Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,219
- 40,451
Mtu mnafiki, mwongo, na ambaye hana uhuru wa mawazo huwa hagundui kitu chochote, akijitahidi ataishia kuiga na kukariri.
Moja ya sababu, wanasaikolojia wanasema kwa nchi ya China kutokufanya ugunduzi, na kuwa nchi ya copy and paste, ni wananchi wake kuelelewa katika mazingira yasiyoheshimu uhuru wa mtu.
Tanzania kuna wakati ilikuwa inaunganisha malori aina ya Scania, sasa hivi tumeishia kuunganisha pikipiki za China.
Kuna wakati tulikuwa tunaunganisha matrekta bora kabisa ya valmet, sahizi hatuunganishi hata power tiller.
Tulikuwa tunatengeneza baiskeli aina ya swala, baiskeli nzuri kabisa,sahizi hatutengenezi hata sindano ya cherehani.
Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza matairi bora kabisa yakijulikana General Tyre, sahizi tumebakia kuwa watumiaji wa matairi ya hovyo kabisa kwa ubora kutoka China.
Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza mashuka bora kabisa toka kiwanda cha Mutex, siku hizi tumebakia kuwa watumiaji wa mashuka ya hovyo kabisa, yapo kama vikaratasi, kutoka China.
Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza viatu bora vya ngozi toka kiwanda cha Moro Shoes, siku hizi tumebakia kuwa wanunuzi wa viatu duni kabisa toka China, ukijikwaa tu kimechanika au kuraruka.
Tulikuwa tunatengeneza ndoo za ubora wa hali ya juu, Amboni Plastics, siku hizi tumebakia na ndoo takataka ukibebea tu maji, mshikio unachomoka au ndoo yenyewe kupasuka.
Wakati ule ilikuwa kipimo cha umaskini kwa mama ni kuvaa kanga iliyotengenezwa China au India, huku mwenye uwezo akivaa kanga ya Urafiki, leo hata ukiwa na hela, kanga nzuri huipati popote, kila mahali ni takataka za kutoka China.
Zamani, katika Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo nchi angalao ilikuwa inaonekana kuwa na demokrasia, leo ndiyo nchi ya mfano kwa utawala usiozingatia sheria, usioheshimu mgawanyo wa mihimili. Tena imekuwa ni nchi ya kidikteta ambayo hata kura ya mwananchi haina maana yoyote katika kuwapata viongozi.
Kenya tuliokuwa tunawaona hawajastaarabika kwa kuendekeza siasa za ukabila, sasa ni nchi ya mfano Afrika Mashariki kwa kuheshimu utawala wa sheria, demokrasia, haki za watu, uhuru wa maoni, na katika kuheshimu mfumo wa siasa za vyama vingi.
Wakati wenzetu, kuendelea inamaanisha kuboresha, sisi kuendelea inamaanisha kuendeleza uharibifu. Tumekuwa Taifa bandia, taifa linaloongozwa kwa hadaa na ulaghai. Majukwaani wanatamka vingine, matendo yanakuwa kinyume. Wateule wamebakia kuumsifia anayewateua kwa unafiki. Kila mahali watasimama na kumsifia aliyewateua ili awaone na kuwasikia, wakiachia mic, wanamsema vibaya. Unafiki mtupu.
Watawala, hata pale ambapo mambo yanaenda vibaya, watakuambia kuwa sasa ndiyo tunapaa, wakati hata vyandarua vya mbu tunapewa msaada. Zamani, Serikali ilikuwa na watu wanapita mitaani kufanya fumigation kuua mbu na mende, leo tunashindwa hata kununua chanjo kwaajili ya watoto wetu wanaozaliwa.
Ni nani atalirudisha Taifa kutoka kwenye unafiki kulipeleka katika uhalisia? Nani ataweza kusimama na kusema kuwa Taifa letu ni duni katika nyanja nyingi, tusimame, turudi na kuanza upya?
Siku zote hatua ya kwanza kuleta mabadiliko chanya ni kuutambua na kuukubali udhaifu wako.