singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
kweli kabisaKama wananchi wanahaki ya kumiliki serikal iwaangalie kwa kutowanyanyasa.
Kama wananchi wanahaki ya kumiliki serikal iwaangalie kwa kutowanyanyasa.
Kwa kweli kuna marehemu wawili maarufu Gavana Balali na Prof kairuki hawa watu walijitwalia maeneo makubwa sana. Sijui wizara inaangaliaje maeneo ya marehemu hawa
Ni haki yako kumiliki shamba sio pori.Kama umelilima na lina mazao hakuna kiyama hapo.Lakini kama ni pori huwezi kusema unamiliki shamba.Shamba na pori ni vitu viwili tofauti.Ndio maana Hata magufuri alisema atayachukua mapori yote na kuyagawa kwa wananchi.Hatachukua mashamba bali mapori.Mashamba yanajulikana hata na mwehu akipita anasema lile ni shamba.Lina mazao yamestawi nk
Wako watu kibao wanamiliki mapori sio mashamba hayo ndio majipu yatakayotumbuliwa
Ushauri wa bure kama una pori liendeleze chapchap au uza vipande vipande haraka haraka hata kwa bei ya kutupwa kuliko kula hasara kabisa
Shamba kwa ajili ya ufugaji inakuaje? Mpaka liwe na mazao? Shamba la kuchimba mawe, kifusi na kokoto ni vipi? Inabidi lilimwe ndo lihesabike shamba?
Huyu waziri ntamwelewa akikomesha uvamizi wa ardhi Kinondoni.
Serikali na taasisi zake pamoja na mashirika ya umma yamejilimbikizia maekari kibao ambayo ni mapori tu. je hili move inawahusu pia?
Wananchi wenye mawazo endelevu tupo na tunainvest for future kama serikali inavyofanya.. sasa kwa nini itulazimishe kuwa mamburula wakati tuko smart tu!!!?? Ni muhimu serikari yenyewe iheshimu utawala wa sheria. kama mtu anamiliki ardhi kihalali ni muhimu serikali iheshimu zile hati zake. Na kama inalihitaji hilo eneo basi ikae nae huyo mmiliki ilinunue kihalali kwa bei ya soko. Isiwafanyie uhuni wananchi wake kwa visingizio visivyo na mbele wala nyuma!!
Kuna siku tutaambiana mwenye nyumba zaidi ya mbili anyang'anywe!! Mwenye mabasi zaidi ya 3 anyang'anywe!! What's the difference? Coz kama huyo mwenye shamba au eneo alilipata kihalali kosa liko wapi? Serikali ikilitaka ifike dau ilinunue tu na sio kutishatisha wananchi wake wanaowekeza kwenye ardhi bila sababu za msingi.
Hawawezi kugusa shamba lenye hati, ni yale mashamba ya kijiji, yasio na hati.Hakuna kitu kama kiama kwa mwenye shamba zaidi ya 50 acres, issue ni kama mwenye shamba hajaliendeleza
Ina maana ukiwa na Hati alafu haujaliendeleza linaachwa? Nafikiri Hati hiyo inafutwa mara moja na Rais!Hawawezi kugusa shamba lenye hati, ni yale mashamba ya kijiji, yasio na hati.
Acha ujinga na soma kwanza vizuri na uelewe kilichoandikwa kabla ya kujibu!
Habari inasema wenye mashamba yasioendelezwa, unaelewa kwanza maana ya hiyo sentensi yenye neno ,,yasiyoendelezwa"?
Mbona umepanic bro?? Ni mhanga?