Wenyeviti wa CCM: uamuzi wa kujivua gamba utenguliwe

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa wamepania kushinikiza kutenguliwa kwa uamuzi wa CC kuhusiana na mkakati huo wa kuwataka makada wake kujivua gamba, Mwananchi limeelezwa.

Mmoja wa wenyeviti hao alisema jana kwamba wanasubiri kwa hamu mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) akisema hawako tayari kuona chama kikisambaratika. “Subirini halmashauri kuu mtasikia, haya wanayoyataka hayana maslahi kwa chama ni makundi ya urais mwaka 2015.” alisema.

My Take: Inaonekana hawa wenyeviti hawawezi kuishi bila ufisadi na je uamuzi ukitenguliwa Rostam aliyejiuzulu watamuomba arejee kazi zake.

Mwananchi.
 
Wakiwavua gamba mapacha watatu kwa nguvu, ccm itakufa ghafla - wanafedha nyingi na siri nyingi sana za jk na serikali yake, wakiwaacha wote waliobaki huku wakiwa wameshawaita mafisadi, ccm itakufa taratibu itafika labda 2015. Chaguo analo kikwete aliyeanzilsha sarakasi hili. Tunamshauri ajiandae kuwakabidhi Chadema nchi 2015. No way out.
 
Hao wenyeviti watambue kuwa shuka likichafuka sio kupulizia perfume bali ni kulifua. Na kitanda chenye kunguni ni kuchoma moto tu. LOWASSA NA CHENGE ni bora kuliko CCM!?? Wa Tz tunaona, tunasikia, tunafuatilia na kuyajadili yoote. OLE WENU, mwendelee kuwa na kigugumizi, mtakiona 2015.
 
Baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa wamepania kushinikiza kutenguliwa kwa uamuzi wa CC kuhusiana na mkakati huo wa kuwataka makada wake kujivua gamba, Mwananchi limeelezwa.

Mmoja wa wenyeviti hao alisema jana kwamba wanasubiri kwa hamu mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) akisema hawako tayari kuona chama kikisambaratika. "Subirini halmashauri kuu mtasikia, haya wanayoyataka hayana maslahi kwa chama ni makundi ya urais mwaka 2015." alisema.

My Take: Inaonekana hawa wenyeviti hawawezi kuishi bila ufisadi na je uamuzi ukitenguliwa Rostam aliyejiuzulu watamuomba arejee kazi zake.

Mwananchi.

Hawa ni Guninita na wenzake wachache ambao maisha bila Lowassa, Chenge na Rostam hayaendi. The guy amekuwa job less na jiko la nyumbani kwake haliwaki bila "Miungu" hawa. Unategemea nini maskini?
 
Guninita kamaliza secondary lini ?Mwaka jana alikuwa kidato cha pili.
 
Hawa ni Guninita na wenzake wachache ambao maisha bila Lowassa, Chenge na Rostam hayaendi. The guy amekuwa job less na jiko la nyumbani kwake haliwaki bila "Miungu" hawa. Unategemea nini maskini?
Si wachache ndugu Mbopo Mkoa wa Shinyanga wamemwambia Nape akienda huko aende na majibu ya umeme siyo maneno ya magamba, hata Kagera nafikiri hivyo hivyo, kidogo kidogo tunaanza kuona watu wanasimama na kuhesabiwa, Lowassa at work.
 
Ukienda hata sumve utakuta sisiem yalia,
Mapacha watatu mapacha wa tatu SISIEM yaliaaaH!

Hata pande za Bukoba Sisiem yaliaaaaH
Mapacha watatu mapacha wa tatu SISIEM yaliaaaH!

Na Bungeni wakibanwa na chadema Sisiem yaliaaaah
Mapacha watatu mapacha wa tatu SISIEM yaliaaaH!

Pacha mmoja kangatuka Sisiem yaliaaah
Mapacha watatu mapacha wa tatu SISIEM yaliaaaH!

Kalivua gamba lake Sisiem yaliaaah
Mapacha watatu mapacha wa tatu SISIEM yaliaaaH!

Wanapanga mikakati pacha wawili wasivue sisiem yaliah
Mapacha watatu mapacha wa tatu SISIEM yaliaaaH!

Watanzania wamechoshwa na pacha tatu sisiem yaliaah
Mapacha watatu mapacha wa tatu SISIEM yaliaaaH!

Sisiem yategemea mapacha watatu sisiem yaliaah
Mapacha watatu mapacha wa tatu SISIEM yaliaaaH!
 
Si wachache ndugu Mbopo Mkoa wa Shinyanga wamemwambia Nape akienda huko aende na majibu ya umeme siyo maneno ya magamba, hata Kagera nafikiri hivyo hivyo, kidogo kidogo tunaanza kuona watu wanasimama na kuhesabiwa, Lowassa at work.

Wana JF,

My Take: Hawa Wenye/K wa CCM mikoa nadhani hawajajua nini kazi ya Nape na Ngeleja nadhani wao ni wana ile itikadi ya CCM kwanza na sio Nchi sasa nape ni wapi na wapi na Umeme? Magamba ndio kazi ya nape kuyakusanya na kuyachoma wao hao wezee wa CCM ni wanafiki sana wame kuwa vibarka wa hao mafisadi njaaaa
 
Jethro kumbuka hao wazee(nec) ndio waliompa kazi Nape ndio wanaoijua CCM Nape ni wa juzi tu kama wakiona anakwenda kinyume kwa nini wasimwambie. Halafu elewa wako wengi na pesa zinatoka huko.
 
Si wachache ndugu Mbopo Mkoa wa Shinyanga wamemwambia Nape akienda huko aende na majibu ya umeme siyo maneno ya magamba, hata Kagera nafikiri hivyo hivyo, kidogo kidogo tunaanza kuona watu wanasimama na kuhesabiwa, Lowassa at work.

Sasa unaposema Shinyanga si unamzungumzia Mgeja ambaye baada ya kumtaja Mungu, huwataja Lowassa na Chenge kama Miungu wake. Wana nafasi kubwa kuliko wazazi wake.
 
Eti wenyeviti wa ccm... utadhani ni weengi wa kuyumbisha NEC, kumbe sana sana ni Mgeja ambaye naye atatakiwa kuvuliwa gamba, Guninita ambaye ni ex darasa la saba, na Kusila wa Dodoma. Wengine hawako tayari kujitoa muhanga kwa ajili ya mafisadi watatu,... na wanajua hata wakisusa na kuamua kuanzisha chama, kupata wanachama itakua ni kazi kubwa. Sababu kila mwanachama mpya akija atauliza "mtanikatia shilingi ngapi"... Ni tofauti na vyama vinavyoongozwa na dira ya kulikomboa taifa. Hao ni genge la kulitafuna taifa!
 
chama cha magamba, kila kukicha kujigamba ,
yale yale ya Mramba, kutufanya sie washamba,
fedha zote kalamba, tena kwa umwamba,
kashiba hata kajamba, sie kafunga kamba,
eti lazima tule nyasi, jidege liwe masalo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom