Wenye silaha wavamia Gereza na kuwafungulia wafungwa 240 Nigeria

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Watu waliojihami kwa silaha nzito wamelivamia gereza moja katika jimbo la Kogi nchini Nigeria na kuwafungulia idadi kubwa ya wafungwa. Msemaji wa gereza la Kabba, Francis Enobore amesema kuwa gereza hilo lilivamiwa usiku wa manane na watu wenye silaha ambao bado hawajajulikana na kuwaachia huru wafungwa 240.

Akielezea mkasa huo amesema washambuliaji kadhaa walishiriki katika mapambano ya kufyatuliana risasi na walinzi wenye silaha wa gereza hilo ingawa haijaweza kufahamika kundi lilohusika na kitendo hicho. Gereza hilo lililoanza kutumika mwaka 2008 na lina uwezo wa kuchukua wafungwa 200.

Matukio ya kuvunjwa kwa magereza makubwa ni ya kawaida nchini Nigeria. Katika shambulizi la Aprili 5, watu wenye silaha walivamia makao makuu ya polisi ya Owerri na kuwaachia huru zaidi ya mahabusu 1,800.
 
Hizo ndio nchi zenye heshima no uonevu wa kipumbavu pumbavu kisha maneno ya dharau kwa wananchi kuna wakati hadi Jiwe alisema Polisi msiwafanye Watanzania ni Wajinga kwa kwasikilizisha ujinga wenu
 
Back
Top Bottom