werema afukuzwe kazi au ajiuzulu: hajui wajibu wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

werema afukuzwe kazi au ajiuzulu: hajui wajibu wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Dec 29, 2010.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nimefuatilia matamko mbalimbali yanayotolewa na jaji Werema ambaye ni mwanasheria mkuu wa serikali na kugundua kuwa hajui wajibu wake.

  (1) Amekuwa ni mtoa matamko ya serikali badala ya kuwa mshauri wa serikali. Kwanza alitoa tamko la serikali kuwa katiba haitabadilishwa, ila itafanyiwa marekebisho tu. Halafu akatoa tamko jingine kuwa serikali itailipa Dowans pesa zote zile na wala hakuna mjadala tena kuhusus hukumu hiyo ya Dowans vs TANESCO.

  (2) Amekuwa haheshimu wakubwa zake wa kazi kwa kutupitilia mbali tamko la waziri mkuu, ambaye ni mkuu wake wa kazi, kuhusu mchakato wa kuandika katiba upya.

  (3) Ameshindwa kuishauri serikali kuwa ICC court of arbitration inatoa usuluhishi katika mambo ya kibiashara ya kimataifa, haitoi hukumu. Kama pande zote husika zikikubalina na usuluhishi huo basi zinaridhia na iwapo upande mmoja usipokubaliana na usuluhishi huo basi pande hizo zifikishane mahakamani katika mamlaka husika. Kwenye kesi ya Dowans vs TANESCO, mamlaka husika na mahakama za Tanzania.

  Bado kuna utata kuwa TANSECO haijakubaliana na hukumu hiyo kwa hiyo jukumu hilo linatakiwa liachiwe mahakama zetu, siyo mwanasheria mkuu.


  Nina wasiwasi sana na interest binafsi za Jaji Werema katika kesi hii na hivyo ninadhani kuwa hafai kabisa kuwapo kwenye nafasi kile; hivyo nio ama afukuzwe kazi au ajiuzulu mwenyewe
   
 2. T

  Tanganyika Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaji werema asifikiri hii Tanzania ya leo ni kama Tanzania ile ya wakati anaingia chuo kikuu (kama alienda). Katiba mpya ni ya watanzania na si yake wala serikali, asifikiri yeye kuwa JM ndo katiba mpya haitapatikana. Katiba isipokuja kwa amani basi itakuja kwa kinyume chake na machafuko yatakayotokea yeye na wahusika wenzeka watawajibika...........angalia Ruto na Uhuru wanavyo hahaa!! Hakuna kisicho na mwisho.........angalia na wewe isije baadaye ukaenda the hague!! Angalia Ouko wa kenya aliwawa miaka 20 iliyopita lakini hivi majuzi kamati ya bunge imetoa taarifa kamili na waliyohusika kumkua..ikiwa ni serikali ambao ni Saitoti na Nicolas biwot na wengine!!! Sasa hawo mwisho wao ukoje? Werema nafikiri hicho kiti ulichokalia Kimeanza kukulewesha.........kama vile Kiti alichokaliaga Basil Mramba kilivyomlewesha na kusema wananchi wale nyasi ili ndege ya rais inunuliwe! kumbuka mwajiri wako ni wananchi na wakuhukumu ni hawo hawo wananchi!!!!! muombe Mungu akusamehe na utubu hiyo dhambi haraka! Hata kwa gharama yeyote KATIBA MPYA HAIKWEPEKI !


   
 3. k

  kayumba JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu ukipitia maneno ya huyu AG kuhusu suala la DOWANS inatia mashaka juu ya nani anataka aibuke na ushindi. Jiulize, kama Tanesco ilikuwa na mawakili wake kule mahakamani wao na hiyo Tanesco si ndio yenye kusema inakata Rufaa ama la?

  Kama AG hakupeleka wataalam kwenye kesi nadhani alikuwa hana wajuzi wa hayo mashauri. Je sasa inakuwaje awe na wajuvi wa kupinga kukatwa Rufaa. Au Kuna hujuma kama ilivyotabiliwa awali?

  Kwa matamshi yake juu ya Katiba mpya na hili la Dowans nafikiri hivi viatu vya u-AG vinaweza kuwa si saizi yake!

  Au katumwa aje kutuandaa watanzania kupokea hayo huko mbeleni?   
 4. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kichuguu,
  Kama kazi ya hiyo court ni usuluhishi tu? kwa nini serikali inakubali haraka haraka ushauri wa hii court?
  Werema ana ajenda gani ya siri kuhusu hizi pesa za walipa kodi?
  Wananchi tuna nafasi gani kupinga pesa yetu isilipwe?
   
 5. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kalambishwa pesa na mafisadi bogus huyu bora afukuzwe kama hataki kujiuzulu
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  kati ya watu wapuuzi na wajing huyu niwa pili........wa kwanza ni jk
   
Loading...