' Wenye Ukimwi Wawekewe Alama Kwenye ****** Yao' - Mbunge Swaziland | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

' Wenye Ukimwi Wawekewe Alama Kwenye ****** Yao' - Mbunge Swaziland

Discussion in 'JF Doctor' started by Pdidy, May 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,097
  Likes Received: 5,563
  Trophy Points: 280
  ' Wenye Ukimwi Wawekewe Alama Kwenye ****** Yao' - Mbunge Swaziland
  [​IMG]
  Mbunge wa Swaziland, Timothy Myeni amependekeza wenye ukimwi wabandikwe alama za kudumuTuesday, May 26, 2009 5:44 AM
  Mapendekezo ya kuwabandika alama kwenye ****** yao watu wenye ukimwi nchini Swaziland yaliyotolewa na mbunge mmoja nchini humo yamesababisha kasheshe kubwa sana kwenye nchi hiyo ambayo ipo kwenye janga kubwa sana la Ukimwi.Mbunge wa Lubilini nchini Swaziland, Timothy Myeni alipendekeza watu wote nchini humo walazimishwe kupimwa kama wameambukizwa virusi vya ukimwi na wale watakaogundulika wana ukimwi wawekewe alama za kudumu kwenye ****** yao.

  Bwana Myeni alisema kwamba hatua hiyo ingesaidia kusimamisha kuenea kwa maambukizo ya ugonjwa wa ukimwi kwa kupunguza mahusiano ya kimapenzi kati ya watu walioambukizwa na wale ambao hawajaambukizwa.

  Akizungumza katika mjadala wa wabunge wa kujadili njia za kuzuia kuenea kwa ukimwi, bwana Myeni alisema "Kabla ya kufanya mapenzi na mtu yoyote, mtu itabidi aangalie ****** ya mwenzake kabla hajaendelea ili ajue kama ni muathirika au la".

  Mapendekezo yake hayo yalizua mtafaruku mkubwa nchini humo huku waendesha kampeni za kuzasaidia watu wenye ukimwi wakipinga vikali mapendekezo hayo.

  Mmoja wa waendesha kampeni za kuwasaidia watu wenye ukimwi bi Siphiwe Hlophe alisema kwamba mapendekezo hayo yakipitishwa yatakuwa yanavunja haki za binadamu.

  "Inakuwaje pale mbunge anapopendekeza watu wenye ukimwi wawekewe alama?"

  "Hatuhitaji wabunge wenye mawazo kama yake kwasababu baadhi ya wapiga kura wake wanaweza wakawa wana ukimwi, sasa kwanini awabague?" alisema bi Hlophe.

  Hivi sasa kuna shinikizo kubwa kutoka makundi mbali mbali yanayomtaka Bwana Myeni ajiuzulu ubunge.

  Swaziland ndiyo nchi inayoongoza kwa idadi kubwa sana ya watu wenye ukimwi duniani.

  Asilimia 43 ya wananchi wa Swaziland inasemekana wanaishi na virusi vya ukimwi.
   
 2. Offish

  Offish Senior Member

  #2
  May 26, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huo ni unyanyapaa, kwa nini wale wasio na ukimwi ndio wawekewe alama kwenye *****zao?
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hayo ndo matokeo ya akili zenye tope
   
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Tatizo kubwa ni jinsi tunavyochagua au kupata viongozi. Huko Swaziland, wabunge wanapewa wadhifa huo kwa namna gani?
   
 5. M

  Motomukali New Member

  #5
  May 26, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli dunia imekwisha, kumbe hata mbunge anaweza kuwa kilaza!
   
Loading...