Wenzetu baada ya kuunga juhudi vipi akili waliacha huku upinzani?

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,346
1,303
Naomba tu niwataje wachache walioamua kuunga juhudi toka upinzani na kurejea CCM . Watu Kama ; Waitara, Gekul, Mkumbo, Mashinji, Kafulila, Silinde, Lijuakali na wengine wengi, hawa kwa Sasa hawaongei masuala ya wananchi.

Hawawatetei Tena bali wanaisaidia Serikali kuwawekea mazingira magumu kiuchumi na hata kuwatishia juu ya masuala ya demokrasia. Hivi siasa Ni kuanzisha pointi ya mafanikio na baada ya kupata unapoteza legacy yako.

Nawakumbuka hawa kipindi wako upinzani walikuwa wakiwatetea Sana wananchi. Kuna baadhi walikuwa hata tayari kufa, kufungwa, kufilisiwa ilimradi awasemee wananchi wa Hali ya chini.

Kwa Sasa hawasikiki au hiyo juhudi Ni sawa na imani ya walioko Freemason. Ukishaingia hakuna kutoa Siri na unaishi kwa masharti ya kikundi.

Kwa Sasa hivi katiba walioipigania na kutambulika ndani ya jamii hawana muda nayo wala hawataki kuisikia inajadiliwa maeneo Yao. Tozo zilizokuwa kero kwao na kwa wananchi wao Ni Kama kelele masikioni mwao.

Hawahitaji kugusiwa neno lolote baya linalotekelezwa na Serikali dhidi ya raia waliowaamini Hadi kuwabrand wakaonekana. Swali langu kubwa Ni kweli ndio wenyewe au washajivua akili wameanza upya kukua Tena kifikra na kimsimamo.

Tanzania kamwe haiwezi kujengwa na watu wa namna hii. Tulidhani wale maadui wa Nyerere washatoweka kumbe tumeweka adui mwingine uwoga. Uwoga huondoa kuniamini na badala yake hujenga taifa legelege. Taifa legelege litaridhia kila aina ya mkataba mbovu.

Mtanzania mwenzangu tumche Mungu , binadamu Ni mpangaji tu hapa duniani. Tusibadilike badilike Kama kinyonga sababu kila kiongozi ana mtizamo wake na hulka aliyozaliwa nayo.

Katiba Ni suluhu kwa kila hatua ya maendeleo tutakayopiga iwe kiuchumi au kidemokrasia. Usalama na amani Ni muhimu zaidi ya kuunga juhudi Kisha unakuwa bubu. Katiba nzuri itawaondolea watu hofu nao wataihoji serikali na kuisimamia.
 
Sifa kubwa na ya kwanza kuwa mwanaccm ni kujitoa ufahamu
JamiiForums313878302.jpg
 
Kosa walilofanya wachaga kushangilia kifo cha Magufuli litawagharimu hadi kizazi cha tatu.
#Gaidi
#corona imekita mizizi Moshi
 
Back
Top Bottom