Wenyeviti wa mtaa na afisa watendaji wana matatizo au??

Solarpanel

JF-Expert Member
Oct 9, 2012
235
38
Habarini wakuu,naomba kuleta hoja hii hawa wenyekiti siwaelewi kama wanavchofanya ni sahihi,mimi nafanya kazi benki kuna fomu tunawapa wateja wetu wakasainiwe na wenyeviti kuverify makazi,lakini wanasema wanawakatalia mpaka watoe hela kama elfu kumi hivi?je ni sawa?kingine hata unapotaka kununua kiwanja ukihitaji huduma yao wanataka ten pacent ya kiwanja ulichonunua ndo wagonge muhuri.is it fair?navojua wanalipwa mshahara kwann wanafanya hivi,je kwa kuanza na huyu mmoja nimtishieje ili aache kuwatesa wateja hivi
 
kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake, rushwa ipo duniani kote ila bongo imezidi kinachofanyika hapo wanakuomba hela ya kuendesha ofisi lakini pia inategemea na ishu unayoenda kufanya mfano barua ya udhamini ndugu yako kaswekwa ndani utachajiwa buku au buku 2 kama huna wanasamehe na wengine njaa wanakukomalia kwa ishu ya kiwanja lazima wakupige hela si unazo na huwezi kuwafanya chochote hao ndo serikali iyo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom