Wenye uzoefu wa kupanda ndege naombeni msaada wenu

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
823
1,000
Habarini za usiku huu, poleni na majukumu.

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, nikiri mbele zenu sijawahi kuanda ndege hata siku moja. Nimepanga December hii kwenye sikukuu ya Christmas niende Mwanza kwa ndege.

Naombeni mchango wenu wa mawazo na uzoefu. Hotel gani ya bei poa pale Mwanza?

Gharama za ndege zipoje kwenda na kurudi, au kwenda pekee? Angani ntakaa muda gani?

Ratiba za kuondoka Dar kwenda Mwanza kwa ndege huwa ni saa ngapi? Ili safari yangu iwe nzuri, nini nizingatie? Changamoto gani ni ya kawaida kuvumilika?

Nimesikia ukifanya booking mapema bei inapungua, je kuna ukweli, na kama ndiyo, utaratibu wa booking upoje?

Karibuni
 
andreakalima

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
3,855
2,000
Habarini za usiku huu, poleni na majukum

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, nikili mbele zenu sijawai panda ndege ata siku moja

Nimepanga December hii kwenye sikukuu ya Christmas niende mwanza na ndege

Naombe mchango wenu wa mawazo na mzoefu

Hotel ya bei poa pale mwanza?
Gharama za ndege zipoke kwenda na kurudi, au kwenda pekee?

Angani ntakaa muda gani??

Ratiba za kuondoka dar kwenda mwanza kwa ndege uwa ni saa ngapi??

Ili safari yangu iwe nzuri nini nizingatie?

Changamoto gani ni ya kawaida kuvumilika??

Nimeskia ukifanya booking mapema bei inapungua, je Kuna ukweli, na kama ndio utaratibu wa booking upoje??

Karibuni
Kabila gani wewe? Tuanzie hapo
 
Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
11,088
2,000
Habarini za usiku huu,

Poleni na majukumu.

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, nikiri mbele zenu sijawahi kuanda ndege hata siku moja.

Nimepanga December hii kwenye sikukuu ya Christmas niende Mwanza kwa ndege.

Naombeni mchango wenu wa mawazo na uzoefu.

Hotel gani ya bei poa pale Mwanza?

Gharama za ndege zipoje kwenda na kurudi, au kwenda pekee?

Angani ntakaa muda gani?

Ratiba za kuondoka Dar kwenda Mwanza kwa ndege uwa ni saa ngapi?

Ili safari yangu iwe nzuri, nini nizingatie?

Changamoto gani ni ya kawaida kuvumilika?

Nimeskia ukifanya booking mapema bei inapungua, je kuna ukweli, na kama ndiyo, utaratibu wa booking upoje?

Karibuni
Umepanga kukaa hotelini kipindi chote??
 
Dickson mwaipopo

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
414
500
Habarini za usiku huu,

Poleni na majukumu.

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, nikiri mbele zenu sijawahi kuanda ndege hata siku moja.

Nimepanga December hii kwenye sikukuu ya Christmas niende Mwanza kwa ndege.

Naombeni mchango wenu wa mawazo na uzoefu.

Hotel gani ya bei poa pale Mwanza?

Gharama za ndege zipoje kwenda na kurudi, au kwenda pekee?

Angani ntakaa muda gani?

Ratiba za kuondoka Dar kwenda Mwanza kwa ndege uwa ni saa ngapi?

Ili safari yangu iwe nzuri, nini nizingatie?

Changamoto gani ni ya kawaida kuvumilika?

Nimeskia ukifanya booking mapema bei inapungua, je kuna ukweli, na kama ndiyo, utaratibu wa booking upoje?

Karibuni
Hotel Farms itakua bei poa kwako na itakufaa hata kwa Week mbili.
 
Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
3,347
2,000
Hivi hizi ndege za ATCL zote zinafanya kazi? Zinaenda mikoa gani maana Moro, Tanga na Pwani sizioni??
 
Zabron Hamis

Verified Member
Dec 19, 2016
1,960
2,000
Hivi hizi ndege za ATCL zote zinafanya kazi? Zinaenda mikoa gani maana Moro, Tanga na Pwani sizioni??
Mkuu, hii mikoa unakuwepo kwawakti mmoja? Au unapiga sinu kila siku kuulizia kama ndege zimefika au bado (hapa itakuwa unafanya kama meneja wa KIMBINYIKO/ABOOD/DAR LUX n.k
Wewe: halo!!
Agent moro: halo, boss za jioni
Wewe: njema, vp huko zimefika bus ngapi?
Agent moro: mpaka sasa zimefika tatu, moja iko njiani maeneo ya dodoma. Ilienda kuchukua abiria waliokuwa kwenye gari x baada ya (x) kupata hitilafu singida
Wewe: ok, hakikisha inafika salama, ngoja niwasiliane na mafundi singida ili nipate taarifa wamefikia wapi mpaka sasa
A/moro: sawa boss

Kisha unarudia na mikoa mingine mkuu, au sio.
 
king jafu

Senior Member
Sep 10, 2019
142
250
Habarini za usiku huu,

Poleni na majukumu.

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, nikiri mbele zenu sijawahi kuanda ndege hata siku moja.

Nimepanga December hii kwenye sikukuu ya Christmas niende Mwanza kwa ndege.

Naombeni mchango wenu wa mawazo na uzoefu.

Hotel gani ya bei poa pale Mwanza?

Gharama za ndege zipoje kwenda na kurudi, au kwenda pekee?

Angani ntakaa muda gani?

Ratiba za kuondoka Dar kwenda Mwanza kwa ndege uwa ni saa ngapi?

Ili safari yangu iwe nzuri, nini nizingatie?

Changamoto gani ni ya kawaida kuvumilika?

Nimeskia ukifanya booking mapema bei inapungua, je kuna ukweli, na kama ndiyo, utaratibu wa booking upoje?

Karibuni
Sasa siuwapigie customer service uangalie bei au kwenye tovuti Yao mkuu
 
Tempus Fugit

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
362
1,000
Ukikuta Airbus basi utatumia wastani wa saa moja na robo mpaka ufike Mwanza. Ukikuta bombardier utatumia zaidi ya muda huo.
 
ISO M.CodD

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
4,811
2,000
Ishu kubwa ni mizigo unayosafiri nayo.

Idadi, uzito na vitu unavyoweka ndani. Soma masharti kwenye tiketi yako.

Ukibeba mabegi mengi zaidi ya unayoruhusiwa, itabidi uyalipie. Gharama yake si ndogo. Vilevile usizidishe uzito wa mabegi yako la sivyo kila kilo iliyozidi utailipia.

Kama unaingia na begi ndani ya ndege hakikisha ndani yake hakuna chupa yoyote yenye kimikinika yenye ujazo wa zaidi ya 200mls kama sikosei mfano perfumes na body sprays, hakikisha hakuna vitu vyenye ncha kali kama nyembe, visu, mikasi, vichongeo . Hivyo viweke kwenye begi litakalosafiri kwenye 'buti'. Ukikosea hapo itakubidi uviache hivyo vitu hapo.

Ushauri wa maana zaidi ni kwa kuwa hujazoea zile security processes wahi airport 2 hrs kabla ya safari ujipe ample time to deal with anything that might arise
 
niah

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
6,559
2,000
Kama wewe msukuma wa Mwanza, kwanini uishi hotelini huna kwenu? Local flight inabidi uliport saa moja kabla ya flight au hata mbili. Huitaji visa wala passport labda kama huna kitambulisho cha taifa inabidi uwe nayo.
Sijui ATCL ila ndege nyingine huwa zinatoa vinywaji kama chai, juice na beer.

Laptop inabidi uibebe mkononi. Usibebe vitu vya ku explode.
 
Top Bottom