Wenye makosa madogo madogo watatumikia kifungo cha nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenye makosa madogo madogo watatumikia kifungo cha nje

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Apr 14, 2010.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wenye makosa madogo madogo watatumikia kifungo cha nje

  Wednesday, April 14, 2010 11:09 AM
  KATIKA hali ya kuonekana kuna msongamdano wa wafungwa gerezani hali iliyopelekea kuwea keo serikali imeamua wafungwa hao kutumikia kifungo cha nje ili kuepuka msongamano huo.

  Wafungwa hao watatumikia kifungo cha nje adhabu zao kwa kufanya kazi za jamii huku wakiishi uraiani.

  Mpango huo ulio chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeendelea kuwapatia mafunzo maafisa wake wa huduma kwa jamii ili waweze kusimamia sheria zinazotoa fulsa kwa wafungwa hao kutumikia adhabu zao uraiani.

  Mkurugenzi wa Huduma kwa Jamii wa Wizara hiyo, Onel Malisa, alisema mbali na kupunguza msongamano wa wafungwa, pia adhabu hiyo itasaidia kupunguza gharama kubwa za kuendeshea magereza.

  Wafungwa watakaotumikia adhabu hiyo itawahusishawaliohusika na makosa ya kama ya wizi wa kukwapua, wanaoiba kuku, wenye kutoa lugha ya matusi na nyingine nyingi ndogondogo zinazoendana na hizo.

  Alisema wafungwa hao watapangiwa kazi kama za kutunza mazingira katika vyanzo vya maji, ujenzi wa shule, kufagia barabara, kuzibua mitaro ya maji machafu, kupangiwa kufagia ofisi mbalimbali kwea kipindi atakachopewa kwa kusimamiwa na maafisa wa huduma kwa jamii nchini.

  Source:Nifahamishe
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ni afadhali wameliona hilo, lakini hili ni sehemu tu ya tatizo kwani hii itahusisha wafungwa. Nionavyo mimi idadi kubwa ya watu wanaojaza mahakama ni mahabusu nadhani mahakama ingejipanga upya na kuangalia kuhusu dhamana. Kesi ya matusi dhamana inayimwa, mshtakiwa anakaa mahabusu miezi mitatu, kesi ikisikilizwa na kuisha adhabu faini shs 50,0000/=. Gharama ya kumuweka miezi yote hiyo ni zaidi ya hela ya faini. Uzururaji, kukamatwa na gongo, bangi, wapiga debe, wadada wanaoshikwa usiku na polisi, wauza chips na makosa yote chini ya sheria ndogo za jiji, hawa wote hawakutakiwa kuwekwa mahabusu.

  Kuna haja ya kuangalia hili kwa undani zaidi, je ni lazima makosa mengine watu wasipewe dhamana????
   
Loading...