Wenye Kujua, Je Mwaka Mpya Huanza Lini Haswaa?

Ndikwega

R I P
Feb 1, 2012
5,979
5,527
Salaam Wanajukwaa

Kuna jambo najiuliza nalo ni Kujua je mwaka mpya kwa kila mwaka huanza lini kiuhalisia?
Nilivyokuwa nasoma Historia shuleni niliambiwa kuwa Miaka yoote kabla ya Kuzaliwa Yesu Kristo huwa inaandikwa BC maana yake Before Christ. Mfano 2000BC, maana yake ni kuwa miaka elfu 2000 kabla ya Kristo.

Vivyo hivyo baada ya Kuzaliwa Yesu Kristo inageuka na kuanza Kuandikwa After Christ au Anno Domino (AD)- I stand to be corrected). Mfano 100 year AD maana yake miaka 100 baada ya Kuzaliwa kwa Kristo. Na ndipo haswa ilipoanza Kuhesabiwa yaani Kuanzia Moja na kuendelea kwa upande was miaka.

Sasa hoja yangu ni Kuwa, Si kweli Kuwa Yesu Kristo alizaliwa Disemba 25, maana hayo ni Mapokeo tu ya Wanadamu, yaani walipanga siku itakayofaa Kusheherekea Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa kujipangia Christmas iwe tarehe tajwa hapo juu kutoka kwa Mfalme Constantine wa huko Roma Italia. Sasa je Tunaanzaje kuhesabu Mwaka tarehe na Mwezi kwa Kutumia misingi ya Kusema AD ama BC.

Ufafanuzi wenu ni muhimu.
Karibuni.
 
Back
Top Bottom