Wenyeviti wa serikali ya mitaa wa Jimbo la Arusha mjini wametoa tamko la pamoja kutoshirikiana Gambo

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,935
5,558
Wana JF.
Kuna mkutano wa waandishi wa habari unafanyika kwenye ofisi za CHADEMA wilaya ya Arusha wenyeviti wa mitaa wanaowakilisha wananchi wametoa tamko la pamoja la kutoshirikiana na watendaji wa kata na mitaa hata mkuu wa wilaya .

Hii inatokana na kuanza kubaguliwa na mkuu wa wilaya katika utekelezaji wa majukumu yao .
Ntawaletea live update .

Tayari waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wameshafika kwenye ofisi za chama.

IMG-20160817-WA0033.jpg

IMG-20160817-WA0029.jpg

IMG-20160817-WA0032.jpg
 
Wana JF.
Kuna mkutano unafanyika kwenye ofisi za CHADEMA wilaya ya Arusha wenyeviti wa mitaa kwa wananchi kupitia waandishi wa habari wametoa tamko la pamoja la kutoshirikiana na watendaji wa kata na mitaa hata mkuu wa wilaya .Hii inatokana na kuanza kubaguliwa na mkuu wa wilaya katika utekelezaji wa majukumu yao .
Ntawaletea live update .
Tayari waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wameshafika kwenye ofisi za chama.
View attachment 383151
View attachment 383153
View attachment 383157

hakuna kitu hapo Zaidi ya kutojitambua na ubinafsi ili tukuone kambale kumbe ni mchicha mwiba
 
Leo wenyeviti wa serikali ya mitaa wa jimbo Arusha mjini wa chadema wametoa tamko lapamoja la kutoshirikiana na watendaji wa wa kata,mitaa hata mkuu wa wilaya.hii inatokana kuanza kubaguliwa na mkuu wa wilaya katika utekelezaji wa majukumu yao.
 
Attachments

  • IMG-20160817-WA0031.jpg
    IMG-20160817-WA0031.jpg
    68.5 KB · Views: 62
  • IMG-20160817-WA0030.jpg
    IMG-20160817-WA0030.jpg
    24.3 KB · Views: 63
  • IMG-20160817-WA0029.jpg
    IMG-20160817-WA0029.jpg
    77.5 KB · Views: 58
  • IMG-20160817-WA0027.jpg
    IMG-20160817-WA0027.jpg
    67.4 KB · Views: 62
  • IMG-20160817-WA0028.jpg
    IMG-20160817-WA0028.jpg
    35.9 KB · Views: 62
Leo wenyeviti wa serikali ya mitaa wa jimbo Arusha mjini wa chadema wametoa tamko lapamoja la kutoshirikiana na watendaji wa wa kata,mitaa hata mkuu wa wilaya.hii inatokana kuanza kubaguliwa na mkuu wa wilaya katika utekelezaji wa majukumu yao.

Arusha haO WENYEVITI wanavunja sheria.Kwanza hiyo takataka inayoitwa umoja wa wenyeviti wa serikali za mitaa Arusha umesajiliwa wapi? Hauko kisheria ni umoja uchwara.

Pili cheo cha mwenyekiti wa Mtaa ni cha kisiasa wakati cha mtendaji ni cha kiserikali.Wenyeviti wa serikali ni kama wabunge wa eneo la mtaani,wao na diwani wao ni wanasiasa.Mtendaji wa mtaa,kata na mkuu wa wilaya ndio watendaji wa shughuli zote za serikali za kila siku.Hawahitaji mwenyekiti wa serikali za mtaa kwenye shughuli zao,ila wakimhitaji sawa wasipomhitaji sio lazima.Mtu akitaka chochote cha kiserikali anaenda kuwaona watendaji si lazima awaone wenyeviti wa mitaa.

Wanajitutumua nao waonekane kama ni viongozi wa serikali mtaani !!! Wao sio viongozi wa serikali mtaani,kwenye kata au wilaya.

Viongozi watendaji wa kata,mitaa na wilaya Arusha endeleeni na shughuli zenu wakiwabughudhi kwenye utendaji wenu kamateni pelekeni POlisi na mahakamani wasiwapotezee muda.
 
magufuli atamaliza miaka mitano kwa siasa uchwara, hajui kazi ya upinzani ninini??
Nashangaa hoja za wapinzani analazimika kujibu yeye,
Rais ambaye atachokwa kwa muda mfupi sanaaaa
Utamchoka wewe, mimi mbele kwa mbele na Rais.Mkuu wa wilaya anawaitaji viongozi wa mitaa kwa kazi gani? Kuna watendaji wa mitaa ,watenaji wa kata, makatibu tarafa atashirikiana nao wanatosha
Na kwa sababu walishaambiwa na viogozi wao kwamba kususa ndo siasa yao ,watapingaje? Hacha waendelee tutakutana 2020 kama hadi hawajajua madhala ya kususa
 
Arusha haO WENYEVITI wanavunja sheria.Kwanza hiyo takataka inayoitwa umoja wa wenyeviti wa serikali za mitaa Arusha umesajiliwa wapi? Hauko kisheria ni umoja uchwara.

Pili cheo cha mwenyekiti wa Mtaa ni cha kisiasa wakati cha mtendaji ni cha kiserikali.Wenyeviti wa serikali ni kama wabunge wa eneo la mtaani,wao na diwani wao ni wanasiasa.Mtendaji wa mtaa,kata na mkuu wa wilaya ndio watendaji wa shughuli zote za serikali za kila siku.Hawahitaji mwenyekiti wa serikali za mtaa kwenye shughuli zao,ila wakimhitaji sawa wasipomhitaji sio lazima.Mtu akitaka chochote cha kiserikali anaenda kuwaona watendaji si lazima awaone wenyeviti wa mitaa.

Wanajitutumua nao waonekane kama ni viongozi wa serikali mtaani !!! Wao sio viongozi wa serikali mtaani,kwenye kata au wilaya.

Viongozi watendaji wa kata,mitaa na wilaya Arusha endeleeni na shughuli zenu wakiwabughudhi kwenye utendaji wenu kamateni pelekeni POlisi na mahakamani wasiwapotezee muda.
Leo umetambua kuwa kuna uvunjaji wa sheria, mnapoonyeshwa uvunjaji wa katiba unaotokana na kuzuiwa mikutano na maandamano mnajifanya kupotezea....kama leo unahitimisha kuwa wenyeviti wa serikali si chochote wakati mamlaka ya serikali yanatoka kwa wananchi, basi sitoshangaa tena ninaposoma post zako zinazowashambulia wanaotetea kuheshimiwa kwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania! Aidha, ni vizuri ukatambua kuwa umoja huanza kabla ya kusajiliwa kisheria, na nia au lengo ni muhimu zaidi kuliko karatasi ya usajili. Unaweza kuwa na taasisi iliyosajiliwa lakini ikafanya mambo ya hovyo kabisa kama tunavyoshuhudia taasisi nyingi zenye usajili wa kisheria zikifanya!
 
Back
Top Bottom