Wenyeji wa Iringa: Lugalo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenyeji wa Iringa: Lugalo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kipala, Jul 7, 2009.

 1. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,448
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Naomba usaidizi wa wenyeji wa Iringa!
  Kijiji cha Lugalo ni mahali pa kihistoria ambako wakoloni Wajerumani walishindwa mara ya kwanza na jeshi la mtemi Mkwawa kiongozi wa Wahehe. Nataka kuboresha makala ya wikipedia juu ya [ame="http://sw.wikipedia.org/wiki/Lugalo"]Lugalo[/ame] lakini sijui inahesabiwa katika kata gani?? Nisipokosei iko [ame="http://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya_ya_Kilolo"]Wilaya ya Kilolo [/ame]je ni kweli? Nani anajua ni kilomita ngapi kutoka Iringa hadi Lugalo?
   
 2. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kilolo, ni kweli ipo wilayani Kilolo kama ubongo wangu upo salama.... kilomita kwa kweli sina uhakika lakini kutokea mjini labda zinaweza zikawa kama 45km or so...
   
 3. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,448
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mzee Morani 75, hizi 45 zako zimeshafika wikipedia! Ninavyokumbuka inawezekana basi.
   
 4. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Sorry mie nilijua ilipo shule ya Lugalo juu karibu na mlima kuna mashimo mengi ndo Mkwawa alijenga mahandaki akipigana na wajerumani, maana tukisoma hapo tulikuwa tukiuliza haya ni mto ni nini tukaambiwa ni mahandaki kumbe sivyo?????
   
 5. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,448
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Asante MamaJoe kama wewe ni mwenyeji je unajua Lugalo ni kata gani??

  Juu ya mahandaki sidhani ni sahihi. Handaki ni mbinu wa vita pale ambako jeshi zinatazamana na kupigana kwa muda mahali pamoja.

  Taarifa za Wajerumani zinasema ya kwamba kikundi chao kilishambuliwa na Wahehe walipopita kwenye manyasi marefu; njia ilikuwa nyembamba sana kwa hiyo walitembea kwa safu ndefu na kamanda Mjerumani aliyedharau Wahehe hakutuma wapelelezi kuangalia njia. Kikundi cha Wajerumani kilichinjwa katika muda wa dakika kumi.
  Angalia habari yake kwa Kiswahili hapa:
  Emil von Zelewski - Wikipedia, kamusi elezo huru
  (wikipedia ya Kiswahili)

  au kwenye wikipedia ya Kiingereza hapa:
  [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Hehe"]Hehe - Wikipedia, the free encyclopedia[/ame]
  (ndani yake tafsiri ya taarifa ya luteni tettenborn aliyeongoza Wajerumani waliofaulu kujiokoa)
   
 6. f

  fkstetes New Member

  #6
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Lugalo ni sehemu muhimu ya kihistoria katika nchi yetu hii. Lugalo iko katika kata ya Irole tarafa ya Mazombe wilaya ya Kilolo. Mahali hapa ni kilomita 22 kutoka Iringa katika barabara kuu iendayo Morogoro na ni kabla ya kufika Ilula eneo maarufu kwa kilimo cha nyanya.

  Lugalo ni rahisi kupafahamu kwani pana mnara ambao ndipo Jemadari wa Kijerumani alipofia na kuzikwa kwa pamoja na wenzake tisa. Jemadari huyu alifahamika kwa jina la Zelewisky au Nyundo. Wahehe huuita mnara huu Kaburi la Nyundo.

  Ukiwa mahali hapa, magharibi yake kuna misheni ya zamani sana iko mlimani (inaonekana kwa urahisi) inaitwa Irole ambayo enzi zake ilimiliki shule ya Irole lower na middle school ambayo imetoa watu wengi maarufu waliostaafu na walioko kazini serikalini, sekta binafsi pia wafanya biashara maarufu. Lakini leo hii misheni ya Irole pia shule hii hali ni ya kusikitisha. Vyote kwa pamoja (misheni, shule) inahitaji misaada wa kuiinua/kuiboresha.

  Watu waliosoma shule hii ya Irole pia waliopata huduma za kiroho misheni ya Irole na watu mbalimbali tufanye harambee tuikwamue. Sasa hivi Watanzania tunahamasishwa kufanya utalii wa kutembelea rasilimali za Taifa (mbuga za wanyama n.k) basi tuzijumuishe pia sehemu za shule zetu tulizosoma toka chekechea (shule za vidudu enzi hizo) hadi vyuo elimu ya juu, kutalii kujionea mabadiliko yaliyopo.

  Kwa upande wa mashariki ukiwa hapa Lugalo asilia kuna mlima ambapo una pango kubwa na juu yake kuna maji meupe yanayotiririka. Pango hili ndipo pia majeshi ya Mkwawa (Mkwavinyika) yalijificha. Majeshi ya Kijerumani yalipopita maeneo haya walishitukia wakishambuliwa kutoka kwa nyuma na hawakuwa na sehemu ya kukimbilia kwani mbele yao kulikuwa na gema au maporomoko marefu ya mlima na hapa wakauawa kwa urahisi.
   
 7. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,448
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Jina la jemadari Mjerumani ni "Zelewski" - asante kwa jina la kienyeji! (Imeingia tayari hapa kwenye wikipedia: [ame]http://sw.wikipedia.org/wiki/Emil_von_Zelewski[/ame]).
  Jiwe la kumbukumbu liliwekwa na Wajeruma ni baada ya miaka kadhaa waliporudi tena kwa nguvu.

  Hakuna uhakika juu ya makaburi tena sijui kama walizikwa - je Wahehe wa kale walizika maiti za maadui?

  Majina kwenye jiwe ni yale ya maafisa na maafande Wajerumani tu - wale askari na wapagaji Waafrika waliokufa (zaidi ya Waafrika 350 waliokuwa upande wa Wajerumani) hawakuandikwa majina yao.

  Nisipokosei Wahehe walijenga jiwe la pili ng'ambo ya barabara kuu kwa ajili ya watu wao.
   
  Last edited: Jul 9, 2009
 8. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Ahsante kwa shule nzuri JF ni kweli ni mwenyeji huko, ila nimekulia sehemu nyingi, lakini pia ninaenda nyumbani mara kwa mara, ahsante kwa kutufahamisha. nakubaliana na kata ya Irole ni sawa.
   
Loading...