Wenye udhaifu huu ni mahodari kwa kuhonga kweli!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
Mwanaume anapohisi kuwa ni dhaifu katika kafanya mapenzi, yaani jogoo wake hawiki huwa anajitengenezea njia za kujitetea, ili kuonyesha kwamba yeye siyo dhaifu. Bila shaka hata wewe unayesoma hapa unaweza kuwa shahidi wa jambo hili.

Kwa mfano watu ambao wana kasoro za kimwili na ambao wanaamini kwamba kasoro hizo zimewapunguzia ukamilifu wao huwa ni wakorofi au wanakuwa na tabia zisizovutia.

Hiyo inatokana na juhudi zao za kutaka kuonyesha kwamba wao sio dhaifu.Wanaume ambao huwa wana udhaifu katika uwezo wa tendo la ndoa na wakautambua udhaifu huo, mara nyingi ni watu wenye kero kubwa sana kutokana na maumbile au malezi na mazingira.

Kwa kawaida mwanaume hujihisi kuwa kamili kama ana uwezo wa kutosha wa kushiriki tendo la ndoa. Kama uwezo huo ni mdogo kwake au hana kabisa ni lazima atajihisi kuwa na mapungufu makubwa.Mwanaume amezaliwa na kulelewa akiwa na imani kwamba uanaume wake hukamilishwa na uwezo wake wa katika tendo la ndoa.

Mwanaume anapohisi kwamba ana kasoro katika uwezo wake wa kushiriki tendo la ndoa, hujihisi unyonge, hiyo ni hatua ambayo hawezi kuipinga, kuna ambao wanajitenga kabisa na jambo hilo na huamua kutolishiriki, kama wameoa hushiriki na wake zao (kama wana uwezo kidogo) kama hawana kabisa uwezo wa kushiriki jambo hilo hawaoi.

Kama udhaifu huo umewakuta wakiwa ndani ya ndoa , mara nyingi ndoa huvurugika. Wale wasiokatishwa tamaa na hali zao huwa wanashiriki kwenye tendo hili bila kujali. Lakini kinachotokea ni kwamba, kwa sababu wao ni dhaifu na wanajua kwamba ni dhaifu, hujitahidi sana kutafuta kila njia ili wanawake wanaokutana nao wawalindie siri za udhaifu wao.Miongoni mwa njia wanazotumia ni pamoja na kuhonga fedha nyingi sana kwa wanawake hao.

Baadhi hufikia hata hatua za kuwajengea nyumba au kuwanunulia magari wanawake hao, ikiwa ni juhudi zao katika kutafuta kufichiwa siri. Inawezekana kabisa wao wenyewe wakawa hawajui ni kwa nini wanatoa fedha nyingi kwa wanawake hao bali hufanya hivyo kwa sababu hiyo.

Wao wenyewe wanaweza kuamini kwamba wanatoa fedha au kuwapa mali wanawake hao kwa sababu wanawapenda. Hii siyo kweli.
 
Duh halinihusu kwa sababu niko kamili na sijawahi honga kwanza
Napita tuu
 
ina ukweli pia hii koz tunasikia mtaani tu labda watakuja ambao wamekutana na dhahma hili
 
Wee mtambuzi kwanini mada zako nyingi ni armchair thinking halafu unazipresent kama ni vile absolute truth?
 
hii nikwelii,kunaa jamaa mmoja arusha...nafinyaaa jina kwapani,jamaaa ni muongajii mzuriii sana,na mwanamke asipite mbele yake jamaa lazimaa amchokoze au amtongozee,mwazoni tlikuwa tunajuaa dah!!jamaa mkare anapigaa mademu classic konomaaa,huwezi amini kumbe jamaa alikuwa awezi kurushaa majiii.yuko rathii kumpa mwanamkee chochote,kumpeleka sehemu yoyote ilaa mwishoni utaskiaa anazungaa anaudhuru analalaa mbele halii mzigo,wanawake wamemjuliaaa wanamchunajeee...kuna day alimleta mrembo tokaa dar akamlipia ticket ya ndege na kumlaza hotel maarufu arushaaa njiaa ya kwenda kijenge na jiro.mswisho wasiku night anajifanyaa kunaa zarururaaa..watoto wa mbwaa wakapitaa na demu.so watu kamaa hawaa wapo.
 
daah hao ndo wananifaa wanipm mambo ya kugaragazwa ya nini bwana? unakula maisha hamna kuzeeshwa kijinga
 
yaani hii ni kweli kabisa kisingizio kikubwa wanakuambiwa wamechoka kazi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom