Wenye uwezo Na nia ya kupata fursa sogeeni hapa

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,625
1,619
Habari wakuu.

Ni wiki chache zilizopita nilipata fursa ya kushiriki katika kazi ya kujitolea Na shirika Fulani ya kukusanya taarifa za wajasiriamali.

Nilitembelea baadhi ya mikoa, Na miongoni Mwa wajasiriamali walengwa ni wale wanaofuga kuku, wakulima wa mboga mboga, Na wavuvi wa samaki.

Hapa nitaegemea kwa wafugaji wa kuku Na mifugo mingine.
Wafugaji wa kuku Na mifugo mingine wanakabiliwa Na changamoto nyingi Sana, kubwa ni magonjwa ya mifugo.

Katika kudodosa, nikagundua kuna fursa imejificha, kwa uwezo wangu Na taaluma yangu siwezi kuitumia.

Fursa ni hii, Hawa wafugaji wanauhitaji mkubwa sana wa ushauri wa kitaalumu juu ya ufugaji Na magonjwa ya mifugo.

Sasa, kwa wale wenye uwezo Na wenye taaluma ya mifugo, fursa iliyopo ni kufungua maabara ya mifugo, maana maeneo mengi yenye wafugaji kwa Tanzania hayana hiyo huduma, pia waweza azisha ofisi yako Na ukatoa ushauri kwa wafugaji.

Kikubwa, ni kuanzisha maabara, katika hili nakuhakikishia utapata wateja wa kutosha, lakini lenga kwanza kwenye kutoa huduma Na sio kwenye kupata fedha kwa haraka.

Nawasilisha.....
 
sawa mkuu na asante kwa kuwaonesha njia bila shaka watakuja weny hiyo taaluma
 
Karibun SGD tunawangoja mfungue maabara. Kinachokwaza ni pale utakapokuta sample za kupima zinapelekwa halafu majibu yote yanafanana kama yale ya binadamu. Hapo ndio naiitaga science ya Tanzania ni arts in science yaani people wanasoma history ya biology, chemistry, agriculture and alike halafu wanapretend we are scientists
 
Back
Top Bottom