Wenyeviti UKAWA wanamtaka Lowassa, makatibu na wanachama wengi hawataki

East African Eagle

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
3,759
2,205
Kuna taarifa kuwa wenyeviti wa UKAWA ndio wanamtaka Lowasa kwa udi na uvumba lakini makatibu wakuu wa vyama vyote vinavyounda UKAWA na wasaidizi wao na wengi wa wanachama wa kawaida wa UKAWA hawamtaki Lowasa ndani ya UKAWA.

Hali ni mbaya mno hasa kwa upande wa Zanzibar.Vikao vizito vinaendelea na vinaendeshwa usiku na mchana lakini bado nguvu ya kumkataa Lowasa kwenye UKAWA ni kubwa mno imewafanya wenyeviti kuanza mawasiliano upya ya kutafakari upya kuhusu Lowasa.

Kuna uwezekano mkubwa wa LOWASA jina lake Kukatwa asiwe mgombea ndani ya UKAWA ili kuokoa hali ya sintofahamu iliyoibuka ndani ya vyama hivyo upande wa bara na visiwani.

Akikatawa itakuwa ndio mwishio wa Safari ya matumaini yake hewa kwani tume ya uchaguzi imeshatoa ratiba ya wagombea uraisi wa vyama vyote kasoro vinavyounda UKAWA.

Ina maana akikatwa tu hatakuwa na chama kingine cha kwenda sababu chama cha mwisho kuchukua fomu ni chenye mgombea kutoka UKAWA.

Je, akikatwa atarudi CCM mbio au atabaki kuijenga CHADEMA hakuna ajuaye isipokuwa Lowassa Mwenyewe.
 
Lowassa kuteuliwa kuwa Mgombea wa Chadema kwenye Kikao cha Kamati kuu tarehe 26 July 2015 kilichofanyika Bahari Beach kwa Mujibu wa Mh.Mbowe, Salum Mwalimu na Tundu Lissu, Mh.Lowassa kakoma kuwa Mwanachama wa Ccm tarehe 30 July 2015 ina maana kamati kuu ilimpendekeza Kuwania Urais akiwa bado ni Mwana CCM huu ni uvunjaji mkubwa wa Taratibu, sheria na Kanuni, Kama Lowassa analalmika kuvunjwa kwa taratibu Ccm hata Chadema nao wamevunja taratibu.Chadema imeanza kuiga tabia za Ma Ccm
 
huo udaku peleka lumumba na ukawaombe na buku saba zako

Tuna taarifa za uhakika kuliko wewe.Nikueleze sasa Lowasa atakapokuwa anarudisha fomu katibu mkuu wa CHADEMA Dk.Slaa hatakuwepo ambaye ndiye alitakiwa apokee hiyo fomu!!! Kasusa.Upo hapo.Nakupa hiyo kama ilivyo we CHADEMA mnywa viroba.
 
Hivi Ukawa wakishindwa si ndio furaha yenu? Sasa kivipi tena mnajidai mnahuruma?
 
Kuna taarifa kuwa wenyeviti wa UKAWA ndio wanamtaka Lowasa kwa udi na uvumba lakini makatibu wakuu wa vyama vyote vinavyounda UKAWA na wasaidizi wao na wengi wa wanachama wa kawaida wa UKAWA hawamtaki Lowasa ndani ya UKAWA.Hali ni mbaya mno hasa kwa upande wa Zanzibar.Vikao vizito vinaendelea na vinaendeshwa usiku na mchana lakini bado nguvu ya kumkataa Lowasa kwenye UKAWA ni kubwa mno imewafanya wenyeviti kuanza mawasiliano upya ya kutafakari upya kuhusu Lowasa.

Kuna uwezekano mkubwa wa LOWASA jina lake Kukatwa asiwe mgombea ndani ya UKAWA ili kuokoa hali ya sintofahamu iliyoibuka ndani ya vyama hivyo upande wa bara na visiwani.Akikatawa itakuwa ndio mwishio wa Safari ya matumaini yake hewa kwani tume ya uchaguzi imeshatoa ratiba ya wagombea uraisi wa vyama vyote kasoro vinavyounda UKAWA.Ina maana akikatwa tu hatakuwa na chama kingine cha kwenda sababu chama cha mwisho kuchukua fomu ni chenye mgombea kutoka UKAWA.Je akikatwa atarudi CCM mbio au atabaki kuijenga CHADEMA hakuna ajuaye isipokuwa Lowassa Mwenyewe.

Historia inaonesha kuwa vipindi fulani katika mstakhabali wa nchi unalazimisha kupima nini ni janga zaidi ya jingine. Marehemu Samora Machel na Frelimo walikubali kutia saini Mkataba wa Nkomati wa ushirikiano na Makaburu kama mkakati wa kujinusuru na kutoa nafasi kukabiri janga kubwa kuliko zote wakati huo la kuondolewa serikali ya Frelimo na Renamo ikisaidiwa na Makaburu. Wakomunisti wa Afrika ya Kusini waliingia ubia na ANC ya mabwanyenye weusi ili kutokomeza kwanza ukaburu na mapambano na ubepari yaje baadaye. Katika Vita Kuu ya Dunia ya Pili wakomunisti walishirikiana na mabwenyenye wa mrengo wa kulia na kati kutokomeza janga kubwa zaidi wakati huo la ufashisti, yaani ubepari wa mrengo wa wa kulia kupitiliza. Hivyo hivyo mapambano ya kuleta uhuru wa Tanganyika yalivyo unganisha nguvu za mabwenyenye wazungu na waasia pamoja na zile za wakulima na wafanyakazi wa rangi zote kwa azimio lile la mkutano mkuu wa Tanu wa 1958 pale Tabora. Hivyo hivyo Mandela na ANC waliingia "urafiki wa mashaka" na De Clerk kiongozi wa Makaburu ili kuondolewa ukaburu kuwe kwa amani ya "kula matapishi" ya kuwalaani huko nyuma kuwa ni wabaya wa Mwaafrika!!

Mabadiliko ya haraka haraka yanayoendelea hapa Tanzania yenye lengo la kuondoa CCM madarakani kama chama dola kinachodumaza na kudhoofisha ushindani wa kisiasa miongoni mwa mabwenyenye wa tabaka tawala Tanzania ni mabadiliko yatakayoleta neema kwa Watanzania wote. Ile tu CCM kudhoofishwa na kujiunga UKAWA kwa Lowassa ni kuvuja kwa pakacha ambayo ni nafuu ya mchukuzi.....Nikuondoa kizingiti kikuu cha kushamiri kwa demokrasia pana na maendeleo endelevu Tanzania ambacho ni kuhodhiwa na ukiritimba wa chama dola cha CCM kinachojinadi kama chama cha mrengo wa kushoto wakati ni chama cha mrengo wa kulia kama vyama vyote vya siasa Tanzania kwa sasa.

Kumeguka kwa CCM-Mambo Leo kama taasisi ya kakundi ka wana mtandao ulioingiza serikali ya sasa ya Tanzania madarakani mwaka 2005, ni faraja kwa wote wenye kuitakia mema nchi hii na ni kiashiria cha kukomaa kwa vuguvugu la ukombozi wa pili wa Tanzania utakaochukua sura ya demokrasia zaidi ili kuwa na maendeleo endelevu zaidi yapatikane kupitia kupatikana nafasi chanya zaidi ya kupitishwa kwa Katiba Mpya kama ilivyopendekezwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Kwa mara ya kwanza vyama vy siasa vya upinzani kiuhalisia (tofauti na vile ambavyo vimebebwa na watawala wa sasa kwa lengo la kuua upinzani wa kisiasa kijanja kijanja kama ACT- Wazalendo), sasa vimeunganishwa na kupigania Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Jaji Warioba ( UKAWA) badala ya kuunganishwa na kutaka kuondoa CCM madarakani pekee.

Ghafla mwanasiasa mwenye nguvu nyingi ndani ya chama cha kifisadi cha CCM, mwanasiasa ambaye umaaarufu wake umetokana na kuongoza mtandao uliouweka utawala wa sasa wa CCM madarakani, Ndugu Edward Lowassa, amekasirishwa na kukatwa jina lake na aliodhani ni rafiki zake ndani ya CCM na kuamua kusema basi na lolote liwe kwa kujiunga na vuguvugu la kupigania katiba mpya!! Naye sasa kang'amua kuwa Katiba ya sasa na ile Pendekezwa ni za ovyo maana haziruhusu kuwepo mgombea huru bila mizengwe. Hasira za Lowassa zimezaa tunda zuri la kug'amua kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko kupitia Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Hasira hizi za mkizi ni furaha ya kunguru na ni busara kwa viongozi wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla kutoongopa "kula matapishi yao" kwa kumkaribisha Ndugu Lowassa...huyu huyu waliomwita fisadi... kujiunga na UKAWA na kugombea urais. Nafasi ya kihistoria imejitokeza ya kukiondoa CCM madarakani kwa amani!!

Sishangai wasaliti wa vuguvugu la kukiondoa CCM madarakani wanatushauri sisi Watanzania wenye shauku ya kuutumia upenyo huu wa mpasuko ndani ya CCM kukiondoa CCM madaraka!!! Eti tuombe radhi kwa" kula matapishi yetu" wote tulio wahi kumwita Lowassa fisadi! Wao wanataka tuendelee kuvumilia kutawaliwa na CCM labda kwa miaka mitano au zaidi hivi mpaka chama kipya cha watakatifu kiitwacho ACT-Wazalendo kitakapo kuwa tayari kututawala badala ya CCM!! Sishangai kusikia ushauri huu kutoka kwa wasaliti hawa ambao kazi yao hata huko nyuma imekuwa ni kuudhoofisha upinzani dhidi ya CCM na kukisaidia CCM kiendeleee kuwa madarakani!! Hawa jamaa ni wasomi sana na ni wajanja sana, ilo lazima kulikiri!!!

Sitashanga kama haya ninayoyasema yatapigwa madongo na wasaliti hawa!! Historia itakapoandikwa baada ya UKAWA kupata viti vingi zaidi Bunge lijalo au hata kuutwaa urais na kupata Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba, itawapa hukumu yao stahiki, wajanja na welevu hawa! Bila shaka wanaoomba UKAWA ishindwe kupata viti vingi Bunge lijalo na iukose urais na hivyo tuendelee kutawaliwa na CCM na wao wapate viti vya kutosha kuwa viongozi wakuu wa eti upinzani muruwa wenye maadili ya Azimio la Arusha Tanzania!! Ni haki yao ya binadamu kuendelea na matumaini haya kama na sisi tulivyo na haki ya kuendelea na matumani yetu ya uwezakano wa ushindi mnono chini ya UKAWA dhidi ya ukiritimba wa chama kimoja chama dola cha CCM!

By Mwl. Lwaitama
 
Nyumba yenu inaungua moto, ninyi mnazurura huku! Nape, Mwigulu, Mahiga, Kilango wamekamatwa na TAKUKURU wakihonga wapiga kura. Ndugai na Wassira kidogo waue watu kwa vipigo. Hangaikeni kwanza na nyumba yenu inayoteketea, haya ya huku hayawahusu, sisi tumeamua ni Lowassa tu, hakuna mwingine!!!!!!!
 
Samora Machel na Frelimo, Mandela na ANC na hata Arafat na Fatah yake ni kweli waliwekeana Mkataba na Maadui zao, Chadema haijaweka Mkataba na Wanamtandao ilichofanya ni kuwakabidhi Chama kuongoza Mapambano na hilo ndo kosa lao kubwa walofanya, Lowassa kama angesaini MOU na Chadema kuindoa Ccm wakashirikiana huku Chadema ikiendelea na misimamo na Mikakati yao isingekuwa shida, Shida ni kulazimisha kubadilisha Gia angani kinguvu huku Wenzio wakiwa wanabisha. unadhani kama Mbowe na Mzee Mtei wangekuwa hataki Lowassa aje Chadema Slaa, Tundu Lissu na Mnyika wangethubutu kumleta??
 
Ukiwa jamii forum waweza dhani Lowasa anapendwa sana. Fanya utafiti mtaani kwako. Waulize nani unataka awe rais awamu hii? Kwa utafiti niloufanya unaonesha lowasa haweziki kuwa Rais endapo uchanguzi ungefanyika wiki hii. Kampeni zikianza labda maoni ya watu yaweza badilika. Najua kuna watu watakuja kukanusha bila utafiti. Ukweli ni kwamba nguvu ya El imekuzwa na media na ni ya kufikirika. Na watu wanaounga mkono humu ni sehemu ndogo tu ya jamii ya watu wenye access na jamii forum. Wasomi wengi wameapa kutompigia kura Lowasa. Wamebakia Nyumbu ndo watakao mpigia kura.
 
Aletwe. .kwa kuwa umeleta mzaha..hapa bar kuna wenzako wamekula kuku wameomba mfuko waondoke na mifupa
 
utafiti umefanya chumbani kwako ....we angalia magamba yanavyoweweseka mitandaoni na press conferency ndio utajua nguvu ya lowasa
 
huyu jamaa anamaanisha uraiani kuna wasomi kuliko jf , kweli naanza utafiti mpya juu yako
 
Kwa taarifa yako kama watu 4 kati ya 10 wanamkubali kabla ya kampenj, basi baada ya kampeni ni mshindi, pia wasomi ni wachache nchii ujue hilo
 
Back
Top Bottom