Wenye nyumba kuanza kulipa kodi msaada kwa mlala hoi au ndio kuongeza machungu??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenye nyumba kuanza kulipa kodi msaada kwa mlala hoi au ndio kuongeza machungu???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanaharakatihuru, Mar 23, 2012.

 1. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wandugu tumeona wabunge wanaojiita vijana wameaamua kabisa kuwauumiza vijana wenzao wasio kuwa na ajira kwa kile wanachokiona kuwa eti ni kuongeza mapato ya serikali ili hali sekta ya madini na tax heaven zinashamiri. Huu ni mtazamo binafsi na usio na mapenzi mema kwa mwananchi wa kawaida mwenye nyumba hana shida, ukimkata kodi kodi atakae lipa ni mpangaji, kumbuka huyu ndio yule yule analipa pay as you earn, na kulipa 18% ya TRA kwenye kila manunuzi yake ya kila siku, umeme ndio huo juu, maji hakuna lakini bili pale pale, hivi kweli wewe makamba ni unatafuta umaarufu au unataka nini wewe unajua bei za nyumba mijini au unakaa kwenye lile ghorofa la dada yako acheni bana labda muongeze kodi kwenye magorofa ya mahotel ya kifahari kuanzia mbuga za wanyama na mijini kote. Eti wewe nani hii hivli lile ghirofa ulilo kodisha NMB unalipa kodi acheni bana.

  Vijana msitafute umaarufu kwa kukurupuka, tafakarini aftermath ya huo *****, leo hii TRA wanakuja na kudai kodi kwa watu wenye vibanda vya chips katika bar na sehemu nyingine kuongeza mapato acheni hiyo bwana, baneni matumizi ya serikali na wawajibisheni mafisadi, makampuni yaweke fedha kwenye bank za ndani yale ya madini, na mengineyo hapo tu. ondoeni misemo rais ya kuvutia wawekezaji wao hawaji huku kwa kuwavutia nyinyi unafikiri siku sisi tukiingia mtaani watakaa humu jifunze kutoka mali.

  Nipo tayari kufa kwa kupinga huu mswada, hakika enough is enough, hata kama mtaanza kutembea na SMG kama wenzenu (malima) tutapambana tu.

  Mungu ibariki Tanzania

  Mungu ibariki Afrika

  Mungu laani mafisadi na uzao wao

  Mungu adhibu mamluki wote viongozi
   
 2. Rabin

  Rabin Senior Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mimi naona inawezekana kama kutakuwa na muongozo wa kodi za nyumba kulingana na thamani ya nyumba. Ikiwa serikali itatoa muongozo wa kodi kuliko ilvyo sasa kila mwenye nyumba anapanga mwenyewe nadhani inawezekana na hasa kama serikali itakuwa na dhamira ya dhati.
   
 3. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 4. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Je hii serikali yetu wewe ni mgeni nayo, au ndio wanataka waongezi mapato kwa ajili ya posho
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Aisee sirikali itachemka kuanza kukusanya kodi huku kwenye nyumba na vibanda vya chips,kwanin wasijikite kwenye madini ambayo yanaweza kuendesha nchi bila kutembeza bakuli?
   
 6. Rabin

  Rabin Senior Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nimesema kwa serikali yenye dhamira ya dhati kabisa inawezekana na italeta unafuu kwa walalahoi lakini kama ni mipango itakayowanufaisha wao hakuna haja ya kuwa na kodi hiyo, kwa sababu kuna vyanzo vingi vikubwa havija fanikiwa
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wanatumia masabauri kufikiri..hivi kuna mtu anajua ni madini /mafuta / gesi kiasi gani yanapelekwa nje ya nchi kwa say, a month? kuna mamlaka yoyote inayojali kuchukua takwimu hizi na kuhakikisha thamani yake na kama kodi zinalipwa ipasavyo? what is the point of ewekezaji while you can't do accounting of what is solely and rightfully yours..nchi ya kibwege sana hii.
   
 8. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii revenue wanayodhani wataongeza itamsaidia nini huyu mlipaji, maana mapato ya Tanzania yanaishia kuibiwa na Viongozi na kupeleka fedha hizo kwenye mabank ya nje! zoezi hili halina faida yoyote kwa Mtanzania ni kuongeza maumivu tu kwa wanyonge! We currently don't have committed goverment!
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni wazo la mtu mmoja au Wbunge wote?
   
 10. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  huyu makamba inabidi ajifunze undani wa kodi.
  Kama anaona kulipa kodi ambayo itaongeza kodi ya nyumba kwa wananchi ni big source of revenue basi anapendekeze pia wenye shule kulipa kodi kwa kila mwanafunzi anaingia shuleni.

  Kuna shule nyingi sana tanzania na wanafunzi ni wengi sana basi serikali ianzishe kodi ya wanafunzi. It will be very big source of income kwa sababu wanafunzi ni wengi sana(kuanzia vidudu mpaka vyuo vikuu)
   
 11. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,122
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kulipa kodi kwa kila biashara halali bila kujali udogo au ukubwa wake ni wajibu wa kila mwananchi. Tatizo linaloikabili serikali yetu ni ubovu wa matumizi ya kodi, jambo ambalo linamfanya mwananchi aone kulipa kodi ni sawa na kuibiwa au kutapeliwa. Lakini ukweli ni kwamba, serikali makini yenye mipango thabiti na ya KWELI inahitaji kodi kwa maendeleo ya nchi.
   
 12. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yuko na wenzake wenye huo mtazamo
   
 13. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  umenena vyema kaka, lakini je Kodi ni kwa mlalahoi tu mbona mlalahoi hagusi taratibu utaanza kusikia tunarudisha kodi ya kichwa ili kuongeze mapato. lazima serikali ifike mahali ituhakikishie hizi hela tunazolipa zinatumikaji sio lipa kodi kwa maendeleo yako wakati bado maisha yako vile vile.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ndugu,

  Kama una kibanda chako ulikuwa hulipi kodi sasa unatafuta sympathy za watanzania umenoa. I support this bill tena imechelewa kuja. Wenye nyumba kwa muda mrefu walikuwa wanakwepa kulipa kodi na kupandisha ada za pango kiholela ili wawe matajiri. Ukiwa unadai kijana atasuffer mie sidhani kwani hao wenye nyumba wakiona bei zao zimepanda sana na hakuna wateja watashusha wenyewe. Mfano mzuri kariakoo sasa hivi juzi juzi nimeshuhudia kodi ya nyumba zikishuka hadi laki tano mpaka laki nne wakati mwaka mmoja kabla kodi ya nyumba ilikuwa imeshuka sana milioni moja na nusu.

  Binafsi nawapongeza sana kina Zitto na January for this bill itasaidia kutupunguzia mzigo sie wafanyakazi wa kodi . Tumekuwa tukikamuliwa sana mzigo wa kodi na serikali. Kuhusu matumizi ya fedha za kodi hilo nakuunga mkono but iende pamoja na huu muswada.

  Wenye nyumba Dar , Arusha, Mwanza mlikuwa mkikamua na kujitajirisha sana kwa muda mrefu. It is time now MLIPE KODI !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 15. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaani sema huku ndio hivyo hatufahamiani majina, ila mtu kama wewe unatakiwa kupigwa mawe hadharani halafu inavyoonekana hujui kulipa kodi unaishi kwenye nyumba ya urithi??? Yaani unaishi kwa assumption kariakoo bei imeshuka eti na huko kwingine itashuka hivi kweli huna akili nzuri wewe Mtanzania???? Hivi unajua adha ya sisi tunaopanga inavyokuwa kua?? Kama wewe ndio mnaoishi kwa kusifia sio wote......Kumbuka kila mtanzania analipa kodi fisadi mwana wa mafisadi zaliwa wa ufisadi weeeeeeeee
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Narudia tena,

  Kama ulikuwa hutaki kulipa kodi ndio ukome mwisho wako umefika. Wenyenyumba Tanzania mlikuwa mnakimbia sana kulipa kodi Tanzania. Matokeo yake mmekuwa mkitajirika na sisi wafanyakazi tukiishia kuwaendeshea serikali yenu. Sasa mlipe kodi tena kwa taarifa yako mie nakaa uswahilini tena nyumba ya kupanga but I feel no sympathy kwa hawa wenye nyumba. Wapigwe kodi hebu tuondoshee upuuzi hawa nina hasira sana nyie.

  Tena ombi kwa serikali mkianzisha kodi hiyo tunawaomba wafanyakazi mtupunguzie kodi ya PAYE ili tuwe na nafuu maana mzigo tunaobeba wafanyakazi Tanzania unatisha. Na bado kuna vile vile sekta zisizo rasmi za kujiajiri nazo ziwekewe mikakati ya kulipa kodi watu wafahamu uchungu wa hela zao na kuwa makini wanapochagua nani anawaongoza. PIGA KODI HAO WALIKUWA WAKIJITAJIRISHA TU HUKU HAWALIPI KODI.
   
 17. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,122
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
   
 19. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kuna mambo mawili, ulipaji wa kodi ya nyumba kwa TRA kisheria unapaswa ulipwe na mpangaji (withholding tax), kimsingi mwenye nyumba atakuambia anataka laki 1 km unataka kulipa kodi basi inabidi iwe laki na kumi hiyo kumi utaizuia na kuilipa TRA.
  Pili kuna ugumu katika kudhibiti bei ya pango kwa sababu supply ya nyumba ni ndogo kwa vile NHC wanajenga kwa kasi ndogo sana nyumba mpya. Kumbuka kodi ikiwa ndogo sana hata wawekezaji wadogo wataacha kujenga nyumba kama biashara hailipi na kuongeza tatizo la nyumba kama hazitaendelea kujengwa.
  Tatizo la kodi kubwa na kudaiwa kwa mwaka litapunguzwa kwa kuwepo nyumba nyingi zinazotafuta wapangaji km ilivyo nchi nyingine.
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Na wewe unatumia nini kufikiri hivi unajua gharama za kuwekeza katika kuchimba hayo madini, mafuta hadi yakapatikana?
   
Loading...