Wenyeviti wawili CCM Tarime watuhumiwa kwa uhalifu:AMA KWELI MWIZI NI MWIZI

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Wenyeviti wawili CCM Tarime watuhumiwa kwa uhalifu

Na Samson Chacha, Tarime

POLISI katika Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya, wamewamtia mbaroni Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM wa Wilaya ya Tarime Samweli Magabe na Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Sirari, Sagara Mokome , wakihusishwa na mtandao wa uhalifu.

Watuhumiwa hao na wengine 30, walikamatwa Agosti 25 mwaka huu na hadi sasa bado wanahojiwa na polisi, kuhusu tuhuma hizo.

Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika Kanda ya Polisi ya Tarime na Rorya, David Hiza, alisema viongozi hao wa CCM na watuhumiwa wengine, walikamatwa katika operesheni maalum dhidi ya wezi wa mifugo.

Kwa mujibu wa Hiza, operesheni hiyo inafanywa kwa shirikiano na polisi wa kanda hiyo na makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

Alisema operesheni hiyo inalenga katika kuwabaini watu wanaojihusisha na mtandao wa wizi wa mifugo, ujambazi wa kutumia silaha za moto na watu wanaofadhili mtandano wa uhalifu.

"Lakini pia operesheni yetu inalenga katika kuwakamata na kawafikisha mahakamani, wachochezi wa vita vya koo, wanaojihusisha na madawa ya kulevya na uharifu mwingine," alisema Hiza.

Operesheni hiyo, imesababisha baadhi ya wafanyabiashara katika miji ya Sirari, Tarime mjini, Nyamwaga na Nyamongo, kukimbia makazi yao kwa hofu ya kukamatwi.

Back
Top Bottom