GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,464
- 108,619
Leo nitawaomba tu mniache niteme " nyongo " kwani hasira niliyo nayo hata mkinipa " Kichuri " haitapungua.
Kuna Watu nadhani wamepewa dhamana ya kuwajibika ipasavyo kwa Wananchi lakini kwa hakika wanachokifanya au kutufanyia nadhani hata Shetani hawezi kutufanyia japo anatutawala " kimtindo ".
Haiwezekani kabisa barabara ambayo imeharibika vibaya sasa inakaribia hata mwaka lakini Wahusika wakuu wamenyamaza tu na wala hawachukui hatua yoyote ya basi hata tu kuirekebisha kidogo huku wakijipanga kwa matengenezo kamili.
KERO iliyopo sasa katika ile barabara ya kuelekea Kituo cha Mabasi kipya cha SIMU 2000 ama hakika haivumiliki. Magari ya Watu hasa " Madaladala " kila kukicha yanaharibika pale huku foleni zisizo na miguu wala kichwa zikitokea kila mara hadi kutusababishia sisi Watumiaji usumbufu mkubwa sana.
Hivi inachukua muda gani au gharama ipi kuamua tu kuitengeneza? Nimeyaweka hapo Makundi matatu Wenye Mamlaka na Kituo, Watu wa TANROADS na hawa wadau wengine wa SUMATRA kwakuwa Wao ndiyo walengwa wakuu katika hii KERO lakini cha kushangaza sana na kutia HASIRA hawa Watu kutwa tunakutana nao katika " Gambe " na " Gesti " kila mara tukistareheka na huku wengine wakinenepeana kama Matenki ya Maji kwa Pesa za Ushuru wa hawa hawa wenye magari ( Madaladala ) lakini hakuna hata mmoja wao mwenye uchungu na hawa Wanaoteseka na hiyo barabara ili kuwatengenezea miundo mbinu yao ili wafanye Kazi zao bila matatizo.
Jamani naomba kwanza niishie hapa nizitulize hizi hasira zangu kwani naona zinanizidi. Ila kwa mwenye " machungu " kama yangu haya juu ya Kituo cha Mabasi cha SIMU 2000 akaribie katika " kutiririka " kihasira hasira.