Wenyeviti wa Vijiji wadai posho,Wachoka kuitwa Waheshimiwa wakiwa mkono mtupu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Wenyeviti wa serikali za vijiji vya tarafa ya Makambako jimbo la Lupembe mkoani Njombe wamesema wamechoka kuitwa waheshimiwa bila kulipwa hata posho wakati wamekuwa na majukumu makubwa ya kuwatumikia wananchi.

Mbele ya mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swalle alipozulu katika tarafa hiyo kwa lengo la kukutana na wenyeviti wote wa vijiji na kusikiliza changamoto za maeneo yao ya kiutawala baadhi ya wenyeviti hao akiwemo Eliud Kaduma kutoka Kichiwa, Fredrick Damian kutoka Mihale Ninga na Ayub Kipuge kutoka kijiji cha Tagamenda wamesema wanashangaa kuona diwani,mbunge hadi Rais ambao nao ni viongozi wa kuchaguliwa kama wao wanalipwa mishahara na posho lakini wao hawapati hata posho kwa miaka mingi sasa.

“Tumekuwa tukifanyia sifa,hii sifa ya kuitwa mwenyekiti tumechoka maana hatuli na hali ni mbaya na ukizingatia kuna wengine wanapata posho na wengine wanazo lakini wanalalamika kwamba mi chache hasa sisi ambao hatuna kabisa ni shida lakini kazi tunafanya na sisi ndio wajenga nchi”alisema Eliud Kaduma mwenyekiti wa kijiji cha kichiwa Kichiwa

“Sisi wenyeviti wa vijiji tunachaguliwa kama mbunge na Mh. Rais lakini kwenye posho tumesahauliwa.Wenzetu wabunge wanapata na madiwani wanapata sasa sijajua tuna dhambi gani wenye viti wa vijiji tuliyoitenda kwenye nchi hii.Kama tunasimamia maendeleo na amani ya vijiji halafu tukatupwa kiasi hicho”alisema Ayub Kipuge kutoka kijiji cha Tagamenda

Wengine wamepaza sauti zao wakidai changamoto za miundombinu ya barabara,afya,elimu na maji na kwamba wanamuomba mbunge huyo awasaidia namna ya kuzitatua.

Akitolea ufafanuzi wa changamoto hizo mbunge wa jimbo la lupembe Edwin Enosy Swalle amesema atakwenda kuzifanyia kazi kero hizo huku akiahidi kuwaalika bungeni mwezi wa sita mwaka huu wenyeviti wote ili pia wakakutane na waziri wa Tamisemi awasikilize kilio chao.

“Hili jambo la posho ninalifahamu ninaomba nikatafutie majibu yake kwasababu nimeshalifanyia utafiti kidogo”Alisema Swalle
 
Wako sahihi kabisa, tuna vijiji around 15,000 au 20,000 serikali haiwezi kushindwa kuwalipa angalau laki moja monthly ili wafanye kazi zao bila kuomba rushwa na kula pesa na michango mbalimbali ya kijiji.

Na hiyo mishahara yao itapatikana kwa kupunguza/kumega mishahara ya wabunge ambayo ni mikubwa sanaaaaa (imagine 12 milioni kwa mwezi???)
 
Yaani mbunge anakula 12m kwa mwezi
diwani 350,000 kwa mwezi
mwenyekitiu wa kijiji 0-aka zero. hawa ndo wanabambikia raia kesi ili wapate chochote kitu
uonevu wa hali ya juu
wanakaribisha rushwa
 
Na hitimishaa....mbugee apunguziwe mshahara apewe milioni 10 plus posho inamtosha kabisaa,kwenye milioni mbili zilizo katwa kwa mbungee.....milioni moja aongezewe diwani iwe analipwa 1350000 plus posho inamtosha,wenyekiti wapewe 1000000 plus posho tunazo wapa za kutugongea mihuri,helaa za kujiunga zengo inawatosha.maamuzi yangekuwa yangu
 
Na hitimishaa....mbugee apunguziwe mshahara apewe milioni 10 plus posho inamtosha kabisaa,kwenye milioni mbili zilizo katwa kwa mbungee.....milioni moja aongezewe diwani iwe analipwa 1350000 plus posho inamtosha,wenyekiti wapewe 1000000 plus posho tunazo wapa za kutugongea mihuri,helaa za kujiunga zengo inawatosha.maamuzi yangekuwa yangu
Hii hesabu yako haiko hivyo, mbunge mmoja katika Jimbo,wakimpunguzia mil 2 anaweza kumlipa mwenyekiti mmoja na diwani mmoja katika Jimbo kwa mujibu wa hezabu hiyo.Lakini Jimbo lina kata zaidi ya 15 hivyo zaidi ya madiwani 15, vijiji au mitaa zaidi ya 100. Kupunguza hela ya mbunge hakuta saidia kuwaongeza madiwani wala kuwalipa wenyeviti wa vijiji na mitaa
 
Pesa wanazopiga kupitia hiyo mihuri yao ni kufuru. Kila wanapoenda mhuri upo kwapani. Waache kelele wenyeviti wote Tanzania kwani wanapiga hela kuliko hicho wanachodai walipwe.
Kama ni kweli hiyo nafasi haina hela, wakabidhi mihuri kwa watendaji wa kata na wajiuzulu nafasi zao kama wanaweza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom