Wenzio hao wahuni!

Choveki

JF-Expert Member
Apr 16, 2006
458
170
Bwana Muro kaa sawa, wenzio hao wahuni
Ndugu Jerry ota mbwawa, wajuwe uwa mjini!
Dogo Muro watauwa, ingia zako mitini!
Wenzio hao wahuni, tulia au ishia!


Tena punguza jazba, tumia mbongo kichwani
Utabebeshwa viroba, vya ushahidi makini
Halafu ije dhoruba, uje ishia jelani
Wenzio hao wahuni, nahisi bora ishia!


Kwa mwoga hwenda kicheko, shujaa ni kilioni
Jilinde nawe kivyako, hata ikiwa mitini
Nasema tena wanoko, wenzio hao wahuni!
Wenzio hao wahuni, sikia kaka sikia


Tena hesabu bahati, ungali bado mjini
Wataka kukuthibiti, uyatoayo kinywani
wangekutwanga baruti, wakakukata maini
Wenzio hao wahuni, sikia Jerry sikia!


Tamati ninaishia, sikia yangu maoni
Ishia au tulia, papara si ushindani
Usije kuja jutia, kutoingia mitini!
Jamaa zako wahuni, tahadhari ewe Muro!


Wakatabahu,



choveki.
 
Back
Top Bottom