Wenye vyombo vya usafiri nashindwaga kuwaelewa (naizungumzia ile mikwaruzo midogo)

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,320
50,538
Unakuta mtu anaendesha ka passo chake au tuseme vits au mkocho wowote afu bahati mbaya dereva mwenzake una mparua kidogo (kwa lugha ya barabaran wanaita kupigwa pasi).

Sasa kibinadam mnashindwaga nini kuelewana aidha kusameheana achen roho mbaya bhana mistake nyingi zinatokea nyingine unamsamehe mwenzako kwa kuwa Hakuna anayependa hilo la kuchubuana kutokea.

Ukipunguza roho ya kutamani kulipwa kila jambo Mungu wetu naye atakubariki eti.kama gari limekwaruzika kidogo unapotezea na hii ni kwa ajili ya upendo pia kwa ajili ya wengine maana utaondoa kero ya kuanza kudai pesa barabaran na utapunguza jam.

Nilipata bahati ya kuishi nje ya nchi kwa kweli mambo kama haya ya kuanza kubishana kutafuta chanzo cha motokaa kuguswa hayapo, sijui labda kwa sababu watu wako busy na mizunguko au labda wana hela lakini kiukweli ulaya huko watu tunagusana gari hata kama imepinda kidogo unaona Hakuna haja ya traffic kuitwa sijui apimishe huyooo unaondoka zako.

Nimeandika haya kwa masikitiko sana kutokana na leo kumchubua jamaa flani na ka noah chake mkwaruzo mdogo sana eti ananiambia nimpe laki na nusu.

Sasa kituko gari lake lenyewe ukiliona limebondeka body sio kidogo, pasi kibao na sura inaonyesha mpango wa kuinyosha hana ila mimi kumgusa kidogo sana na alteza yangu ikawa shida akaona aponee kwangu.. Sound nyingi nikamtoa 30000 mwishon ila kiukweli sio poa sometym tukikwaruzana Road tusamehane yaishe sisi sote binadam magari ni mavitu yetu tu
 
Mkuu kagombe sijui wamekuwa na roho gani Watanzania wenzangu
Roho nyeusiii hazijui maana ya msamaha
 
Aisee kwa pasi tu mm huwa nasepaga
Ashawahi jamaa kuivaa gari nyuma akachuna kidogo nikaona sio issue nikamwambia km vp jamaa sepa
 
Kama issue ni kusamehe iwe kwa magari yote.. sio wenye passo tu!!!

Btw pasi zingine ni za makusudi au uzembe.. usipomlipisha atazoea!!!

Asante tumefaham una ka-alteza... haka hakana tofauti na ist ya 2015
Mkuu ndio maana kunogesha bandiko sikutaka niweke za bei juu ungesema najipa promo, hata me najua alteza ni gari ya kawaida
Lingine ni kuwa Umesahau kugusia kuwa umeshajua kuwa nimekaa nje ya nchi
Usikariri ya humu ndani, dondoo nyingine achana nazo
 
Aisee kwa pasi tu mm huwa nasepaga
Ashawahi jamaa kuivaa gari nyuma akachuna kidogo nikaona sio issue nikamwambia km vp jamaa sepa
Nyie ndo watu original buana ebu kula 5 sio kama wengine sijui ni tamaa sijui ni kweli anakua na uchungu.. Mimi sijawah kupigwa pasi ila hata siku ukinipiga ntakupotezea
Sijui kwanini labda kwa kuwa na pesa nyinginyingi
Hahaha
 
Wenye bebiwoka huwa ni watata sana mtu kajichanga kakopa vikoba saccos upatu uwatu kibati kajichanga kanunua gari umpige pasi lazina aruke na wewe tuuu
 
Wenye bebiwoka huwa ni watata sana mtu kajichanga kakopa vikoba saccos upatu uwatu kibati kajichanga kanunua gari umpige pasi lazina aruke na wewe tuuu
Tena nafuu huyo aliyejichanga na kukopa, balaa ni wale masista duu wenye mabebiwoka ya kuhongwa na mijibaba sasa ole wako uwaguse kidogo tu aisee wanavyokuja juu utakoma mwenyewe....
 
Mkuu kwa uendeshaji wa DAR ukisamehe kila anaekupiga pasi hio gari itatazamika?? Au kazi yako iwe kusamehe na kuingia gharama za makosa ya wengine? Gari nyingi zina insurance lakini kulipishana ni kutiana adabu watu wawe responsible barabarani,sio papara za kijinga kutaka kujichomeka unakwangua gari ya watu.
 
  1. unamiliki alteza
  2. umekaa ulaya
  3. umeendesha gari ulaya
  4. una moyo wa kusamehe kupigwa pasi
ahsante mkuu
Tehe tehe ..mimi binafsi nimejiuliza hayo maswali mkuu. Angemalizia tu na kutaja Kabila lake!!! Daaah hawa jamaa hawaachi majigambo hata wasome na kupata PhD za hapa na pale.
 
Back
Top Bottom