Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Nimeangalia video za mtoto Charles Mbena, Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kujalia maarifa ya ziada. Mtoto wa miaka sita kumudu hesabu za kutoa na kujumlisha kwa kiwango cha Charles ni kusema Jina na Mungu lihimidiee.
Kuna taasisi zilizojitokeza kumsaidia Charles, nimemuona mpaka RAS amefika shuleni kwa Charles. Katika misaada yote sijaona msaada unaojumlisha wazazi wa Charles. Charles ni mtoto wa miaka sita, anahitaji upendo na malezi ya wazazi wake waliomlea mpaka leo anaonekana alivyo.
Kumpeleka shule ya boda au kumtenga na wazazi wake ni kumnyima mapenzi ya wazazi anayostahili. Ikiwezekana, baba wa Charles arafutiwe ajira karibu na shule atakayosoma mtoto wake na jamii iendelee kuisaidia familia ili iweze kulea watoto wao akiwemo Charles.