Wenye mamlaka, vyanzo hivi vinaweza kuwa suluhisho au sehemu ya suluhisho la upatikanaji wa fedha kwa ajili ya HESLB

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,012
144,371
Niliwahi leta mada hapa Jukwaa la Siasa nikipendekeza vyanzo maalumu kwa ajili ya kukusanya fedha za kupeleka Bodi ya Mikopo ili kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la upatikani wa mikopo kwa ajili ya kugharamia elimu ya juu.

Mada yenyewe ni hii hapa chini ingawa mods waliipeleka Jukwaa la Elimu wakasahau kuwa wanasiasa ndio watunga sera na ndio watunga sheria hivyo hii mada ilikuwa inawahusu zaidi.

Mada hii inaweza kuboreshwa kuongeza vyanzo vingine na hivyo tukawa tumeisaidia serikali kupata vyanzo mbadala na mahususi kwa ajili ya Bodi ya Mikopo.

Hivi vinaweza kuwa vyanzo mahususi vya mapato kwa ajili ya Bodi ya Mikopo
 
Mawazo mazuri, nami hapo kwenye ruzuku kwa vyama vya siasa ndo pa kuanzia. Wale wabunge wanapewa mshahara na posho nyingi, wanachama wa hivyo vyama ndo wabebeshwe huo mzigo siyo kutusumbua hata tusio na vyama.
 
Wakifanya kama unavyosema,hlf kila mwanafunzi aliyepata admission aombe mkopo,kama unajua hesabu kwa haraka haraka unaona kabisa hata 5% ya wanafunzi hawafk watakao pata mkopo. Kwa kuanza tu mwanafunzi mmoja huwa anatumia zaidi ya mil 4 kwa mwaka
 
Wewe badala ya kubuni vyako unahoji hivi nilivyotoa wakati nimesema wazi vyanzo hivi pekee vinaweza kupunguza tatizo tu na sio kulimaliza kabisa.
 
Unakata wafanyakazi ambao ni wanufaika wa Bodi ya mikopo asilimia 15 ya mishahara yao midogo alafu unashindwa kuwakata wabunge walau asilimia 10 ya posho ya kukaa (sitting allowance)?!

Hivi nchi hii tunawaza sawasawa kweli?
 
Wewe badala ya kubuni vyako unahoji hivi nilivyotoa wakati nimesema wazi vyanzo hivi pekee vinaweza kupunguza tatizo tu na sio kulimaliza kabisa.
Ndio maana kila siku tunakushauri uache kubeza miradi ya miundombinu inayofanywa na serikali, hiyo n zaid ya mikopo tosha kwa wanafunzi wote in a long run
 
Wakifanya kama unavyosema,hlf kila mwanafunzi aliyepata admission aombe mkopo,kama unajua hesabu kwa haraka haraka unaona kabisa hata 5% ya wanafunzi hawafk watakao pata mkopo. Kwa kuanza tu mwanafunzi mmoja huwa anatumia zaidi ya mil 4 kwa mwaka

Haitonshi?

5% ya makosa ya barabarani kwa mwaka bei gani

5% ya hizo posho za serikali alizozisema kwa mwaka kiasi gani?

Reduction ya Ruzuki kwa mwaka kiasi gani?

By the way hata kama hazitoshi hebu toa mchango wako tuone kifanyike kipi hasa kuondoa hili tatizo
 
Ndio maana kila siku tunakushauri uache kubeza miradi ya miundombinu inayofanywa na serikali, hiyo n zaid ya mikopo tosha kwa wanafunzi wote in a long run
Wewe ni zero kichwani! Kushauri miradi hiyo ifanywe kwa awamu ndio kubeza? Mngeifanya kwa awamu wanafunzi wangekosa mikopo?

Mnanunua ndege sita kwa muda mfupi tena kwa kulipa cash alafu mnakuja na vigezo vyenye lengo la kuwanyima wanafunzi mikopo! Hii wewe unaona sawa tu!!!

Miaka zaidi ya 50 tangu tupate uhuru bado tu mnatenga bajeti ya kukimbiza mwenge huku watoto wa masikini wanakosa mikopo!Hii kwako wewe unaona ni sawa tu!!

Ovyo kabisa!!
 
Back
Top Bottom