Wenyeviti wa CCM mikoa yote, Wataoa Pongeza kwa Rais MAgufuli, Makamu wake Mama Samia Suluhu

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,194
1,416
TAMKO LA WENYEVITI WA CCM MIKOA LA KUPONGEZA USHINDI WA RAIS NA MAKAMU WA RAIS MHESHIMIWA DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI NA MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN


Sisi wenyeviti wa CCM wa Mikoa yote ya kichama katika Jamhuri ya Munngano wa Tanzania, tunawapongeza Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa ushindi walioupata katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Tarehe 25/Oktoba/2015.

Sanjari na pongezi hizo tunawashukuru wanaCCM na wananchi kwa ujumla wao kwa kukipigania na kukichagua Chama cha Mapinduzi katika nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais na hivyo, kukiwezesha kuwa Chama Tawala kinachounda Serikali itakayowatumikia Watanzania wote kwa miaka mitano ijayo.

Katika kampeni zilizoendeshwa kote nchini, Dkt Magufuli aliahidi, Watanzania watakapomchagua kuwa Rais wa nchi yetu, atatekeleza kwa juhudi na maarifa masuala yafuatayo; (i) kuondoa umaskini; (ii) kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana; (iii) kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma; na (iv) kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama kwa maisha ya wananchi na mali zao. Alisisitiza kutowaangusha Watanzania kwa kauli mbiu yake isemayo ?Hapa Kazi Tu?.

Sisi Wenyeviti wa CCM wa Mikoa, tunaungana bega kwa bega na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020, kwa ufanisi mkubwa. Tunamwomba Rais Magufuli aendeleze kasi yake ya kutekeleza majukumu yake na asisite kuwawajibisha watendaji wote wazembe wanaozalisha kero ya utoaji huduma duni kwa wananchi. Sisi tutazidi kuungana nae katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye mikoa yetu na kuzihimiza ngazi zote za uongozi wa Chama kufanya hivyo bila kusababisha muingiliano wa kimajukumu.

Aidha tunampongeza Mhe. Rais kwa uteuzi ulioufanya hivi karibuni wa nafasi ya Waziri Mkuu kwa kumteua Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa. Uteuzi huu umeonesha mwelekeo wa aina ya Baraza la Mawaziri analotegemea kuliunda na hazina kubwa ya viongozi wachapakazi na wanyenyekevu na watumishi bora wa umma waliopo ndani ya CCM.

Sisi Wenyeviti wa CCM wa mikoa, tutakuwa hatukumtendea haki, kama tutaacha kumpongeza Mhe. Rais kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa kwenye ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hotuba ile ni mwongozo na mwelekeo wa Tanzania tunayoitarajia, na imehuisha matumaini ya Watanzania na kuleta ari ya uzalendo na haja ya kulitumikia taifa lao.

Tumefadhaishwa na vitendo vya ukosefu wa nidhamu, vilivyofanywa na wabunge wa kambi ya upinzani vya kupiga kelele na kusababisha kutolewa nje kabla ya Mhe. Rais kutoa hotuba yake. Chama Cha Mapinduzi, kinazitaka mamlaka zinazoendesha vyombo vya Bunge na Baraza la wawakilishi kuchukua hatua stahiki kukomesha vitendo kama hivyo kwa vile vinadumaza demokrasia. Tunawaasa Waheshimiwa Wabunge kuwa mfano wa mwenendo bora na desturi za jamii wanayoiongoza.

Aidha Wenyetivi wa CCM wa mikoa, tunazipongeza na kuziunga mkono hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Mhe. Rais za kubana matumizi ya umma kuziba mianya ya rushwa, kupiga vita ubadhirifu wa mali ya umma na kurejesha nidhamu na uwajibikaji kwenye vyombo mbalimbali vya umma na nchi kwa ujumla. Ni muhimu kwa waTanzania wote na hasa wanaCCM kuziunga mkono jitihada hizi za Mheshimiwa Rais, kwa sababu anachokifanya ni kuziishi ahadi tisa za mwanachama wa CCM kama zilivyoainishwa kwenye katiba ya CCM ya mwaka 1977; toleo la mwaka 2012, Nyongeza A, ukurasa 199! Ahadi hizi ndio uti wa mgongo wa hatua hizi zinazochukuliwa na Mheshimiwa Rais.

Mwisho; tunawaombea Rais Magufuli na wasaidizi wake wote afya njema na hekima itokayo kwa MwenyeziMungu katika kutekeleza kazi zao kwa wepesi na kasi, ili kuleta maendeleo endelevu, kukuza umoja wa kitaifa na kuimarisha mustakabali wa nchi yetu na watu wake.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,

MUNGU IBARIKI AFRIKA,

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!

Imetolewa na Wenyeviti wa CCM wa Mikoa yote
06 December, 2015

Kwa Hisani ya Channel Ten
 
Sioni ukali wa tamko,kichwa cha habari hakiendani na habari yenyewe!
 
Sioni ukali wa tamko,kichwa cha habari hakiendani na habari yenyewe!

Hawa makanjanja ambao pia ni mburula hawajui kuwa kutoa TAMKO KALI ni kukalipia kitendo husika ; hawa wanaojiita wenyeviti wa magamba hawakukalipia bali walitoa pongezi kwa mheshimiwa Rais JPM!!
 
unafki, kwanza hawajasema ahadi zote za makufuli
kama wanalaumu wapinzani kuzomea kwa kumkataa sheni, na kumpongeza kwa kumchagua Majaliwa haraka kuwa waziri mkuu kwa nini wasimlaumu kwa kuchelewa kuchagua baraza la mawaziri?
 
Jamani muda wote huo mlikuwa mnaandaa tamko hili tu!?

Tamko hili limetolewa baada ya mwezi mmoja. Hii ni baada ya Rais kuchukua hatua kadhaa kiutendaji. Sasa wewe ulitaka tamko hili litolewe lini? Au ulitaka litolewe siku ya kwanza tu? Wakati mwingine tunalazimika kutafakari kwanza kabla hatujatoa hoja.
 
Hili ni karipio kwa wote mnaopinga juhudi za Dr. JPM Kama wewe huku mkikisingizia chama. ACHA MARA MOJA!!!

Queen Esther

Hawa makanjanja ambao pia ni mburula hawajui kuwa kutoa TAMKO KALI ni kukalipia kitendo husika ; hawa wanaojiita wenyeviti wa magamba hawakukalipia bali walitoa pongezi kwa mheshimiwa Rais JPM!!
 
Pointi kubwa ni kwamba; kuna watu watu walikuwa na labda bado wanasubiria CCM ijaribu kumfunga Gavana Magufuli; ili kwamba waweze kusema si tulisema "CCM ni ile ile"? Sasa ikitokea kwamba kweli CCM nayo ikasoma namba ya Magufuli ikajipanga nyuma yake na Kikwete akaachia pia Uenyekiti wa CCM kama inavyotarajiwa na baadhi yetu ina maana hata fisi anaposubiria mkono wa mtu anayetembea uanguke ili aunyake anaweza kufika mahali akasema tu "duh hauanguki huu".
 
Your wisdom is unexplainable. Thank you Mzee Mwanakijiji. We need more of your kind in JF.

Queen Esther

Pointi kubwa ni kwamba; kuna watu watu walikuwa na labda bado wanasubiria CCM ijaribu kumfunga Gavana Magufuli; ili kwamba waweze kusema si tulisema "CCM ni ile ile"? Sasa ikitokea kwamba kweli CCM nayo ikasoma namba ya Magufuli ikajipanga nyuma yake na Kikwete akaachia pia Uenyekiti wa CCM kama inavyotarajiwa na baadhi yetu ina maana hata fisi anaposubiria mkono wa mtu anayetembea uanguke ili aunyake anaweza kufika mahali akasema tu "duh hauanguki huu".
 
Wanaweweseka hao maana ni miongoni walioidhoofisha nchi kwa zaidi ya miaka 40. Na walikuwa wanajivunia kuwa chama tawala kisichoisaidia nchi kuendelea
 
Hawa makanjanja ambao pia ni mburula hawajui kuwa kutoa TAMKO KALI ni kukalipia kitendo husika ; hawa wanaojiita wenyeviti wa magamba hawakukalipia bali walitoa pongezi kwa mheshimiwa Rais JPM!!


Hawa wenyeviti wa Magamba ni sharti sasa wajipendekeze kwa Magufuli kwani wengi wa hawa hawa wenyeviti ndio waliokula hela nyingi za Lowassa na kujiapiza kuwa asingeteuliwa pangechimbika!!! Sasa wanaona Magufuli anavyochacharika hawana jinsi bali kumuunga mkono!! Kimbisa nae si mwenyekiti na alijitokeza kupinga uteuzi wa Magufuli!! Lakini Magufuli amewagundua kuwa wengi wao ni wanafiki!
 
Hivi Tanzania hakuna mtu mwenye mawazo ya maendeleo ya jamii yake anayoiongoza ni mpaka tuige ya Raisi naona uwekwe muongozo wa kila kiongozi kutoa mahitaji ya sehemu yake husika anayoongoza na kuwaletea wananchi wake maendeleo. kila wakat unasikia tunaunga mkono hotuba ya Raisi je nyinyi viongozi mlikua wapi msitoe matamko yenu sahihi kwa eneo husika? Mmekua viongozi kwa muda mrefu mnatokea tu kuunga mkono hotuba ya Raisi kila wakati, naona hamfai kuongoza waje watu wenye misimamo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom