Werema jibu hoja hizi kwa watanzania sio kung'ang'ania Zitto...

jobe ayoub

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
203
195
(Hayo ndio maazimio ya Bunge ambayo Werema anakwepa kueleza utekelezaji wake. Hii ni vita ya Watanzania, Waafrika na wanyonge wote. Sio vita ya mtu mmoja. Wanaharakati wabebe kazi hii takatifu ya kutokomeza ufisadi)
Hayo ndio maazimio ya Bunge ambayo Werema anakwepa kueleza utekelezaji wake. Hii ni vita ya Watanzania, Waafrika na wanyonge wote. Sio vita ya mtu mmoja. Wanaharakati wabebe kazi hii takatifu ya kutokomeza ufisadi( By zitto)...

KWA HIYO BASI naliomba Bunge lako Tukufu liazimie:-
(i) Kwamba Bunge lako Tukufu liunde Kamati Teule kuchunguza raia wa Tanzania wenye kumiliki fedha za kigeni na mali nje ya Tanzania. Kamati Teule hiyo ifanye kazi zifuatazo:-
(a)Kuchunguza mfumo mzima wa utoroshaji wa fedha na kufichwa nje ya nchi;
(b)Kuchunguza na kupambanua mali na fedha haramu dhidi ya halali zinazomilikiwa na raia wa Tanzania katika taasisi za fedha nje Tanzania;
(c)Kuchunguza utaratibu mzima wa kugawa vitalu vya utafutaji mafuta na gesi kati ya mwaka 2003 – 2008;
(d)Kuchunguza mtiririko mzima wa utoroshaji wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania kupitia kampuni ya Meremeta na pia kampuni tanzu ya Triannex pty ya Afrika Kusini naDeep Green Finance Limited na kupendekeza hatua za kuchukua dhidi ya wahusika wote wautoroshaji wa fedha kwenda nje;
(e)Kuchunguza umiliki wa Watanzania kwenye kampuni zote zenye mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi hapa nchini na namna umiliki huo umekuwa ukibadilika yaani proceedszilizotokana na mabadiliko hayo ya umiliki na kama kodi stahili zimekuwa zikilipwakutokana na mabadiliko ya umiliki huo; na
(f)Kuchunguza kwa kina mali za Watanzania wote waliowahi kushika nafasi za UwaziriMkuu kati ya mwaka 2003 mpaka 2010, waliowahi kushika nafasi za Uwaziri wa Nishati na Madini, Uwaziri wa Ulinzi, Ukuu wa Majeshi, Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi, Uanesheria Mkuu wa Serikali, Ukamishna wa Nishati, Ukurugenzi Mkuu waTPDC, Uenyekiti na Ujumbe wa Bodi waTPDC katika ya mwaka 2003 mpaka 2010.
(ii)Kwamba, Serikali ilete Muswada wa Sheria Bungeni ifikapo Mkutano wa 11 wa Bunge kwamba itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi yeyote wa Umma au mume au mke wake au watoto wake kuwa na akaunti katika mabenki nje ya nchi isipokuwa kwa sababu maalumu na kwa kibali rasmi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(iii)Kwamba, Serikali iwasiliane na Benki ya Dunia ili kupitia Kitengo cha Assets Recovery Unit ili mabilioni ya Fedha na mali zisizoondosheka zinazomilikiwa na Watanzania katika mabenki ya nchini Switzerland, Dubai, Mauritius na visiwa na maeneo mengine yote ambapo hufichwa fedha na mali ili kukwepa kodi na kwamba mali hizo na mabilioni hayo yaliyopatikana kiharamu yarudishwe nchini mara moja.
(iv)Kwamba, katika Muswada tajwa hapo juu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aimarishiwe mamlaka ya kutoa kibali kwa Mtanzania yeyote anayetaka kufungua akaunti ya Benki nje ya nchi na kwamba kila mwaka Gavana atatangaza kwenye Gazeti la Serikali na magazeti yanayosomwa na wananchi wengi orodha ya Watanzania walioomba na walioruhusiwa kuwa na akaunti ya benki nje ya Tanzania;
(v)Kwamba, Watanzania wote wenye akaunti za fedha nje waeleze wamezipataje na TAKUKURU wachukue hatua za kisheria dhidi ya watu wote wenye kumiliki fedha na mali kinyume na mapato yao halali;
(vi)Kwamba, Serikali, katika Mkutano wa Bunge wa Kumi na Moja (11) na baada ya Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu raia wa Tanzania wenye kumiliki fedha za kigenikwenye mabenki na mali nje ya Tanzania ilete taarifa ya hatua ilizochukua ili kuziba mianya ya utoroshaji wa fedha nje ya Tanzania.
(vii)Kwamba, Serikali katika Bajeti ya mwaka 2013/2014 itaanzisha kodi maalum ‘financial transaction tax’ ya angalau asilimia 0.5 ya thamani ya ‘transaction’ ili kuweza kuwa narekodi zauhakika za fedha ndani na zinazotoka nje ya nchi.

Swali, ni kipi kimefanyika hadi sasa zaidi ya jitihada za kuligeuza suala hili kuwa naming and shaming politics?

AU kujua majina tu kutoka kwa zitto ndio maazimio yatakua yamepata majibu..
RETHINK...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom