Wenyeviti wa vitongoji Bunda kuiburuza Halmashauri yao Mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenyeviti wa vitongoji Bunda kuiburuza Halmashauri yao Mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 12, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Kuandamana kupinga kuondolewa uenyeviti wa vitongoji


  na Ahmed Makongo, Bunda


  [​IMG] JUMLA ya wenyeviti 14 wa mamlaka ya mji mdogo wa Bunda, mkoani Mara, wamesema kuwa wataingia mahakamani kupinga hatua ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bunda, Cyprian Oyier, kuwaandikia barua kwamba kuanzia sasa sio wenyeviti wa vitongoji.
  Wenyeviti hao wakiwemo waanzilishi wa mji mdogo wa Bunda, wakati huo ukiwa na vitongoji 14 tu, hivi karibuni wameandikiwa barua na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Bunda, Oyier, kwamba kuanzia sasa sio wenyeviti wa vitongoji hivyo.
  Wenyeviti hao ambao 12 ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mmoja Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), wamedhamiria kwenda mahakamani kupinga uamuzi huo, kutokana na kuchaguliwa kwa mujibu wa sheria hivyo ni viongozi halali.
  Akizungumza na Tanzania Daima Erenest Nkonoki mwenyekiti wa kitongoji cha Mbumatare, ambacho awali kilikuwa Nyamakokoto, alisema hakuna kikao chochote kilichopitisha maazimio ya kuwaondoa madarakani hali ambayo imewafanya waamue kufanya maandamano ya amani ya kupinga maamuzi hayo.
  ‘Sisi lazima twende mahakamani kupinga uamuzi huu maana sisi tumechaguliwa kihalali kabisa na wananchi wanatuamini sasa leo hii tuchakachuliwe kiasi hiki….. hatukubali, wananchi wameamua kufanya maandamano ya amani katika kupingana na hilo,” alisema.
  Kwa upande wake Oyier amekiri kuwaandikia barua ya kutowatambua wenyeviti hao 14 na kwamba amefanya hivyo kwa mujibu wa sheria na kuongeza kuwa ufafanuzi kamili juu ya suala hilo atatoa kesho Desemba 13.
  Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kupata nakala ya barua iliyoandikwa na mkurugenzi huyo ambayo ina kichwa cha habari kisemacho ‘Marekebisho ya vitongoji katika kata, mamlaka ya mji mdogo wa Bunda’ iliyoandikwa Desemba 3, mwaka huu.
  Barua hiyo inasema: “Mnafahamishwa kuwa kutokana na marekebisho yaliyofanywa katika sheria ya serikali za mitaa (mamlaka ya wilaya) sura ya 287, tangazo la serikali Na. 173/2010, (Amri ya kugawa maeneo mapya katika kata) ya mwaka 2010, tangazo hilo limefanyiwa marekebisho tangazo la serikali namba 205/2009.”
  Aidha, barua hiyo inawataka wenyeviti wa vitongoji hivyo kukabidhi vifaa vyote vya ofisi zao, zikiwemo mihuri kwa watendaji wa kata zao husika ambapo taarifa ya makabidhiano hayo inatakiwa ifanyikie ofisini kwa mkurugenzi huyo, siku 7 kuanzia tangu kutoka kwa taarifa hiyo
   
Loading...