Wenye nyumba kudai kodi ya mwaka mzima ni sahihi wakati mishahara inalipwa kwa mwezi?

AMEDEUS

New Member
Dec 16, 2010
4
0
Je wenye nyumba kudai kodi ya mwaka mzima ni sahihi? nini kifanyike kuondokana na tatizo?
 
Huo ndo ubepari, usahihi au kutokuwa sahihi doesn't matter hapa, cha muhimu maslahi ya mwenye nyumba aliyewekeza mtaji wake, period.
 
Je wenye nyumba kudai kodi ya mwaka mzima ni sahihi? nini kifanyike kuondokana na tatizo?

Mkuu post yako imenifanya nijiulize maswali mengi mno, Nahisi kodi yako imefika ukingoni thats why umeandika hivyo.
Mkuu watu wote si wafanya kazi, hiyo ni moja.
Pili hiyo ni biashara kama zingine na wenyewe wanaanalia maslai yao, na kawaida ya biashara haiangalii source yako ya income
 
Je wenye nyumba kudai kodi ya mwaka mzima ni sahihi? nini kifanyike kuondokana na tatizo?

Kuingia kwa wawekezaji nchi ndiko kulichangia kwa % kubwa sheria ya makazi kufutwa kwani miaka ya nyuma hiyo sheria ilikuwepo kuwa mpangaji anapaswa lipa kodi ya nyumba kwa miezi isiyozidi miwili sasa wenye nyumba wanadai watakavyo hutaki sepa basi sasa hapo haki ya Raia kuishi ndani ya nchi yao inakuwa ya kunyanyasana kwa kuwa wewe mwenye mali umewahi kujenga basi ndio unajiamlia kufanya sasa hapo kweli inawawia vigumu hata raia wengine wenye kipato cha chini kulipa kodi ya miezi sita,

Ila Jana Bonge wa Clouds FM alikutana na mtendaji mmoja wa Taasisi ya watu wanao tetea wapangani ja wanao wapangisha wakasema chama hicho kipo ila sheria ndio hazikidhi bado mahitaji ya wadai na wadaiwa

 
Hapa Tanzania kila mtu anafanya anavyotaka,kwani hatuoni ajabu wakati pesa halali inayotakiwa ifanywe kwenye mauzo na malipo hapa Tanzania ni Shilingi ya Tanzania lakini bila aibu kila kitu kuanzia kuuza vifaa vya elektroniki hadi upangishwaji wa nyumba hufanywa kwa pesa ya Marekani yaani Dola,utadhani hapa nchini hakuna vyombo vinavyosimamia mambo ya pesa?Tanzania ni Banana Republic FULL STOP
 
Hapounapoisi mkuu nahisi mwenye house amekubadilikia sasa anahitaji kodi ya mwaka! Pambana umlipe sivyo asije kukupa NOTICE
 
ni sahihi kabisa, wanatakiwa kuendelea kufanya hivyo ili akili yako ichangamke, upige mishemishe zaidi usiku na mchana ili ujenge yako. wasipofanya hivyo utajisahau...nampongeza huyo mwenye nyumba wako, anakupenda anataka upate akili ya kujenga yako...Mungu akusaidie.
 
wengine wanatambia nyumba za urithi tu na kuwa wasumbufu kuliko wazazi wao waliojibana katika kujenga, pumbaffuuu zao
 
Ndio maana mie nimejenga ya kwangu... Na hili ndilo suluhisho kwa wote
 
Nashauri tuunde chama cha wapangaji Tanzania (CWT) ambacho kitashughulikia haki zetu. Wenye nyumba wanatufanya tushikwe kiwewe kodi ikiisha. Unakuta mzee wa nyumba unaangaishwa kupata 3.6m kulipa pango kwa mpigo.
 
Hii ya kulipa kwa mwaka ni uonevu kwa wapangaji wanaotegemea kamshahara... ila inauma kutoa 3.6 million kama pango halafu nyumba si yako.Dah bora ninunue kiwanja nijenge kuliko kutupa hizo 3.6 million...
 
Mkuu post yako imenifanya nijiulize maswali mengi mno, Nahisi kodi yako imefika ukingoni thats why umeandika hivyo.
Mkuu watu wote si wafanya kazi, hiyo ni moja.
Pili hiyo ni biashara kama zingine na wenyewe wanaanalia maslai yao, na kawaida ya biashara haiangalii source yako ya income

Mkuu Paulss, huo ndo ubinafsi wa binadam...je unasemaje kuhusu biashara ya fuel kuwekewa uangalizi na EWURA? je hiyo si biashara kama zingine?..
 
Je wenye nyumba kudai kodi ya mwaka mzima ni sahihi? nini kifanyike kuondokana na tatizo?

Pole sana Amedeus (Sijui kama una uhusiano na Askofu Msarikie)

Si haki kulipa kodi kwa Mwaka - Ni utapeli! ::

Kuna mswaada wa sheria unaandaliwa ku-amend/kuipa nguvu sheria ya "upangaji" ambapo, kwanza itabidi kila mpangishaji alipe kodi serikalini kama biashara zingine, pili kiwango cha kodi kulipa in advance kisizidi miezi mitatu...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom