Wenye nyumba wanamtaka kiongozi wao, jirani inawauma nini?

Kama ambavyo magufuli anawafanya hamna hata wa kumhoji tangu lini gekul na kalanga wakawa na nguvu kushinda nyie watetezi wa chama wa muda mrefu? Wanachukua ubunge kwa ubua sana nyie mnabak macho tu si umemuona katambi na machali
Hata Mbowe akija tutamuachia ubunge wake!
 
Chadema hampo tofauti na sie tunaotaka Magufuli aongoze angalau kwa miaka 20,ili tunyooke vizuri
Wekeni akiba ya maneno,demokrasia inaanzia nyumbani kweli kama mlivyosema
Labda huelewi kuwa Mbowe anaongoza wanachadema tu na Magufuli anaongoza wanaCCM na wanaCDM na wengine wote! Kwa hiyo unaposema 'sie' inamaana unawasemea na wanaCdm pia. Kitu ambacho sio sawa.
 
Kama mitizamo ndio hii, basi hakuna haja ya vyama vya upinzani kuendelea kupiga ngonjera za kutaka kuitoa CCM madarakani. Acha CCM "iendelee kuongoza tu maana wananchi ndo wanaiweka" Charity must begins at home. Kutokuwa na ukomo wa uongozi kwenye katiba ya CHADEMA na vyama vingine vyote vya siasa ni aina flani ya ufisadi, ulafi na unkurunzinza.
Tatizo mheshimiwa Consultant hutendei haki jina unalojiita. Hivi waweza kusema ni wapi katika katiba ya Chadema Mbowe amevunja kugombea uongozi tena? Angeweza kuachia madaraka pamoja na kuwa katiba haimzuii, lakini wanachama wanataka aendelee kwani mpnzani wao mkubwa CCM anataka aondoke na anatumia propaganda na mbinu za kishenzi kumkomoa kiuchumi. Kwanini wanataka aaondoke? Ndio na wao wanasema haondoki.
Hayo ya CCM hakuna anaye ngilia lakini ya Kitaifa tunataka Katiba na sheria zifuatwe. Hivi nani aliwahi kuhoji au kulalamika jinsi Mwenyekiti wa CCM anavyopatikana? hayo yao wenyewe na ya wengine hayawahusu
 
Katiba ya Chadema ilikua ni miaka mwisho kabisa miaka 10 lakini kipindi cha Mbowe kilipokaribia kuisha Mbowe na Genge lake wakabadili katiba. Sio Wote ndani ya Chama waliopenda katiba iweke misingi ya Kidikteta kwenye Chama kinachopigania Demokrasia. Dhambi ya Mbowe kubadili katiba ili aongoze Daima itakigharimu Chama sana . Tena wakati huo serikali iliyokuwa madarakani na Chama chake hawakua na muda wa kuwafuatafuata wapinzani ili warudi CCM lakini bado Mbowe alijidai kuwa yeye ni kiboko ya CCM yeye peke yake.

Nawashangaa watu kama akina Kubenea na Komu wenye Fikra pevu kuendelea kubaki gerezani ndani ya Chadema wakati Rais wa Nchi na amirijeshi mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ameshawaita wapinzani wote wanaosumbuka na kulemewa na mizigo waende wakapumzike kwenye Chama cha mapinduzi na serikali yake.
Muda waliopewa ni sawa na askari magereza kuacha mlango wazi,wafungwa wenye akili watatoroka na kwenda sehemu salama.

Hasa Kubenea usipoteze Muda ndani ya Chadema ,hicho ni Chama cha mtu ninafsi kwa manufaa yake na wale anaowataka.

KADA WA CCM.jpeg
 
Chadema hampo tofauti na sie tunaotaka Magufuli aongoze angalau kwa miaka 20,ili tunyooke vizuri
Wekeni akiba ya maneno,demokrasia inaanzia nyumbani kweli kama mlivyosema
Muwekeni kwenye chama chenu, uzuri wake katiba yenu pia inaruhusu.
 
Hata CCM mwenyekiti wetu hataki kuendelea kuwa mwenyekiti sema sisi wanachama ndio tunataka aendelee kuongoza angalau hata miaka 50. Yaani itaniuma sana aliondoka baada ya miaka kumi tu. Sema tukifanya hivyo tutakuwa tunakiuka katiba ya chama. Na demokrasia tutakuwa tumeivunja kwa makusudically.
Umesahau jina na namba ya simu
 
Audio inasema BONI ndiye anayempa uhalali Mbowe wewe unakuja na story za Mbu wa Kijani
 
Tatizo mheshimiwa Consultant lakini wanachama wanataka aendelee kwani mpnzani wao mkubwa CCM anataka aondoke.
Nadhani hapa ndo tatizo lilipo kwenye hivi vyama vyetu. Lipumba na John Momose Cheyo wamekuwa wenyeviti wa vyama vyao tangu mid 90's (miaka ambayo baadhi ya watu humu ndani walikuwa hawajazaliwa bado) na eti "wanachama wanawataka waendelee". Kuna tatizo mahali flani.
 
Muwekeni kwenye chama chenu, uzuri wake katiba yenu pia inaruhusu.
Kwa nini wasiweke kwenye katiba ya Nchi wakati watanzania ndio watakaomlazimisha ondoa kifungu cha ukomo wa rais kuwa madarakani kwenye katiba na Chama chake kina wingi wa kura za kuipitisha.
Suala ni kuwa hatutaki ajipe mamlaka hayo peke yake bali bunge muhimili halali.

Hapo ndipo Mbowe atakapogundua umuhimu wa kuheshimu katiba hasa kwenye nafasi ya uongozi. Hakuna mtu mmoja anayeweza kujenga Chama.
Hata Mwalimu alipewa Kuongoza Chama sio kwa sababu alikua ndiye kibako ya wakoloni la hasha ni kwa sababu alikua na elimu kubwa kubwa kwa wakati huo ukilinganisha na wapambanaji wenzake. Lakini kuna watu walianza kupambana tangu mwaka 1922 wakati anazaliwa.

Mbowe alitakiwa afuate mkondo wa wapigania Uhuru wetu ambao walimkabidhi Mwalimu Chama kutokana na Elimu yake na sio fedha kama leo Wanachadema wengi wanaofikiri kuwa fedha za Mbowe ndizo za muhimu katika kuongoza Chama na kujenga itikadi ya nguvu ya umma bila kujali uwezo wake kielimu. Chama sio kuongoza kwa ujeuri tu Bali ni maarifa na kujua falisafa na mbinu mbalbali za kukabiliana na wapinzani wake ambao kimsimgi wanaelimu kubwa kuliko yeye.
Mfano kupambana na safu ya uongozi wa sasa wa CCM ni kazi ngumu Sana kwa Mbowe zaidi ya kubaki akitukana na kujisifu huku akiwalazimisha wabunge wake wasishirikiane na serikali bila kuwaambia mipaka ya ushirikiano iwe ni ipi , matokeo yake wanajikuta wakipinga mpaka maendeleo ya majimbo yao kwa kufuata maelekezo ya kiongozi asiye na maarifa.
 
Tumeshuhudia CCM na washabiki wake wakitumia nguvu kubwa kutaka Mbowe aondolewe kuiongoza Chadema wakisema amechokwa na anatumia hila kuendelea kuwepo madarakani.
Sasa wenye chama wamejibu kuwa wao ndio wanataka aendelee ili malengo ya chama yatimie. CCM kamwe haiwezi kuichagulia Chadema Jenerali wa kuongoza mapambano, maana wanataka wampate mpinzani wa category ya Mrema.View attachment 902926

Acha uzwazwa wewe....mbona mnasifia wazungu wanapompinga Kagame ama Museveni??.....watu wa nje wanaweza kuona tatizo ambalo nyinyi mliokua ndani hamlioni
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom