Wepesi wa serikali kusamehe mapato yake na ugumu wake kugharimia mambo muimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wepesi wa serikali kusamehe mapato yake na ugumu wake kugharimia mambo muimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Dec 17, 2010.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa miaka nenda miaka rudi, serikali imekuwa inapuuzia kukusanya kwa ukamilifu mapato yake, ikiwa ni pamoja na kutotilia maanani ufuatiliaji wa marejesho ya madeni yake. Kwa mfano, wadadisi wa mambo, wamebaini kwamba kila mwaka serikali inapoteza wastani wa thelusi moja ya mapato yake, kwa misamaha holela ya kodi. Kama hiyo haitoshi, thelusi moja nyingine inapotea kwa kutoza ada na mrahaba katika maeneo fulani fulani, mathlani madini, vitaru vya uwindaji na magogo, chini ya viwango vya kimataifa. Aidha, serikali kwa makusudi kabisa imekuwa ikipiga dana dana linapokuja suala la ufuatiliaji la madeni yake sugu. Kwa mfano inasemekana serikali inadai zaidi ya bilioni 900 za import support, na vile vile zaidi ya bilioni 300 ya mikopo ya pembejeo, inapobanwa na wafadhili ndipo inapocheza usanii ili kuwalaghai wafadhili hao kuwa wanafuatilia irejeshwaji wake. mbali na hayo kuna pia bilioni 150 walizokopeshwa kampuni ya mwananchi na BOT. Vile vile kuna zaidi ya bilioni 10 iliyolipwa na BOT kwa niaba ya kampuni ya Mzindakaya, mbunge wa zamani wa Sumbawanga, aidha kuna zaidi ya bilioni 100 zilizolipwa na serikali kwaajili ya Kagera Sugar n,k Wakati serikali inazembea ukusanyaji mapato hayo, huku inashindwa kukidhi matumizi muimu kama kutoa mikopo inayokidhi haja kwa watoto wetu walioko vyuoni, kwa kisingizio cha uhaba uhaba wa fedha.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wewe vipi, This is Africa where human sweat is cheaper than petrol!
   
Loading...