Wenyeviti Taifa wa CCM wanafanana? Kwa nini wanarudia yaleyale?

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Kuna jambo moja la kustaajabisha sana ambalo lipo na linatokea kila awamu.
Lakini kinachonishangaza ni namna ambapo Jambo hilo hushughulikiwa ili liishe na mara zote haliishi vizuri.
Mwinyi akiwa raisi alikuwa na watu ndani ya chama ambapo walikuwa hawamtaki na walikuwa wakimkosoa, mmoja wao alikuwa Prof.Kighoma Malima na suala lake halikuisha vizuri.
Hayati Mkapa nae alikumbana na wasiontaka ndani ya chama, mfano ni Holace Kolimba na kupelekea kilichotokea.
Kikwete naye aliingia kwenye misukosuko ya kutokukubaliwa na wanachama baadhi ambao ni nguli Kama Sitta, Mwakyembe, Mwandosya na Lowassa.
Kilichotokea nadhani tunakumbuka Mwakyembe na Mwandosya kupewa sumu.
Hayati Jiwe, nae alikutana na wapinzani ndani ya CCM ambao walikuwa hawakubaliani nae na ikapelekea Kinana,Makamba na Membe kuitwa kamati kuu na kumfuta Membe uanachama.
Yote haya hayakua sawa.
Mama Samia sasa hivi nae amekutana na wapinzani ndani ya chama, njia ya kuwashughulikia ni ileile, wote njia zinafanana.
Bado najiuliza kwani mkiwa na madaraka mkikutana na wanaowapinga hamuwezi kuwavumilia tu?
Iweje mtake kupendwa na kila mwanachana wenu? Mbona katika Hali ya kawaida ni kitu hakiwezekani?
Mnasema mnawanachama zaidi ya mil10, Sasa wote Hawa wawe wanakupenda na kukubaliana na uongozi wako? Haiwezekeni.
Wenyeviti CCM vumilieni wapinzani wenu ndani ya chama.
Maneno ya Kolimba sikuwahi kuona kama ni ya hatari Sana, sikuona maneno ya Mwakyembe pia Kama ni hatari, sikuona Kama maneno ya membe ni hatari na bado sijaona Kama maneno ya polepole ni ya hatari.
 
Sisiyemu wanaamini siku zote wao wako sawa. Pia imani yao wanaamini ukiwa mwana chama lazima usitofautiane na mwenyekiti wako. Matokeo yake ni aya tunaona leo.
 
Back
Top Bottom