina Mkono na Mengi yasikuyumbishe.
 
omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,154
2,000
Wakati Mh. Mbowe anasoma barua ya ofisi ya mwanasheria mkuu kumtaka mwanasheria wa TANESCO akafanye 'due diligence' mara waziri/naibu akasema yeye haijui na ndipo Mbowe akaseme "hii ndio sign nyingine ya a failed state".
Hapa nadhani alikuwa akikazia maneno ya Zitto kuwa wizi kama huu hauwezi kutokea katika nchi iliyo na utawala. Lakini ndio umeshatokea TZ 'yenye utawala'.

Kitendo cha kuamua 'kumsikilizia' mkuu wao ni wazi wanajua kitu, labda nao walikuwa mamesenja na wanataka kujua kama kufikicha ujumbe wa kukwapua pesa lilikuwa kosa lao au kosa la aliyewatuma!
 
gsu

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
3,463
1,225
Tanzania mbowe gazeti la udaku eti nao kwa akili yao wanachochea mgogoro jk siku zote huchanganya na zake siyo za kuambiwa mtasota sana majungu kwa jk mwiko.
 
gsu

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
3,463
1,225
Wakati Mh. Mbowe anasoma barua ya ofisi ya mwanasheria mkuu kumtaka mwanasheria wa TANESCO akafanye 'due diligence' mara waziri/naibu akasema yeye haijui na ndipo Mbowe akaseme "hii ndio sign nyingine ya a failed state".
Hapa nadhani alikuwa akikazia maneno ya Zitto kuwa wizi kama huu hauwezi kutokea katika nchi iliyo na utawala. Lakini ndio umeshatokea TZ 'yenye utawala'.

Kitendo cha kuamua 'kumsikilizia' mkuu wao ni wazi wanajua kitu, labda nao walikuwa mamesenja na wanataka kujua kama kufikicha ujumbe wa kukwapua pesa lilikuwa kosa lao au kosa la aliyewatuma!
mbowe mwenyewe zero anakipi cha kuzungumza mbele ya washika dau wenye akili zao,ila jk hatasikiliza majungu kamwe simama kidete rais wetu.
 
gsu

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
3,463
1,225
Unaonaje ukimchukua akawa houseboy wako kumaliza majungu ya watu.
majungu ya mengi hayana nafasi tena kwenye serikali yetu sikivu jk kathubutu kaweza na sasa anasonga mbele.
 
majoto

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
2,087
2,000
Tunamshauri Rais asisikilize majungu. Hawa wachapa kazi hawafai kuachishwa kazi hata chembe.

Rais baki nao hawa umalize nao awamu yako, hayo majungu ya akina Mkono na Mengi yasikuyumbishe.
Kweli kabisa... tumeiona kazi yao ya wizi uliobobea mchana kweupe tena macho makavu yasiyo na haya wakiwaacha wagawa kura wao wakifa kwa kukosa dawa na watoto wao wakijiuza kwa kukosa kazi.

Tunamngoja huyo prof aliyewaajiri kwa kazi hiyo....
 
Cybercrime

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
3,248
2,000
Wakati Mh. Mbowe anasoma barua ya ofisi ya mwanasheria mkuu kumtaka mwanasheria wa TANESCO akafanye 'due diligence' mara waziri/naibu akasema yeye haijui na ndipo Mbowe akaseme "hii ndio sign nyingine ya a failed state".
Hapa nadhani alikuwa akikazia maneno ya Zitto kuwa wizi kama huu hauwezi kutokea katika nchi iliyo na utawala. Lakini ndio umeshatokea TZ 'yenye utawala'.

Kitendo cha kuamua 'kumsikilizia' mkuu wao ni wazi wanajua kitu, labda nao walikuwa mamesenja na wanataka kujua kama kufikicha ujumbe wa kukwapua pesa lilikuwa kosa lao au kosa la aliyewatuma!
MBOWE na ZITTO wote wezi tu waae, halafu wanaogopana kwa hiyo walitumka ESCROW kuwakutanisha
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Kweli kabisa... tumeiona kazi yao ya wizi uliobobea mchana kweupe tena macho makavu yasiyo na haya wakiwaacha wagawa kura wao wakifa kwa kukosa dawa na watoto wao wakijiuza kwa kukosa kazi.

Tunamngoja huyo prof aliyewaajiri kwa kazi hiyo....
Huo wizi uko wapi? tuoneshe kwenye ripoti ya CAG.

Unaandikia mate na wino upo?
 
joharry

Member
Nov 22, 2014
54
0
Kikwete usikubali kusikiliza upuuzi,hawajibiki mtu hapa safi sana wanaume wa shoka hamyumbishwi kijinga jinga,izo zilikua kelele za siasa ukweli utabaki pale bale,fitina za wasira,lukuvi na wengineo watakufa nazo

kikwete usiwapoteze watu hawa plzzzz
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,847
2,000
Kumbe hata kanisa katoliki wameishitukia repoti ya PAC?.au nao ni mafisadi.
 
Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,019
2,000
Tunamshauri Rais asisikilize majungu. Hawa wachapa kazi hawafai kuachishwa kazi hata chembe.

Rais baki nao hawa umalize nao awamu yako, hayo majungu ya akina Mkono na Mengi yasikuyumbishe.
Wewe huna hadhi hata ya kumshauri mwenyekiti wa Kijiji sembuse rais. Unaota wewe
 
Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,995
1,500
Huo wizi uko wapi? tuoneshe kwenye ripoti ya CAG.

Unaandikia mate na wino upo?
Biashara ya escrow account ilikwisha last week,

wajinga mnafikiri bado kuna majadiliano mengine mtasubiri sana ila wenye akili tunasubiri marejesho.
 
Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,019
2,000
Kikwete usikubali kusikiliza upuuzi,hawajibiki mtu hapa safi sana wanaume wa shoka hamyumbishwi kijinga jinga,izo zilikua kelele za siasa ukweli utabaki pale bale,fitina za wasira,lukuvi na wengineo watakufa nazo

kikwete usiwapoteze watu hawa plzzzz
Nyie magamba naona Kama mnavuana nguo hadharani. Ifikie hatua muheshimiane kwa maneno unayosema Ni wazi kuwa ccm imepasuka vipande vipande Kuna ccm imani Na ccm maslahi.
 
dabluz

JF-Expert Member
Feb 28, 2013
2,406
2,000
Kuna Dada mmoja humu huwa simuelewi elewi sijui ni jambaz sugu!!
Anaroho ngumu huyu mtu sijawahi ona.. fox
 
Last edited by a moderator:

kiwososa

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,125
1,500
Tunamshauri Rais asisikilize majungu. Hawa wachapa kazi hawafai kuachishwa kazi hata chembe.

Rais baki nao hawa umalize nao awamu yako, hayo majungu ya akina Mkono na Mengi yasikuyumbishe.
Umekuwa lini mshauri wa rais???!! au unajustify pesa ulizopewa kwamba ulizifanyiya kazi???!!!! Ila una roho ngumu??!!!!kweli njaa mbaya.na kejeli zote toka kwa watanzania bado tu unaendelea kutetea wezi. Fungu lilikuwa kubwa sana nini???
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom