Wenzetu Kibakwe mmemwelewa George!!?

Ngonepi

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
1,872
1,200
Imekuwa ni kawaida sasa viongozi kutoa kauli za kejeli kwa wananchi wanapohoji mambo muhimu yawahusuyo,
Walianza viongozi wengi hapa Tanzania hapo kabla kutoa kauli za kashfa na kejeli kwa wananchi wao wanapoona hawawaungi mkono katika baadhi ya maamuzi yao, lakini wa vile Tanzania haijawahi kupata KIRANJA mwenye kumudu kumwajibisha kiongozi wake anapokosea limekuwa ni tatizo la kudumu sasa sisi wananchi maskini kukashifiwa na kukejeliwa.

Juzi hapa waziri wetu anayehusika na mambo ya UMEME ametuambia kama hatuwezi kununua umeme kwa bei wanayozidisha basi tukae GIZA au tutumie KOROBOI,

Hizi ni kashfa kwetu, ukweli watanzani walio wengi zaidi hatumudu kulipia umeme hata kwa bei iliyopo sasa! Na viongozi si kwamba hawajui!

Wastani wa kima cha mshahara kwa Mtanzania ni ngumu sana kutumia umeme kihalali kama inavyotakiwa. Mara nyingi tumeona operesheni kata umeme mitaani, lakini si kuwa watu tumapenda kudaiwa au tunapenda bure, ukweli ni kuwa umeme ni bei juu mno kwa mwananchi wa kawaida!

Nina ushahidi wa matajiri weengi wanaoiba umeme, na ukiwauliza mbona wanaiba na wanapesa madai ni hayohayo ya bei kubwa ya nishati hii.

Sasa bora viongozi wangekuwa wanakuja na kauli za kistaarabu wanapotaka kutuumiza na si maumivu na kashfa juu yake!!

Nimetaka kuwauliza wenzetu huko KIBAKWE na ninyi mtauziwa bei sawa na sisi jamani!! Taratibu na hizi kauli zenu hata kama mna uhakika hatuna cha kuwafanya wazee!!
 
Huko kibakwe wamemwelewa vizuri tu kwani wao hawaujui umeme ni kitu gani! Na wnaamini umeme ni aina ya kinywaji ambacho kwao hakina maana kwani wamezoea kunywa msabe na komoni au dadii. Ni utani tu.
Binafsi namshangaa sana huyu mwalimu asiyewajali waliomfikisha hapo. Watu wa kibakwe mngemwacha tu aendelee kula chaki kule Arusha Technical hadi akome.
Naomba kujuzwa juu ya hii taasisi ya uteuzi wa viongozi hasa mawaziri, hivi hawana chombo cha kudeal na nidhamu za mawaziri wa aina ya huyu na mulugo, muhongo na magufuli? Kama chombo hicho kipo kifanye kazi yake na kitangaze adhabu hizo hadharani. Otherwise wao wanachangia kuiua ccm.
 
Nchi haina kiranja hii, kila mtu mbabe, kila mtu ndio mwenye kauli ya mwisho, yaani vurugu tu!
 
Kwa hali hii, wanaoiba umeme hawata acha kabisa na wasiojua kuiba wengine watajifunza. Kwa ujumla wamewatengenezea ulaji vishoka wa Tanesco. Huenda pato wanalotegemea kupata hata nusu wanaweza wasipate.
 
Kwa hali hii, wanaoiba umeme hawata acha kabisa na wasiojua kuiba wengine watajifunza. Kwa ujumla wamewatengenezea ulaji vishoka wa Tanesco. Huenda pato wanalotegemea kupata hata nusu wanaweza wasipate.
Kibaya zaidi waheshimiwa wanafahamu kabisa kuwa hata ukiongeza bei ya umeme matatizo ya Tanesco hayawezi kwisha.

Shirika lina mikataba mibovu saana iliyoingia na wawekezaji wanaoliuzia umeme, kiasi mapato asilimia zaidi ya sitini inayokusanya inalipa kwa hawa wawekezaji.

Ni mikataba mibovu kweli, haiwezekani mtu azalishe umeme kwa jenereta ili akuuzie lakini kwa sharti la mafuta yatumikayo ujaze wewe mteja!! Haya ni maajabu kabisa!!

Juzi tumesikia mwanasheria Mtanzania mwenzetu anaidai Tanesco zaidi ya tsh 18bilion kwa ushauri wa kisheria alioutoa Tanesco na ambao uliishia kulitumbukiza shirika kwenye matatizo zaidi,

Sasa kwa mambo kama haya hata umeme uuzwe tsh 500 kwa unit bado shirika haliwezi kutosheka au kujiendesha kwa faida kwa kuwa pesa zote zinaenda kwa wawekezaji matapeli waliotusainisha mikataba kwa kutumia udhaifu na tamaa za viongozi wetu,
Leo waziri anatutukana!!
 
Back
Top Bottom