Uchaguzi 2020 Wenzangu na mimi tulioaminishwa na kutabiri kifo cha CHADEMA na kuinuliwa kwa NCCR na ACT, mpo?

Fya-fyafya

Member
May 2, 2019
43
125
Sio siri tulio wengi tumejawa mate mdomoni na hatuamini hiki kinachoendelea kwenye mikutano ya chama cha CHADEMA.

Kutokana na Sekeseke kilichopata, Kazi kubwa ya kimaendeleo iliyofanya na CCM ndani ya muda mfupi, hama hama ya madiwani na wabunge, kukosa wawakilishi wenyeviti wa vijiji na mitaa, mlengo wao juu ya Janga la Corona, basi wengi tulidhani kwenye mikutano yake ya kampeni watu wangekuwa wa kuokoteza (wachache mno) ila cha ajabu sivyo ilivyo. Hapa nakumbuka kuwa usilolijua sawa na usiku wa giza na Usione na ukadhani.

CHADEMA kwenye kampeni hizi ndio chama ambacho kinachuana na CCM kwenye mahudhurio ya watu mkutanoni.

Yaani hii ndoa derby kisiasa kwenye kampeni hizi. Bado tunaona Lisu akiendelea kuwa na mvuto wa aina yake. Yaani jamaa anakismart awapo jukwaani. Sera yao ya Uhuru, Haki na Maendeleo imeonekana kukonga moyo za watu wengi.

Kama tumjuavyo Lisu, ni mtaalamu wa kujenga na kutetea hoja. Sasa kwake si shida kuwaelewesha maelfu ya wanaokula kumsikiliza sera ya Utani yao.

Ukiacha na nafasi ya Uraisi, wabunge na madiwani wanapeperusha chadema nao wana morali na wafuatao wengi sana kiasi kwamba unashindwa kupredict matokeo haraka haraka. Hii haikufahamika hivo kabla ya kampeni.

Vyama ambavyo vilitabiliwa kuwa vyama vikuu vya upinzani (NCCR na ACT) mambo si mazuri kwao. Kama wasipoingia mitini na kukacha kampeni A urais basi wanajitafutia magonjwa ya Presha na Sukari kwa kuumia mioyo juu ya mahudhurio hafifu sana.

Leo hii CHADEMA, chama ambacho wabunge na madiwani wengi walikuja na na kujiunga na vyama vya CCM, NCCR na ACT, kwenye kampeni hizi kinaonekana bado ni imara na pendwa kwa watu.

Kuna wengine wanasikiliza wakisema kuwa mvuto wa CHADEMA kwa sasa ni zaidi ya ule wa uchaguzi wa 201 enzi za Mzee Lowasa. Je, ni kweli?

Wao wanasema kuwa chadema ile ilikuwa imejaa mamruki wengi na kuwafanya hii ya sasa ni ya wnachadema halisi. Je ni kweli?

My take: Kuanzia uchaguzi huu, nimeamini kuwa siasa ni imani na imani haitoki moyoni. Kwani mazishi kuona jinsi gani watu wanavyozidi kujitokeza kwenye kampeni za chama hicho huku wakiwa wamevalia sare za chama kifua mbele. Hii ndoa demokrasia sasa.

Viva Tanzania.
 
Jamaa aliaminishwa ujinga eti ukinunua mchezaji uwa mchezaji anaama na mashabiki wa timu hivi ronaldo kuama man u kwenda madrid aliama na mashabiki ile biashara yao ya kununua wabunge na madiwani imebuma imewaumbua kuwa kununua viongozi sio ndio njia ya kuvunja upinzani, njia bora ya kuvunja upinzani ni maendeleo ya vitu yaendesambamba na maendeleo ya watu
 
Sio siri tulio wengi tumejawa mate mdomoni na hatuamini hiki kinachoendelea kwenye mikutano ya chama cha CHADEMA....
Kwa nzia uchaguzi huu, nimeamini kuwa siasa ni Imani na Imani haitoki moyoni. Kwani mazishi kuona jinsi gani watu wanavyozidi kujitokeza kwenye kampeni za chama hicho huku wakiwa wamevalia sare za chama kifua mbele. Hii ndoa demokrasia sasa.
 
ACT Walijiloga baada ya kukaribisha mzee wa "HELA ZA GHADAF"
Ni kosa lile lile la upinzani ambalo wamekuwa wakilifany mara kwa mara
 
Back
Top Bottom