Uchaguzi 2020 Wenye nguvu tuandike tusije laumu baadae hatukutimiza wajibu wetu

Peter Dafi

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
388
271
Na. Egla Mamoto

Wakati Serikali Ya Awamu ya Tano Ya Rais Dr.John Pombe Joseph Magufuli ikilaumiwa na Baadhi ya wapotoshaji eti imejikita katika ujenzi wa Uchumi wa Vitu Badala ya Uchumi wa watu, napenda kuifahamisha Jamii kuwa "Serikali inapojenga UCHUMI WA VITU ni wakati huo huo ndipo inajenga UCHUMI WA WATU."

Leo nimeamua kushika kalamu yangu baada ya kuona wapinzani wanatufanya watanzania wapumbavu hatuna akili, vipofu, hatuoni lakini wanataka hata kutuziba maskio tusisikie ukweli unaosemwa.

Watanzania wenzangu uchumi ni dhana inayoelezea masuala ya uzalishaji, usambazaji, biashara kwa ujumla na matumizi ya bidhaa, pamoja na huduma, yote kwa pamoja yakiwa yanafanywa na wadau mbalimbali.

Dhana juu ya UCHUMI WA WATU NA UCHUMI WA VITU ni dhana inayojaribu kujadili juu ya uchumi mkubwa ambao kwa lugha rahisi ndiyo uchumi wa vitu (macro economy) na uchumi mdogo ambao kwa lugha rahisi pia ndiyo uchumi wa watu (micro economy) na kwa mujibu wa kanuni za kiuchumi, serikali ndiyo yenye jukumu la kuwekeza katika kujenga uchumi mkubwa (macro economy) ambao ndiyo uchumi wa vitu.

Tazama miundombinu iliyojengwa na Serikali ya Awamu ya Tano (ambayo ndiyo inasemwa kuwa ni uchumi wa vitu). Yote itaishia kutatua shida za mtu mmoja mmoja (yaani kujenga uchumi wa watu) kama ilivyoainishwa hapo chini.

1. MIUNDOMBINU YA USAFIRI NA USAFIRISHAJI
hapa tunazungumzia barabara, madaraja, reli, viwanja vya ndege, ununuzi wa ndege, meli na vivuko;
  • Yote haya yatarahisisha na kushusha gharama za usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo,
  • Itarahisisha wananchi kufanya biashara za kusafirisha bidhaa na huduma mbalimbali
  • Inasaidia kupendezesha miji
  • Itaongeza ajira kwa wananchi katika sekta ya usafirishaji
  • Itarahisisha uanzishwaji wa viwanda kwa kurahisisha usafirishaji wa vifaa vya ujenzi, nguvu kazi (watumishi), malighafi, pamoja na bidhaa zilizozalishwa na viwanda husika,
  • Inahamasisha biashara ya utalii wa ndani na wa kimataifa
  • Itarahisisha utoaji huduma nyingine kwa mfano kilimo, afya na elimu.
2. MIUNDOMBINU YA AFYA (Hospitali, Vituo Vya Afya, Zahanati na Vifaa Tiba)
Sote ni mashahidi namna serikali ilivyopambana kuhakikisha ndani ya miaka mitano 2015-2020 imejenga na kuboresha miundombinu katika sekta ya afya na matokeo ya hayo yote ni:
  • Kuongezeka kwa Ajira kwa wananchi waliyo na ujuzi katika kada za afya na wengineo
  • Imesaidia kupatikana kwa huduma za afya katika maeneo ya karibu
  • Kuimarika kwa nguvu kazi ya Taifa kutokana na wananchi kuwa na uhakika wa afya bora.
3. MIUNDOMBINU YA UMEME
  • Imerahisisha huduma nyingine mfano afya, elimu na mengineyo mengi,
  • Inarahisisha ukuaji wa uchumi wa viwanda,
  • Inaimarisha ukuaji wa miji na vijiji pia kusaidia matumizi ya majumbani.
4. MIUNDOMBINU YA ELIMU (Ujenzi wa shule, Vifaa Kujifunzia na Kufundishia, Elimu Bure)
Hili limegusa jamii moja kwa moja kwa sababu
  • Imezalisha wasomi wapya,
  • Imeimarisha mfumo wa elimu,
  • Imeongeza idadi ya wahitimu wa elimu ya msingi na sekondari,
  • Imeongeza kiwango cha ufahamu katika jamii,
  • itaongeza wataalam wengi ambao ni wazawa.
Ndugu zangu Watanzania yote hayo na mengine mengi yaliyofanyika chini ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kipindi cha miaka mitano yanajibu kwa ushahidi dhana hii ya uchumi wa vitu dhidi ya watu. Naomba Watanzania Tumchague tena Dkt. John Pombe Magufuli kwa sababu chakula ametafuta, amepika, amepakua na sasa kazi iliyopo ni kula neema za kazi kubwa aliyoifanya Dkt. Magufuli kwa miaka mitano.

Kwa leo wino umeishia hapo.
 
Dafi SINIC GERANKE MANUMOOK OHE........ Manda ahayarane I arir wa koman
 
1602508024728.png

Unapomlaumu Rais anaemaliza muda wake na kuweka ahadi zako, ilhali anaemaliza muda ni wewe mwenyewe.
 
Unayefaidika na kipato haramu awamu hii utaachaje kujitoa ufahamu namna hii? Acha wanaoumia kiukweli kwa ugumu wa maisha uluosababishwa na awamu hii wafanye yanayowapasa.
 
View attachment 1597960
Unapomlaumu Rais anaemaliza muda wake na kuweka ahadi zako, ilhali anaemaliza muda ni wewe mwenyewe.
Ndo kaliona hilo leo ..... Angetoa hizo m.50 kila kijiji zimetengeneza ajira pia , sema ajira kazipeleka kwa watu na nchi zao kutengeneza ndege, na wana leta vitu vyao kwenye ujenzi wa miradi yote hiyo mikubwa anayo tusimangia kama kwamba tz ndo ya kwanza kuwa navyo.
 
Ndo kaliona hilo leo ..... Angetoa hizo m.50 kila kijiji zimetengeneza ajira pia , sema ajira kazipeleka kwa watu na nchi zao kutengeneza ndege, na wana leta vitu vyao kwenye ujenzi wa miradi yote hiyo mikubwa anayo tusimangia kama kwamba tz ndo ya kwanza kuwa navyo.
Hata kuweka utaratibu mzuri wa kodi
Kusingewakimbiza wafanyabiashara wakubwa waliohamishia biashara zao Zambia, Malawi ect kukwepa kodi mkomoeni. Na ajira wakahama nazo.
 
Ata wale walio kua wana piga kelele za jamaa aongezewe mda nazani wana jificha kwa aibu
Hao walikuwa wanapigania matumbo yao yashibe,hivyo hawawezi kuona aibu kwa ni watu wabinafsi,wanahitaji kufahamu yakwak pekeyao.Hawa huwa yawengine hayawahusu wao.
 
The point is that, Meko fool lacks the mental capacity to serve this country as a local government chairman, sorry I mean a president.
 
Back
Top Bottom