Elections 2010 Wenye nchi wamshtaki Jeetu Patel and Sumaye kwa JK!

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,059
4,055
Wananchi wa vijiji vya Mvumi na Mvomero mkoani Morogoro, wamewashitaki mfanyabiashara Jeetu Patel na Waziri Mkuu wa Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye kwa mkuu wa nchi, kwa kujimilikisha ndefu (kubwa) bila kuiendeleza na kutaka wanyang’anywe.

Wenye nchi hao walieleza masikitiko yao kwa JK wakati aliposimama kuwasalimia akiwa katika kampeni ya kuomba kura ili achaguliwe tena kuiongoza Bongo kwa mara nyingine.

Akiwa njiani kutoka Kilosa alikohutubia mkutano mkubwa wa kampeni, mgombea huyo wa CCM alisimama katika Kijiji cha Mvumi, ambako moja ya kero alizokumbana nazo ni ya Jeetu kuhodhi mashamba makubwa matatu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Jeetu ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini, anamiliki mashamba hayo na hayamudu katika uwekezaji wake, na zaidi anayakodisha kwa wananchi kwa Sh 50,000.

“Jeetu Patel, amehodhi mashamba bila ya kuyamudu na anatoza shilingi elfu hamsini kwa ajili ya kulima. Suala hili limepelekwa kwa uongozi wa Wilaya na Mkoa, lakini hakuna utatuzi,” alisema na kushangiliwa na wananchi wenzake.

Akijibu hoja ya suala la Jeetu Patel, JK alisema, “niacheni nihangaike nalo, halikuwahi kufika kwangu, ndio kwanza nalisikia kwenu, lakini hakuna lisilowezekana. Niachieni nitafute ukweli wake.”

Akiwa Kijiji cha Mvomero katika Wilaya ya Mvomero, kilio cha ardhi kilisikika tena, na safari hii, kilimgusa Waziri Mkuu wa kipindi chote cha miaka 10 ya Awamu ya Tatu, Sumaye anayemiliki ardhi kijijini hapo.

Mmgombea wa udiwani wa CCM, Selemani Shomari maarufu Siri, alieleza wazi kero inayowasumbua ni shamba la Sumaye.

“Tunataka shamba la Mhe. Sumaye lirudi katika Mamlaka ya Mji Mdogo kwa sababu lipo katikati ya mji,” alisema Shomari na kushangiliwa na maelfu ya wakazi wenzake wa mji huo wa Mvomero.

Kama ilivyokuwa katika majibu yake kwa wananchi wa Mvumi, Rais Kikwete alisema, “niachieni nihangaike nalo, nilijue vizuri na kupata majawabu stahili, kwa sababu ardhi ikishatolewa na serikali, kubadili ni lazima ufuate taratibu.”

Shamba la Sumaye alilolinunua akiwa madarakani, linadaiwa lilikuwa la Ushirika wa Wakulima wa Mvomero, uhamishaji wa miliki yake unadaiwa kwamba haukufuata utaratibu husika. Sakata lake lilivuma sana mwaka 2005
 
Jeetu Patel....! mageni katika nchi anawakodisha wenye nchi ardhi...kwa Tsh 50,000????

HAKUNA TUSI KUBWA KAMA HILI...! SERIOUS...!!!!!!!!

KISA ATI NI MFADHILI WA CCM
 
Wenye nchi wa Mvumi na Mvomero wanapata jeuri hii ya kumtetemesha Jakaya Kikwete kwa sababu wanajua fika kuwa amebanwa kisawasawa na jeshi la Ukombozi wa pili wa Tanzania ukiongozwa na CHADEMA na DR SALAA na wapo wazalendo ambao wamejitolea kushiriki mapambano ya kukikomboa nchi kutoka makucha ya MAFISADI wa CCM na vikaragosi wao. Vibaraka wa mafisadi Tandale One na wenzako mpo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Endeleeni kuganga njaa sisi tunawakomboa watanzania kidogo kidogo.
 
Back
Top Bottom