Wenye uwezo wa kutabiri; Kwanini Mzee Abdalah Bulembo hajagombea uongozi Jumuiya ya Wazazi?

Wanajamvi naomba wenye maono ya mbali mtusaidie , nini malengo ya Bulembo kuachia ngazi ya uwenyekiti jumuiya ya wazazi. Huyu mzee kuna kitu. Au mnasemaje ?
Ubunge una hela sana, mwenzio kaamua kujielekeza huko
 
Ccm inakwenda kuzaliwa upya kabisa ninavyosema upya ni upya kikweli kweli.mtandao unakwenda kukatwa.sasa hivi tunataka viongozi vijana wapya wenye uchungu.chadema wao mwenye chama wao hakubali kuachia chama kwa wanaharakat wakweli kama tundu lissu
Wewe ni wa ajabu sana!,Umeulizwa bulembo na ccm wewe unajibu ya chadema.............Hebu tuambie,"Je,Uchafuzi wa ccm,Magufuri alishindanishwa na nani kwenye ngazi ya uenyekiti?
 
Possibly anampango wa kurithi nafasi ya kinana maana kinana alikwishamaliza mda wake sema alilazimishwa kuendelea thus why hatumuoni font fed
 
Abdalah Bulembo, mzee mwenye kashfa kibao za wizi na utapeli, leo ndio mpambe mkuu wa JPM ama kweli kuwa uyaone, muendelee kuniombea.
 
Ccm inakwenda kuzaliwa upya kabisa ninavyosema upya ni upya kikweli kweli.mtandao unakwenda kukatwa.sasa hivi tunataka viongozi vijana wapya wenye uchungu.chadema wao mwenye chama wao hakubali kuachia chama kwa wanaharakat wakweli kama tundu lissu

vijana wenye uchungu wakina bashite wezi wa vyeti au wakina Gumbo wazee wakutoa rushwa kwa madiwani wajiuzulu
 
Alisema hagombei akaja kuchukua fomu baadae akakumbushwa na mkt "je umesahau turikubariana nafasi moja mtu mmoja?!" Hakurudisha fomu. Chezea magu wewe!
 
Naomba kuuliza hili swali, Kwani nimekuwa nikitafakari sana juu ya hili swala, pia juu kikao kinacho endelea Ikulu cha CCM.
Katiba ya ccm hairuhusu mtu awe mwenyekiti wa TAPA,wakati huo huo awe mbunge
Wote akina Msukuma watachagua ubunge au uenyekiti wa mkoa
 
Katiba ya ccm hairuhusu mtu awe mwenyekiti wa TAPA,wakati huo huo awe mbunge
Wote akina Msukuma watachagua ubunge au uenyekiti wa mkoa
Vipi kuhusu kuwa Mwenyeki wa chama na wakati huo huo ni Rais?? Hilo pia katiba iliangalie vizuri litaepusha huu mgongano wa majumu ya serikali na chama kufanyika wakati mmoja. Pia mwenyekiti itakua ngumu kupeleka mikutano ya chama Ikulu kwa sababu kule kutakua na Rais.
 
Hata angegombea au kuitetea nafasi ile asingeambulia za kutosha kwani bakishishi isingewezekana kuitoa! Kwa sasas anasubiria nafasi za huruma tu za kuteuliwa kwa kuandamana na mwenyekiti kila mahali na huenda akapewa ukinana ili aendelee kuwafitinisha wenzake kumfurahisha mtukufu sana!
 
Means hakushindanishwa?
Kwa mawazo yako jpm alishindanishwa na nani kuwania uenyekiti wa ccm?......Je,Kwa sasa (kwenye uchaguzi wa ndani wa ccm unaofanyika mwaka huu ,Ameshindanishwa na nani?......Kwa nini ccm imetweka kwenye katiba yake kuwa hakuna mtu kuchukua form ya kugombea urais 2020 kumpinga jpm ndani ya ccm?...hiyo ndo demokrasia?
 
Wana ccm tuliompatia Magu urais tujitafakari upya. Ni wakati sasa wa kuanzisha chama mbadala. Ccm hii haitavuka 2020.
 
Back
Top Bottom