Wenye makosa madogo madogo watatumikia kifungo cha nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenye makosa madogo madogo watatumikia kifungo cha nje

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Apr 15, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  KATIKA hali ya kuonekana kuna msongamdano wa wafungwa gerezani hali iliyopelekea kuwea keo serikali imeamua wafungwa hao kutumikia kifungo cha nje ili kuepuka msongamano huo.

  Wafungwa hao watatumikia kifungo cha nje adhabu zao kwa kufanya kazi za jamii huku wakiishi uraiani.

  Mpango huo ulio chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeendelea kuwapatia mafunzo maafisa wake wa huduma kwa jamii ili waweze kusimamia sheria zinazotoa fulsa kwa wafungwa hao kutumikia adhabu zao uraiani.

  Mkurugenzi wa Huduma kwa Jamii wa Wizara hiyo, Onel Malisa, alisema mbali na kupunguza msongamano wa wafungwa, pia adhabu hiyo itasaidia kupunguza gharama kubwa za kuendeshea magereza.

  Wafungwa watakaotumikia adhabu hiyo itawahusishawaliohusika na makosa ya kama ya wizi wa kukwapua, wanaoiba kuku, wenye kutoa lugha ya matusi na nyingine nyingi ndogondogo zinazoendana na hizo.

  Alisema wafungwa hao watapangiwa kazi kama za kutunza mazingira katika vyanzo vya maji, ujenzi wa shule, kufagia barabara, kuzibua mitaro ya maji machafu, kupangiwa kufagia ofisi mbalimbali kwea kipindi atakachopewa kwa kusimamiwa na maafisa wa huduma kwa jamii nchini.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4351498&&Cat=1
   
Loading...