Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,526
3,801
Hakuna mtu alikuwa na dingi mkali kanda ya kati kama mimi.

Yani Tabora, Dodoma na Singida nna uhakika mzee wangu ndio alikuwa mzee mkali kuanzia miaka ya 1976 mpaka alipofariki mwaka 1997.

Mzee alikuwa fundi umeme, ndani alikuwa na nyaya za umeme za kutosha siku ukifanya kosa anachukua nyaya anaikunja mara mbili anaanza kukupa kichapo. Ukishika umefuta.

Maumivu ya nyaya ya umeme yasikie ndugu, ya mkanda yanasubiri sana. Maumivu ya nyaya nadhani ilibaki kidogo yafikie kwenye maumivu ya mapenzi (hahaha, joke)

Tulikuwa na choo na majani, siku moja nikawa nachezea kibiriti nikachoma choo then moto ukaenda kugusa kenchi za nyumba ashukuriwe Mungu majirani waliwahi kabla moto haujapamba lakini aliporudi mzee chamoto nilikiona, nilikuwa siwezi kukaa wiki nzima mfululizo kalio zimevimba balaa.

Pamoja na yote lakini nakukumbuka sana mzee wangu (RIP).

We mzee wako alikuwa mkali? Tupe story
 
Mzee alikua anasema kama unajiona upo vizuri njoo tuzipange.

Alikua hapendi mtu anyoe kipara, kaka yangu akawa mbishi siku hiyo karudi home na kipara. Mzee akamwambia kimbia ukiona upo mbali sema tayari.

Jamaa akakimbia mzee anaona mdau anasogea tu hasemi tayari, akamuungia. Dakika kadhaa mbele tunaona kaka anarudishwa kabebwa begani.
Kufika home akaambiwa tuzipange, ghafla jamaa kapiga magoti analia anaomba msamaha.

Mzee akamwambia adhabu yako utakua unapaka kiwi kichwa hadi nywele ziote.
 
Dingi ya jamaang, marehem mzee kadege alikua OCS au OCD kpnd hicho, kulala sero, kutandkwa na msauz/fimbo itumiwayo kuadhb waarfu polic ilikua kawaida kwa jamaang na kakazake.

Sku moja mwaka 2001 katka kucheza cheza tukiwa na kbert cha ges, ambach jamaang uyo alimwbia mzee wake uyo uyo, tuliwasha moto fensi ya almashaur ilyokua imeungana na fensi ya hosptal ya wilaya, fens ilkua imepgwa seng'enge uku ikwa imepandwa mit na maua mbalmbal, meng yalkua yamekauka kwan ilikua n kiangaz.

Nasema iv bila watu kuingilia kat na kumchomoa jamaang mikonon mwa yule mzeee naamn jamaang angekua marehem leo, kipgo alchopata ilbd tu alazwe.

Pia nashukuru Mungu jithada za raia wema walfanikwa kuuzima moto ule japo ulileta madhara kias, miaka iyo zimamoto ilkua mkoan tu uku wilayan hazkuepo kabsa
 
Mi nadhani Mzee wangu ndo mkali kuliko wote Tz.

Nakumbuka mwaka 2002 nilikuwa napenda sana kusikiliza mikanda ya kaseti, siku moja redio ikawa imekorofisha nikaona isiwe taabu nikachukua bisibisi nikaifungua, nilivyoifungua ndo nikawa nimeharibu zaidi alivyorudi jioni kutoka kazini aliyeharibu redio nani nikatajwa mimi nilipewa adhabu ya kula majani pamoja na maziwa pamoja na fimbo kumi na nne kwa muda wa siku mbil.
 
mzee wangu hakuwa mkali tatizo lilikua mimi, sidhani kama pamepata kutokea mtoto mtundu kama mimi ebufikiria nimefanya attempt mbili za kumuua dogo ikiwemo kumnywesha sumu ya kuoshea ng'ombe nikijua maziwa,nilinusurika kuchoma nyumba, though sikuanajua nlichokua nafanya sababu ya utoto lakini mzee alikua akininyoosha kisawasawa hakika nilichezea kipigo btw R.I.P Baba
 
Mwaka 99, enzi hizo simu ya mezani, alikuja mgeni akaomba simu apige hapo simu inakaa chumbani, nikamwambia dingi mgeni anaomba simu, dingi akaguna tu nikajua kakubali nikatoa simu mgeni kaongea alivoondoka mweh!!!!
Nlichezea kichapo heavy yani mvua ya stiki..... Apumzike kwa amani mdingi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom